Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akizungumza na wakazi wa Gongolamboto (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kuwaona waathirika wa milipuko ya mabomu iliyotokea katika kambi ya JWTZ Gongolamboto leo jijini Dar es salaam ambapo ametoa wito kwa mamlaka zinazohusika na ugawaji wa misaada kuhakikisha kuwa misaada hiyo inawafikia walengwa.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia moja ya nyumba iliyoteketea kwa moto kutokana na milipuko ya mabomu eneo la Majohe leo jijini Dar es salaam.
Wajasilia mali wa kikundi cha SEUMA kutoka Segerea jijini Dar es salaam wakimkabidhi Waziri mkuu Mizengo Pinda msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa milipuko ya mabomu ya Gongolamboto leo jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wa nne kulia) Pinda akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw.Gabriel Fuime(wa sita kushoto) kuhusu upokeaji na uhifadhi wa misaada mbalimbali inayotolewa kuwasaidia waathirika wa mabomu Gongolamboto inavyohifadhiwa na kugawiwa kwa walengwa husika leo eneo la Shule ya Sekondari Pugu jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Bw. Reginald Mengi akikabidhi kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda msaada wa tani 17 za vyakula mbalimbali na hundi ya shilingi milioni 15 kwa ajili ya kutoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu zao kutokana na milipuko ya mabomu iliyotokea eneo la Gongolamboto.Wasanii wa Muziki na Filamu wakipita mbele ya Waziri mkuu Mizengo Pinda na kuwasilisha michango mbalimbali ya fedha na vitu vyenye thamani ya shilingi milioni 76 waliyoipata kutokana na tamasha walilolifanya kuchangia waathirika wa Mabomu katika eneo la Gongolamboto jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia)akizungumza na baadhi ya familia za waathirika wa milipuko ya mabomu eneo la Majohe leo jijini Dar es salaam na kuwahakikishia kuwa serikali itafanya kila linalowezekana kuwasaidia.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapa pole baadhi ya wananchi wa Majohe ambao nyumba zao ziliharibiwa na mabomu yaliyolipuka katika kambi ya JWTZ ya Gongolamboto hivi karibuni wakati alipoeatembelea leo.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Just a thought, no offense. Michuzi, I would suggest that you either post using swahili language or english language. The mixing in a way, is depleting seriuosness of the message that the posted pictures are intended to project. As much fun as you may want to play with your post, you got to keep it focused and professional. You came up with the blog, I give you a big up for that, you do not give some of your readers a reason to diss your blog.

    ReplyDelete
  2. kwa kweli Mh. Mengi mungu akupe maisha marefu sanaaaaaaaa maana unatoaga misaada kila siku,kuna matajiri wengi lakini wengine hawana moyo wa kutoa kama wewe mungu akupe nguvu uishi milele.

    ReplyDelete
  3. kutoa sadaka kama hizi sio lazima ujitangaze. Labda kwa sababu ya kumbukumbu. Lakini unatakiwa ukitoa kwa mkono wa kulia wa kushoto usijue.

    ReplyDelete
  4. kwa kweli wafanya biashara na wasanii wapewe shukrani kubwa kwa mchango wao ambao wautoa kwa waathirika hao sio serikali ambayo naona viongozi kazi yao ni kutembelea na kuuza domo wakati wao ndio chanzo cha hili tatizo hatutaki kuuziwa domo tumewaweka katika madarka kutupa ufafanuzi kwa vitendo nakutuhakikishia usalama wetu hii ni mara ya pili hii hali inawtokea wanainchi na serekali haiwezi hata kuwajibisha wahusika wakati watu wanakufa wamepoteza makazi jamani serikali tafadhali msijisahau kiasi hicho tuangalie yanayotokea kwa wenzetu na je uvumilivu huu wa wanainchi mpaka lini tunaelewa nchi yetu ni maskini lakini japo kidogo tuoneshe tunajali sio kuwapa wabunge mil 90 wakati wengine hawana hata hela ya kula wakati wanalipa kodi kwa kweli wanainchi wapewe kipao mbele kuliko kitu kingine chochote kwa kweli vinatia imani.

    ReplyDelete
  5. matajiri wetu wengi hasa wenye asili ya kihindi hawatowi msaada au zawadi yoyote bila kuwepo televisheni na wana habari wa magazeti yote ya ulimwenguni(tanzania)
    nimekumbuka kule zanzibar yule mkereketwa wa ccm maarufu bw raza aliahidi kuoa msaada hospitali ya mnazi mmoja baada ya kugundua kuwa hakutokuwa na waandishi wa habari hasa televisheni zanzibar akagoma hata baada ya kubembelezwa sana hakukubali na wale jamaa wa televisheni walipoombwa kwenda hospitali kuchukua japo mkanda mtupu ili aridhike pia nao wakagoma na wakasema kama anataka kutoa hivyo vitanda atowe kama hataki basi akalalie mwenyewe kwani tumechoka kurekodi utowaji zawadi hata wa visu viwili vya jikoni anataka kamera iwepo.
    sasa kuhusu bw mengi mimi sielewi undani wake lakini ningemshauri aunde kamati ya kushughulikia na kuwasilisha michango yake na awe makini katika uteuzi kwani uaminifu ni mdogo sana kwenye nchi yenye dhiki kama yetu huu ni ukweli na anaweza kufuatilia kwa njia za siri ili kufahamu kama misaada imewafika walengwa badala ya kuwa yeye ndio muhusika mkuu kila siku iko haja ya kubadili mfumo hili ni ombi au wazo.

    mdau.
    kansas,usa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...