Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wananchi wakati akitoka makao makuu ya wizara ya Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam mara baada ya ziara yake ya kikazi wizarani hapo ambapo alifanya mazungumzo na wafanyakazi na viongozi na kutoa maelekezo na miongozo ya kazi. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hivi ankal huwa unamtumia JK maoni yote yaliyo critics to him, kama unafanya hivyo hiyo ni nzuri sana angalau anasoma maoini ya watanzania na watu wanafikiria nini kuhusu utendaji wake wa kazi. Kwani tangu tulalamike japo hakupost hizo critics za kuhusu kwamba JK muda wote anatumia katika mwezi kwa safari za nje na kutumia hela za walipa kodi kwa fujo sasa amejirekebisha angalau ameanza kutembelea wizara mbalimbali na kujua matatizo yanayowakabili. Anachotakiwa kufanya sasa ni kutembelea miradi mbalimbali inayosimamiwa na kila wizara na kuona imefikia wapi kwani siku zinakimbia na miaka 5 itapita atajikuta hajatimiza ahadi yoyote. Vile vile asisahau kuwatembelea wapiga kura wake na kuona ni jinsi gani walivyo na hali ngumu ya maisha na anatakiwa kutatua matatizo basics yale makubwa amwachie successer wake.
    Aasante kama utamfikishia ujumbe huu hauna haja ya kupost hewani kwani nilikuwa ninaanza kukuchukia na kusema kwamba haufikishi kilio chetu wananchi kumbe una print na kumpelekea mwenye ikulu. Tunashukuru amebadilika angalau mwezi huu anaumaliza akiwa nyumbani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...