Mchungaji Maximiliani Machumu Aka (Mwanamapinduzi) ambaye ni mwimbaji wa muziki wa injili akiongea na waandishi wa habari leo katika Mgahawa wa Chines uliopo Jengo la Kitegauchumi jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akitoa shukurani kwa watu waliochangia ujenzi wa kituo cha watoto yatima cha (HUIWA) na kuelezea lengo la kufanya matamasha mengine mikoani kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kituo hicho kitakachojengwa jijini Dar es salaam katika picha kulia ni mshauri wa Mchungaji huyo Bw.Geovan Festo.

HOTUBA YA MCHUNGAJI MACHUMU KWA WAANDISHI WA HABARI

Ndugu waandishi wa habari, awali ya yote napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa viongozi waheshimiwa wabunge waliohudhuria katika tamasha langu la uzinduzi wa albam ya Bonde la Kukata Maneno, niliyoizindua kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Machi 6/2011 mgeni rasmi akiwa Mh. Edward Lowasa.

Siwezi kuwataja wote waliofanikisha uzinduzi wangu, lakini nitakuwa sina shukurani endapo sitawataja hawa wafuatao, kwanza Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Edward Lowasa, ambaye katika uzinduzi huo ambao uliambatana na kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto yatima cha Huduma ya Injili Kwa Watoto (HUIWA), alichagia shilingi milioni 10 na kusaidia sana hamasa kwa watu mbalimbali kuchangia katika harambee hiyo.

Pia napenda kuwashukuru Mh. Beatrice Shelukindo Mbunge wa Kilindi, Vick Kamata Mbunge wa Viti Maalum CCM, Mchungaji Josephat Gwajima kanisa la Glory of christ, na wadau wote wa muziki wa injili ambao walichangia kwa kiwango kikubwa kufanikisha kwa uzinduzi huo, pamoja na kuchangia fedha kwa ajili ya kituo hicho cha (HUIWA) ambapo fedha taslimu pamoja na ahadi zilipatikana shilingi milioni 68.

Katika kuhakikisha kwamba kituo hicho kitakachogharimu shilingi milioni 120 kinakamilika kwa haraka zaidi, tumepanga kufanya matamasha mengine kwa ajili ya kukusanya fedha zaidi, ambapo tutafanya katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Mbeya na Tanga. lengo likiwa kukamilisha ujenzi wa kituo hicho kitakachogharimu shilingi milioni 120 katika hatua za awali, ambacho kwa sasa maandalizi ya ujenzi wake yameanza kwa kumpata mtaalam ambaye anafanya tathmini ya ujenzi wa kituo kitakavyokuwa.

Lakini pia tunatarajia kutoa albam inayoitwa “Nani atakwenda badala yake”, ambayo ina nyimbo nane(8) zinazoelezea na kuhamasisha watu, makanisa na taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali kusaidia na kuwajali watoto yatima popote walipo nchini, ili kukomboa kizazi hiki ambacho kiko katika mateso makubwa katika jamii na kuisaidia serikali katika majukumu yake ya kuwasaidia wananchi.

Mchungaji Maximilian Machumu amesema, atawawekea mikono ya baraka na kuwaombea wale wote waliotoa michango yao, katika kufanikisha ujenzi wa kituo hicho ili pale walipopungukiwa mungu azidi kuwaogezea katika vipato vyao na kuwabariki, amemaliza Mchungaji Maximilian Machumu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...