Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar mapema leo asubuhi kuhusu kushiriki kwa kampuni hiyo kwenye maonesho ya Wiki ya Maji iliyoanza leo kwenye viwanja vya Nyamagana, jijini Mwanza. Kulia ni Meneja Miradi Maalum wa TBL, Emma Oriyo.

Kwa niaba ya Kampuni ya Bia Tanzania napenda kutangaza rasmi kuwa kampuni hii itashiriki kwenye maonyesho ya wiki ya maji yaliyoandaliwa chni ya wizara ya maji kwenye viwanja vya Nyamagana mkoani Mwanza.

Kampuni ya Bia Tanzania imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye maswala mazima ya maji. Akiongea wakati wa maongezi na waandishi wa habari bi. Editha Mushi ambaye ni meneja mawasiliano na uhusiano wa jamii alisema “Kufuatia mipango ya kampuni mama ya SABMiller, viwanda vyetu vyote vimewekewa mitambo muhimu ya kuchuja maji kabla ya matumizi na baada ya kutumika.

Pamoja na kuwa na mitambo hii muhimu kwa kuchuja maji, Kampuni ya Bia Tanzania imeweza kupunguza matumizi ya maji kutoka lita 8 za maji katika utengenezaji wa lita 1 ya bia mpaka kufikia matumizi ya lita 5 – 5.5 kwa lita 1 ya bia.

Tunaona mafanikio katika hili kwani ni sehemu ndogo sana imebaki kufikia vipimo vya kimataifa ambavyo ni kutumia lita 3 – 3.5 kutengeneza lita 1 ya bia. Mfano kiwanda chetu cha Mbeya ni mfano mzuri sana kwani hata teknolojia zinazotumika kuendesha kiwanda hicho ni za hali ya juu katika uzalishaji”

Aliongeza, zaidi ya hayo pia asimilia 70 ya fedha zinazotengwa kwa ajili ya kusaidia jamii zinalenga kwenye kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama kwenye mataasisi na jamii kwa ujumla”. “Mpaka sasa, kwa upande wa kampuni tumeweza kuekeza kwenye miradi mbali mbali ya maji kupitia mradi wetu mkubwa wa HAKUNA MAJI,HAKUNA UHAI.

Tumeungana na kikundi cha MSABI kilichopo Ifakara Morogoro kwenye kuendeleza miradi ya maji kwenye vijiji vitano, pia tuliweza kuweka mtambo na hifadhi za maji kwenye shule ya msingi Daraja Mbili, wilaya za Kitunda na Ludewa, Chuo kikuu Huria, Hospitali ya Ocean Road, ujenzi wa visima vya maji kwenye Shule ya Msingi Magomeni ”. Bado tunaendelea kupokea maombi kwani huu ndio muelekeo wa kampuni kwa sasa”

Nae Meneja wa miradi maalumu bi Emma Oriyo alisema, “ Ukame ni tatizo kubwa lililopo mbele ya kila bara hapa Tanzania, ni wajibu wa serikali, mashirika na hata wananchi kushirikiana na kuhakikisha kwa pamoja tunaitikia lengo la kupambana na ukame unaotabiriwa ifikapo mwaka 2025 na pia kuokoa jamii ya Tanzania”, Aliongeza.

Ushiriki wa Kampuni ya bia kwenye maonyesho haya ni kuelemisha serikali na jamii mzima juu ya juhudi kampuni yetu inafanya na kuunga mkono jitahada za serikali katika kuhakikisha kila mtanzania anaweza kuapata maji yaliyosafi na salama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Uncle hee sikujua tanzania ina "mabara" Je yako mangapi?Naona meneja wa miradi maalumu kama ajachapia basi mimi ndio sijiui.



    Mdau wa mada zako.

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Emma, Huko Zain sijui Airtel walikupotezea muda tu chapa kazi mama uwezo unao.

    ReplyDelete
  3. Namuunga mkono Mdau wa kwanza hapo juu,nimesoma na inaonekana kuna tatizo kidogo.Hakuna mabara Tanzania...!.Lakini Ujumbe tumeupata vizuri tu na ongera kwa TBL na wajumbe wao kwa kupambana na tatizo la maji.

    Nina swali kwa wadau wote,hivi Tanzania water usage per household ni kiasi gani? Na maji safi katika viwango vya Tanzania ni vipi?Nitakuwa Ipalamwa Village, Iranga mwezi ujao kwa rain water catchment project.

    Mdau kutoka Uk

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...