Mabingwa wapya YANGA Mabingwa wastaafu SIMBA

HIYO IMEKUJA KUFUATIA TOFAUTI YA MAGOLI YA KUFUNGA NA KUFUNGWA BAADA YA WOTE KUWA NA POINT SAWA 48. Yanga wamefunga magoli 32 na wamefungwa 7 (32-7=25) na Simba wamefunga magoli 40 na wamefungwa 16 (kama matokeo ya leo ni 4-0) hivyo (40-16=24).


Goli la kwanza la Simba SC leo dhidi ya
Wana Yanga wakianza mchakamchaka
kuelekea Jangwani kama kawa
Mashabiki wa Simba wakiwa
wameduwaa baada ya gemu


Yanga leo wameifunga Toto Africa mabao 3-0 uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na kufanikiwa kuwavua ubingwa Simba SC ambao pamoja na kuifunga Maji Maji ya Songea bao 4-1 katika mchezo wao wa mwisho uwanja wa Uhuru jijini Dar, wamejikuta wanatema ubingwa kwa tofauti ya kagoli kamoja. Yanga wamemaliza ligi hii ya Vodacom wakiwa na magoli 25 ya kufunga wakati Simba wana magoli 24 ya kufunga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Common mwananchiApril 10, 2011

    Hongereni Yanga, Simba tulizembea wenyewe katika mechi mbili za mwisho na kwenye soka ukifanya makosa wenzako wanatake advantage.

    Hata hivyo kwa kusaidia tu sio kweli kwamba Yanga wamemaliza ligi wakiwa na magoli 25 ya kufunga na Simba wana 24. HIYO NI TOFAUTI YA MAGOLI YA KUFUNGA NA KUFUNGWA. NA HII IMETUMIKA BAADA YA WOTE KUWA NA POINT SAWA 48.

    Yanga amefunga magoli 32 na amefungwa 7 (32-7=25) na Simba wamefunga magoli 40 na wamefungwa 16 (kama matokeo ya leo ni 4-0) hivyo (40-16=24). Inauma lakini ndio mchezo. Hongereni Yanga.

    ReplyDelete
  2. michuzi spain pia walishinda world cup kwa kagoli hako hako unako kaita kamoja.

    ReplyDelete
  3. Kwa kweli Mungu ni mkubwa sana. na haki ya mtu haidhulumiwi. pamoja na wenzetu kuzidisha maneno na fitna mbalimbali kuwa wao iwe isiwe ndio mabingwa lakini wameishia maneno. sasa wajipange kwa ajili ya mwakani.Ila tunawapa pongezi maana tunajua viongozi wanapiga hesabu ya Mil 300 za Mazembe na za Ushindi wa 2 Ha ha ha ha.

    Yanga nawapongeza sana kwa mafanikio haya. ila viongozi sasa ni wakati wa kumaliza tofauti zilizokuwepo na kuitisha mkutano ili kama kuna matatizo yarekebishwe na kumalizwa. then tujipange kwa ajili ya hatua za mbele.

    Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki YANGA AFRICA.

    ReplyDelete
  4. Huleeeeee yaaaaaaaanga!!!! safi saaaaana simba walizembea wenyewe mechi za mwisho.... leo ni biaaa!!! fosterz, na whisk kama kawa za kumwaga tuu plus arsenal kushinda leoo eeeeeh!! simba poleni saaaana

    ReplyDelete
  5. Mchawi wa soka la Tanzania ni Simba na Yanga.Tanzama walivyonunua mechi katika michezo yao ya mwisho.Kumekuwa na upangaji wa matokeo wa wazi kabisa.Ndio maana kila mwaka wanaishia hatua za mwanzo katika michuano ya CAF.TFF inabidi ichukue maamuzi magumu na kutoa adhabu kwa vilabu hivi viwili. Nimeona jinsi Toto walivyoitengenezea ubingwa Yanga.Pia watu wanasema Simba na Majimaji nako mambo yalikuwa sio kabisa.Ni aibu kubwa, timu hizi zimekuwa zikinunua mechi kila wakati.

    ReplyDelete
  6. Hivi kuna watu bado huwa wanafuatilia league ya bongo?? league haiuzi kabisa!! Mambo yoteee EPL or UCL soccer la nguvu

    ReplyDelete
  7. wewe anonymous hapo juu.. nini maana EPL or UCL.. ni bora ushabikie timu yako ya nyumbani unayoweza kuiona wewe. ushawai hata kuingia uwanjani kwenye hivyo vilabu? e kama yatafika...... ina maana kwenu kukiwa na nyumba ya miti utasema sio kwa baba yako?..peleka usharobaro wako kwa wenzako huko...TP MZEMBE OYEE!! EEH NIMESAHAU KUMBE YANGA OYEEE!!

    ReplyDelete
  8. Yanga Oyeeeeeeeeeeeeeeee I am so happy here.

    ReplyDelete
  9. Si ajabu Yanga wameshinda kombe mara ngapi? Na Simba mara ngapi? Lakini kila mwaka ni wahapahapa tu..kila mwaka ni kununua mechi tu.Siku moja TFF izishushe Simba na Yanga...ili wajifunze.Hongera Azam, pamoja na hujuma za Simba na Yanga; mmejitahidi kusimama.

    ReplyDelete
  10. kununua mechi inawezekana si ajabu, lakini nani anaweza hakikisha hilo au unazungumzia ushabiki wa mimi simba na wewe yanga,chakufanya toa maoni na ushauri wa nini kifanyike na sio lawama, sikuzote hazijengi.Arsenal alipofungwa na barcelona kila mmoja alisema maneno yanayofanana ya hayo, mara refa kapendelea n.k lakini tujifunze kujenga timu si kwa maneno na kuchangia pia, timu zinakuwa na ukata, huku wanachama na washabikiaji tunapiga kelele. Embu tuwe wanachama na washabiki hai wanaoweza kujenga timu kwa faida ya leo na kesho kufungwa ni sehemu ya mchezo, kila upande ijiandaa kadri ya uwezo ili ishinde. Ni hayo tu kwa leo

    ReplyDelete
  11. "I keep my enemies close
    I give ‘em enough rope
    They put themselves in the air
    I just kick away the chair"

    - Jigga

    ReplyDelete
  12. Eti Azam walinunua mechi ya Simba ahaahhaa

    ReplyDelete
  13. Huyo mdau anayeshbikia EPl na UCL ana matatizo si kidogo. Timu yako hata kama ni mbovu unatakiwa uipe moyo na kujitahidi kuitengeneza sio kuikimbia na kujifanya unashabikia timu za watu. Kwanza kitendo tu cha kujua kuwa timu yako ni mbovu ni mwanzo wa kutengeneza mikakati ya kuiboresha. Kwa sababu ya uvivu wetu ndio maana tunakimbilia vilivytengenezwa tayaritayri. Ona tunavyoagiza bidhaa china zingine tunaweza kutengeneza lakini uvivu wa kufikiri unatawala. Mafisadi wakikwapua pesa wanazificha nje ya nchi badala ya kufanya maendeleo hapa Tz. Na hata wainvest wanaishia kufungua hoteli na mabaa. Biashara ambayo kila mtu anayo.

    ReplyDelete
  14. Kwa nguruwe hako kagoli kamoja anazaa 12, acha dharau wewe. Yanga daima

    ReplyDelete
  15. Nick DizongaApril 11, 2011

    Watu hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee! kwa kweli ningeshangaa sana kama Yanga wasingekuwa mabingwa. kwani wana kila kitu kwa nchi hii kwa ajili ya soka letu. Mashabiki wenye moyo na timu yao, timu nzuri,kocha bora, Uwanja wake wa mazoezi (hata kama hauna hadhi ya kimataifa), na viongozi waliopo kwa mujibu wa katiba. nawapa pongezi sana kwa Ubingwa na mmethibitisha maneno yenu ya kuwa Simba wamewashikia ubingwa wenu kwa muda na sasa mmeshachukua ubingwa wenu. Hongera sana. Mjipange kwa ajili ya mashindano ya kimataifa mwakani. msije leta maneno kama ya wenzenu wa Simba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...