Wanamazoezi wa klabu ya Obama wakiwasili katika bandari ya Mkoani, Pemba
Wanamazoezi wa Obama Unguja na Pemba wakifanya mazoezi ya Pamoja

Wanamazoezi wa Obama wakifanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya AbdallahMzee

Muamko uliopatikana katika Jamii ya Wa zanzibari katika kufanya mazooezi ni mkubwa lakini imeonekana kwamba muamko huo uko zaidi katika maeneo ya mji wa Zanzibar ambapo wananchi wengi wameonekana wakijitokeza katika harakati za mazoezi asubuhi na jioni.

Katika harakati za kupanua wigo wa ufanyaji mazoezi Zanzibar nzima,wanamazoezi wa klabu ya Obama fitness Club walifanya ziara ya ki mazoezi kisiwani Pemba siku ya Jumamosi hii kwa madhumuni ya kuhamasisha Jamii ya Wazanzibari waishio huko kufanya mazoezi kwa lengo la kujenga Afya zao.

Sambaba na hilo klabu hiyo ilizindua rasmi Tawi la klabu hiyo la Mkoani Pemba, Pamoja na kufanya mazoezi ya viungo klabu hiyo huwa inajishugulisha na shuguli mbali mbali za kujitolea hasa za usafi wa mazingira.

Katika ziara hiyo Klabu ya Obama fitness Club ya Unguja ikishirikiana na Obama ya Pemba walifanya usafi wa mazingira katika hospitali ya Abdalla Mzee ya Mkoani Pemba,

Muuguzi mkuu wa Hospital hiyo alitoa shukurani za dhati kwa wanamazezi hao kwa msaada mkubwa walioutoa Hospitalini hapo hasa ukuzingatia kwamba wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa wafanyakazi jambo linalowapa ugumu mkubwa katika kufanya usafi katika maeneo yao.

Pamoja na jitihada hizo za ufanyaji mazoezi na uhamasishaji jamaii, vyama hivi vinakabiliwa changamoto mbali mbali zikiwemo ukosefu wa ofisi za kudumu, vifaa vya kufanyia mazoezi pamoja na ukosefu wa taaluma ya mazezi ya viungo , kwa hiyo wito unatolewa kwa Wa Tanzania wa nje na ndani katika kuchangia ili kufanikisha lengo la mazoezi kwa Afya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. hongereni sana wana Obama kwa kufika Pemba,mumeonyesha mfano mzuri wa kuigwa. Ni jukumu la seriali kushirikiana na nyie na vilabu vyengine katika kujenga afya za raia wake. Bajeti ya Wizara ya afya ya mwaka 2012 inatakiwa izingatie kuwawezesha nawatakia kila la kheri,
    Khamis UK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...