Usataadh Muhidin naomba uniweke kwenye safu yako ili nami nitoe rai yangu kwa wana Arusha ambako mimi ni mdau kuhusiana na kauli za akina Mbowe na Lema.

Nianze kwa kusema nasikitishwa mno na uzandiki wanaotuonyesha kwani mwelekeo wao ni wa kung'ang'ania shari badala ya amani. Madiwani ambao wamepigiwa kura na wananchi wa kata zao wamewasikiliza wapiga kura wao na wakaona busara ni kukaa kwenye meza ya muafaka na kupata muafaka ili shughuli ziende mbele.

Leo anaibuka bwana Lema na kudai ati hautambui muafaka kwa kuwa hauna baraka za vikao vyao vya chama chao. niseme tu huu ni upuuzi ambao ukiachiwa uendelee utaturudisha nyuma kimaendeleo. Madiwani walikuwa wakisusia vikao lakini kwa kuwa kanuni zinawabana vikao vikawa vinaendelea na maamuzi yanatolewa. sasa wameona hawana tija kwa kususia vikao na ni bora washiriki vikao vya kuleta maendeleo jijini Arusha.

Leo wanaibukla watu wawili na kuropoka bila aibu ati hawautambui muafaka mpaka OCD na Mkurugenzi waondolewe. Kisa hawakufanya kazi kwa matakwa yao. Nchi haiendeshwi hivyo. wale ni watumishi wa umma waliokabidhiwa majukumu ya kulinda usalama wa raia na kuhakikisha jiji linaendeshwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za serikali.

 Mambo ya kudai ati chama hakina habari ni kutaka kuchochea vurugu tu, na kuendelea kumpa nafasi bwana huyu akamwaga uchochezi wake kwenye vyombo vya habari ni kutaka kuliangamiza taifa bila mantiki. Mimi nasimama upande wa madiwani na nawaunga mkono kwa dhati kabisa na kama wao akina Mbowe na Lema hawataki basi wawavue uanachama na uchaguzi mdogo utaitishwa nasi tutawaita kwenye chama chetu tuwasimamishe na kuwahakikishia ushindi.

Jamani Arusha tuamke sasa, tazameni barabara za maeneo ya bondeni zilivyoharibika, nendeni marikiti muone kulivyokosa mpangilio , piteni pembezoni mwa jiji muone adha ya miundombinu. sasa tunamaliza mwaka kwa porojo za siasa tu na malumbano na serikali hakuna hata dalili ya maendeleo. Tuseme hapana kwa Lema ili akafanye kazi tuliyomtuma na kama ameshindwa bas awapishe wenye nia ya kuchapa kazi. Hatujamtuma akapigane bungeni kwani ubondia wake hauna tija kwetu wana Arusha.
 
Ndimi Yussufu Laiza
mwana Arusha mzaliwa wa Bondeni
simu ya kiganjani 07 13 211 726

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2011

    Umekaa kishari Shari vile na madiwani wako vilaza.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2011

    Kaka hicho kitendo walichokifanya Madiwani wa Chadema cha kukubali nafasi za uongozi wakati kesi zikiendelea mahakamani ni kujishusha kisiasa maana Taifa zima tungetambua kwamba Chadema hawapo kwa masirahi ya nchi bali ni kutaka nafasi za uongozi tu. Ndugu yangu mimi nahisi wewe ni mwanachama wa kile chama kinachouza rasilimali zetu kwa maslahi binafsi ili tu nchi iwe na wawekezaji.. Huu ni wakati wa kutafakari kabla ya kutenda na kujua madhara ya maamuzi huchukuayo kwa baadae

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2011

    Mdau uliyetoa mada naona umechemsha, yaani unataka kutuambia hiyo miundimbinu unayosema imechakaa ilikuwa haijaonwa miaka yote 50-1 ya uhuru? Acha ushabiki wa kisiasa angalia ukweli ulipo kama tukiendeleza haya ya kugawana madaraka watu watakuwa wanafanya makusudi ili waweze kugawana madaraka. Tena kama ni mtz mpenda maendeleo kama unavyojiita ni heri kutokuwa na kiongozi kuliko kuwa na kiongozi wa maslahi yake binafsi. Hiyo miundombinu chakavu ilikuwepo na wala haijaletwa leo na wala kama unavyodai haitaisha leo maana watakuwa wanafanya kazi kwa sababu tu wamepewa madaraka. FUKUZA HAO NA UCHAGUZI URUDIWE KAMA CHAMA CHENU KILISHINDWA KITASHINDWA TENA TUNATAKA WATU WENYE UPEO NA UCHUNGU WA NCHI HII SI WAPENDA MADARAKA>
    " SECRET SHOULD NOT BE USED TO COVER UP ABUSE"

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2011

    chadema wanatuharibia nchi kwa tamaa ya madaraka...sioni walichokifanya mpaka sasa zaidi ya kupeleka malumbano na mipasho bungeni....kinachohitajika ni kupata rais makini zaidi kutoka CCM awamu ijayo ila sio Chadema..,..kadri muda unavyoenda nazidi kuona kuwa chadema haifai kupewa madaraka kuongoza nchi hata kidogo....nimepoteza imani yangu juu ya chadema....CCM linusuruni taifa letu

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 02, 2011

    kweli nimeamini msemo wa siku nyingi kwamba msafara wa mamba na kenge wapo, mdau hapo juu kusoma hujui hata picha inakushinda lini hiyo nusura ya taifa ilitoka kwa wa kijani mh sikio la kufa halisikii dawa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...