Kuanzia Ijumaa hiii ya tarehe 01 Julai, 2011 Kituo cha Utamaduni Makumbusho (Makumbusho Cultural Centre kwa kushirikiana na Kijiji Cha Makumbusho Pamoja na bendi kongwe ya muziki Tanzania Msondo ngoma, watakuwa wanawaletea burudani kabambe ya Mtanzania, ambayo inajulikana kama JIVUNIE CHAKO MTANZANIA. Siku hiyo itakuwa ni siku ya mtanzania kujivunia na kufurahia kilicho chake.

Kutakuwa na vyakula cya asili, vichekesho vya kitanzania, Maonesho ya mavazi, Ngoma za asili, burudani ya muziki kutoka bendi za Kitanzania, huku ukinywa vinywaji vilivyotengenezwa na makampuni halisi ya Kitanzania.


Hakuna mahali pengine mtanzania utaonesha Utanzania wako, ni Makumbusho Cultural Centre ndani ya Kijiji cha Makumbusho, Kila IJUMAA YA KILA WIKI.


KARIBU NI WOTE TUJIPONGEZE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2011

    Vitu vyao huwa bei ghali sana... wa TZ huwa hamjui biashara. sijui huogopa msingamano wa wateja!

    Punguzeni hizo bei watu waje wengi na muuze kwa sana...

    ReplyDelete
  2. Kuanzia SAA NGAPI?

    Jamani mbona waTanzanai hata Matangazo madogomadogo tu hivi yanatushinda tunashindwa kujieleza?
    Tumekalia kuwashutumu waKenya tu kumbe tuajiloga sisi wenyewe!

    Khaa!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2011

    Bendi ya msondo ngoma inajitosheleza kabisa kwa nyimbo zao nyingi, hivyo haina sababu ya kuchanganywa na watu wengine. Inawezekana mchanganyiko huo ukawavutia watu wa aina mbali mbali lakini nina mashaka kama wapenzi wa msondo watafurahia mchanganyiko huo.

    ReplyDelete
  4. Mambo ya asili why msondo ngoma za asili zitumbuize kila kabila liwe na siku yake n a ngoma zitachezwa acheni mambo ya kuuwa utamaduni wetu. Msondo akatafute ukumbi apige muzilki watu waje kwa mapenzi yao lakini sio kulazimisha kusikiliza msondo siku ambayo kabila fulani linaonyesha utamaduni wao.FUNGUKENI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...