Na Prof. John Mbele


Hivi karibuni, nitakuwa Tanzania na wanafunzi katika programu ya masomo inayoendeshwa na vyuo kadhaa vya Marekani kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 

Kabla ya kuwafikisha Chuo Kikuu Dar es Salaam ambapo watasoma kwa muhula mmoja, nitakuwa nao maeneo ya nyanda za juu, hasa Iringa. Lakini, katika kupanga safari hii, nimeamua kuwafikisha hadi Mbeya na Ziwa Nyasa, wakaone na kujifunza. Iringa naifahamu vizuri, ila Mbeya nilipita tu mara moja, miaka ya mwisho ya sabini na kitu.

Wakati nangojea kwenda Mbeya, nawazia utamaduni wa wa-Nyakyusa. Mimi kama mtafiti, nimesoma kiasi kuhusu masimulizi yao ya jadi. Ninakumbuka maandishi ya watafiti kama Monica Wilson. Nina kitabu kiitwacho The Oral Literature of the Banyakyusa, kilichoandikwa na Christon S. Mwakasaka. Nadhani nilikinunua Dar es Salaam, nikawa nakisoma mara moja moja.

Lakini wakati huu ninapongojea safari ya Mbeya, kitabu hiki kinanivutia kwa namna ya pekee. Kina hadithi za jadi, lakini vile vile nyimbo na tungo zingine zinazoelezea mambo ya hivi karibuni ya historia na siasa u-Nyakyusa na Tanzania kwa ujumla. 

Natafuta maandishi mengine ya kuongezea ufahamu wangu. Kwa hilo naweza kusema nimeathiriwa na wa-Marekani. Wao, kabla ya kusafiri, wana hiyo tabia ya kusoma habari za sehemu waendako. Ni jadi nzuri. Kusafiri kunatupanua akili, lakini kusoma habari za tuendako kunautajirisha zaidi ufahamu wetu.



Kupata chanzo BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 29, 2011

    Aah sijui nianzie wapi. nilikisoma kitabu hiki choote mwaka 1994 au 1995. nilikisoma wakati kizungu changu kina makorongo makubwa kuliko leo. kilikuwa nyumbani kwetu. nilimuazima jamaa yangu akiitwa emanuel mwambelo pale mbeya day secondary school. hakukirejesha hata leo. ningetamani nikisome tena. mbali na hizo hadithi na hekaya za wanyakyusa, pia kuna asili ya wanyakyusa na jina 'nyakyusa'. kwa kifupi kulikuwa na mzee alikuwa na wake wengi. miongoni mwa wake zake mmoja aliitwa 'kyusa'. watoto wa mzee huyo, ambao walikuwa wengi kwa kuwa alikuwa na wake wengi, walitambuliwa kwa majina ya mama yao. hivyo watoto wa mke aliyeitwa kyusa waliitwa .watoto wa kyusa', that is, bana ba kyusa/banya kyusa hence the name banyakyusa, simplified in kiswahili as 'WANYAKYUSA'. kuna stori nyingi, ila nazikumbuka mbili ambazo zilinisisimua sana. moja KAMPAPABUNGA THE IMPOSTOR, nyingine TWO CUNNING MEN.

    Wazungu karibuni Mbeya, karibuni kwa wanyakyusa

    John Mwaipopo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...