Taarifa ya Uongozi wa Kiwanja kuhusu maandishi yanayodaiwa kuwepo kwenye mlango wa usalama


                                                                                               
7.9.2011
Kwa
Mkurugenzi,
Issamichuzi.blogsport.com

YAH: KICHWA CHA HABARI ILIYOTOKEA KWENYE MTANDAO WA ISSA MICHUZI CHENYE KUSOMEKA LIBENEKE LA MAANDISHI LAONEKANA TENA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIGOMA YA TAREHE 7.9.2011.

Tafadhali husika na somo hilo la hapo juu, nakujulisha kuwa maandishi hayo yalishafutwa toka mwezi January 2011 baada ya mwandishi aliyeyaandika kuyakosea na kuchukuliwa picha yalifutwa mara moja toka January 2011 na hakuna maandishi ya aina hiyo kama ulivyoonyesha tarehe ya leo 7/9/2011 kwenye mtandao wako. Kwa yeyote atakayesoma mtandao wako ataamini kuwa maandishi hayo yapo kuanzia kipindi chote hicho January 2011 – 7.9.2011.

Uongozi wa Kiwanja umesikitishwa sana na hali hii iliyojitokeza kuonekana kuwa maandishi haya bado yapo wakati sio kweli. Abiria wanaotumia Kiwanja hiki ni mashahidi kwa hili. Naambatanisha picha ya eneo hili kuonyesha kuwa maandishi haya hayapo toka kipindi hicho.

Ni matumaini ya Uongozi kuwa kabla ya kurusha habari utafanya uchambuzi wa kina kwa kipindi husika ili kutoleta mkanganyiko katika jamii. Picha ya eneo husika imetumwa kwako kuthibitisha kuwa maandishi yale hayapo kwa kipindi hiki ambacho umetoa picha ya nyuma kwa suala ambalo limeshafanyiwa kazi.

Uongozi
Kiwanja cha Ndege cha Kigoma.
-----------------------------
Kwa: Uongozi
Kiwanja cha Ndege Cha Kigoma


Asante sana kwa taarifa. Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza baada ya mdau kutuletea taswira ambayo imepitwa na wakati na kufanyiwa kazi kama waraka wenu unavyosema na inavyoonesha pichani juu. Juhudi za kuupata uongozi wa Kiwanja cha Ndege cha Kigoma zilifanyika lakini ikashindikana kwa kuwa hakuna email wala namba ya simu iliyopo kuijibu maswali yetu. 


Hata hivyo tunategemea kwamba uongozi wa uwanja utatupa taarifa ya kwa nini maandiko ya awali hayajafanyiwa kazi tarajiwa badala ya  kuacha sehemu hiyo kuwa 'bubu' bila maelekezo husika. Wengi tulitarajia kwamba baada ya 'kufanyia kazi' matatizo yaliyojitokeza awali, kungewekwa maandiko mbadala kuonesha umakini uliotarajiwa. 


-MICHUZI


Kupata chanzo cha sakata hili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. YANI UNA SABABU YA KUJITETEA ,HUONGOZI WA WENU UNAONEKANA BOMU NA WABABAISHAJI, KUNA MAKOSA MABAYO UTAKIWI KUKOSEA , HATA YESU AWEZI KUKUSAMEE.USHAURI WA BURE KAMA HATA KAMA HIZO KAZI MMEPEWA HAPO HUWANJA WA NDEGE BILA KUWA NA SIFA ZA KUWA HAPO BASI MUWE HATA WAANGALIFU MNAPO FANYA KAZI ZENU. NAOMBA KUULIZA HUO UWANJA WA NDEGE UNA WATO WA CONTROL ROOM KWELI? KAMA NAO NI VILAZA KAMA WATUMISHI WANAO USIKA NA HAYO MAANDISHI , MTAKUJA KUUWA WATU SIKU, HAIWEZEKANI WAFANYAKAZI WA UWANJA HUO WOTE AMKU ONA HILO TATIZO MIAKA YOTE UNLESS KWAMBA HAMJALI WALA KU CARE AS LONG MPO HAPO KULA TU !
    MDAU CHINA

    ReplyDelete
  2. Wewe uliyetoa maoni hapo juu kabisa, ungepewa hata kazi ya kuandika maandishi kwa Kiswahili ungeandika utumbo mtupu! Kiswahili chako hovyo kabisa! Na usijaribu kuniroga, ama utakiona cha mtema kuni!

    ReplyDelete
  3. Wewe kiomgozi wa uwanja wa ndege, hujui kwamba hayo maandishi ingawa yalikosewa yalikuwa muhimu? Sasa umerekebisha nini kama umeondoa kabisa. Sio wote wanaokuja huko ni wenyeji wanaojua entrance iko wapi na exit door iko wapi, mizigo yao wapate wapi na abiria wapumzike wapi wanaposubiri kusafiri. Maandishi yote hayo ni muhimu sana, na yawe kwa lugha zote, Kiswahili na English FASAHA. Weka hayo maandishi, weka na contacts za uwanja na email. Kama ume-access Michuzi.com na kuona 'lugha gongana' ina maana una ABC za teknologia ya mawasiliano, unajua umuhimu wa vitu hivi, sasa kwanini uwanja uwe bubu na wadau tusiwe na namna ya kuwasiliana na nyie?? Unalaumu tu wala hushukuru kwamba blogspot hii imekusaidia kugundua tatizo ambalo wewe hukuligundua miaka nenda rudi!

    ReplyDelete
  4. Umekuwa muungwana kwa "ku-respond" japokuwa ni wazembe, inakuwaje maandishi kama hayo yanabandikwa kwenye mbao kwa ajili ya kusoma watu lakini kumbe wahusika hamna habari maandishi yenyewe yameandikwaje/yanasomeka vipi!!! Jierekebisheni ili kuondoa aibu tena.

    ReplyDelete
  5. NINACHOSHANGAA WATANZANIA HASA WALIOPO NJE WANAJISAHAU NA KULAUME KAMA VILE LUGHA YA KINGEREZA NI LUHGA YETU YA KWANZA NA HATUTAKIWA KUKOSEA.ACHENI HIZO HUO NI UTUMWA WA KIUTAMADUNI, NILIKUANDIKIA MICHUZI SIKU ILIPOTOKA TASWIRA YA PILI KUKUELEZA KUWA NIMETOKA KIGOMA JULY SIJAONA KITU KAMA HICHO, ILA KWA KUWA LENGO NA MTU MAJI NAWE PIA ILIKUWA NI KUENDELEZA LAWAMA NA SHUTUMA BILA KUTOA SULUHISHO UKAIBANIA UENDELEE KUWAFURAHISHA HAO WANAOJIFANYA WANAJUWA SANA LUGHA ZA WATU.HEBU TAZAMA HUYO MDAU HAPO JUU ANAEKOSOA WAKATI YEYE MWENYEWE ANAANDIKA"KISWA-ENGLISH", KINGERAZA WALA KISWAHILI HAJULIKANI NINI ANAANDIKA.

    ReplyDelete
  6. Mawazo ya Mdau hapo juu ni sawa lakini pia naye Kiswahili anaandika lugha gogana kwa mfano HUONGOZI ni Uongozi,UTAKIWI ni Hutakiwi,AWEZI ni Hawezi,HUWANJA ni Uwanja,USIKA ni husika, AMKUONA ni Hamkuona, nahisi Mdau kutoka china Ka-storway bandalini Dar with no school,asituharibie kiswahili chetu.
    Mdau Dar.

    ReplyDelete
  7. kaka michuzi kwani maaandishi yenyewe yalikuwa yanasomekaje? hebu ya post ili tujue sakata hili lilianzia wapi, maana wengine tumeikutia story katikati nakuona watu wanaanza kuomba radhi kwa usumbufu uliotokea.

    ReplyDelete
  8. Wee bosi acha kitetea ujinga kwani ulipotoa kazi ina maana hukuikagua na ulimlipa huyo aliyeandika huo upupu hapo bila ya kuangalia kama aliandika mlivyokubaliana. saswasawa niwa yenu ni kuanikwa humu ili mtie akili. na tunaomba maandishi mapya au bado mnatafuta mkalimani?

    ReplyDelete
  9. Kwanza kabisa nianze na wewe Mdau kutoka China, wewe pia ni Mtanzania na inaonesha hauko makini katika swala la maandishi....umekosea kosea kiswahili wakati ulikuwa unakosoa mwenzio.

    Pili nirudi kwenye hili sakata, huo uongozi wa uwanja ni shida, hana lolote la kutueleza. Unachotakiwa ni kuomba radhi na sio kumshutumu mdau aliyerusha. Hivi watanzania kwanini hatukubali pale tunapokosea....Siasa nyiiiingi. Ulevi noooooommaaaaaaaa!!!!!

    Mr. Ndizi Nyama, Bukoba

    ReplyDelete
  10. Michuzi upo sawa kabisa wala hujajikwaa popte.Wao kama "walifanyia kazi"kwanini wasionyesha kilichofanyiwa kazi..
    Na kuna hili tatizo website nyingi za taasisi mbalimbali zimeandikwa tu ila hata ukijaribu kulogin zinakuwa hazipatikani au hazifanyiwi update za mara kwa mara,
    Hao wakubali WALICHEMKA,NA WANAENDELEA KUCHEMKA kwa jinsi wanavyojitahidi kutatua tatizo ndio wanazidi kuliongeza.

    Wadau endeleeni kutuletea Taswira zaidi za kuliamisha taifa letu maana wengine wapo usingizini.
    TUTAFIKA TU

    ReplyDelete
  11. Big up Misupu, Mzee wa libeneke! Nimependa hilo Jibu, Tunamsubiri huyo afisa habari aliyeandika hapo aje na majibu ya kuridhisha la sivyo atakuwa amejiabisha tu!
    Libeneke Hoyeee!

    ReplyDelete
  12. Hawa watu wanajitetea nini? kwa nini waliandika lugha waioifahamu, kisha wakaishia kuchekwa na kuamua kufuta?. Tutajuaje imefutwa tokea Januari kama walishindwa hata kutoa notisi kwenye vyombo vya habari au vinginevyo kuwa wamefuta?..Meneja wa Uwanja halikuwa wapi siku zote hizo wakati maandishi hayo yanawekwa pale? yaani alikuwa hasomi au hajui kiingereza? ..hakuna cha kulaumu hapo wala kujitetea Uncle, hawa ni watanzania wazembe na wasiotimiza wajibu wao, nani angejua kuwa wamefuta kama si mdau kutundika mapungufu katika blogu ya Jamiii?

    Watujulishe ni shilingi ngapi zilitumikam kuandika yale maelezo na shilingi ngapi zimetumika kufuta? Haya ni matumizi mabaya ya Fedha za umma hakika...

    ReplyDelete
  13. Michuzi,
    Sina kawaida sana ya kaundika lolote kwenye mtandao wako. Ukweli ni kuwa napita kusoma na kuangalia yaliyomo karibu kila siku. Kuhusu yaliyojiri uwanja wa kigoma naomba nichangie kuwa:
    Uomgozi wa kigoma ungekuwa na unyenyekevu wa kukushukuru kwa kutoa angalizo na kuomba samahani kwa watanzania kwa kufanya makosa amabayo yanatia aibu. Yaani walimtafuta mtu wa kuandika maandishi hayo , wakamlipa pesa za umma nab ado wanataka michuzi ndiye awe makini. Jamani , kwa nini hatuwajibiki kwa kazi zetu ? kukubali kosa ni alama mojawapo ya kuwajibika. Sisi si malaika ,tuanpokosolewa tukubali. Kwa mfano kama utaona makosa katika maandishi yangu haya niambie name nitakubali kosa. Muwe na siku njema uongozi wa uwanja wa ndege –kigoma.
    Pole Michuzi , ndilo jukumu uliloamua kulibeba name nakupa hongera kwa kulibeba bila hiyana.
    UONGOZI: ANDIKENI BASI UJUMBE MLIOUKUSUDIA KWA KUMTUMIA MWANDISHI MAKINI.

    ReplyDelete
  14. Mdau wa China toa boriti katika jicho lako kabla hujatoa kibanzi katika jicho la jirani yako. Comment yako imejaa makosa kama vile "huongozi" "awezi""huwanja" "wato" etc., sijui ungeambiwa uandike kwa lugha ya kigeni kama aliyeandika kwenye huo uwanja ingekuwaje! Aibu zaidi.

    ReplyDelete
  15. wanajishaua tu, mbona rangi yenyewe inajionyesha ya jana tu, inaonekana wamefuta baada ya kupost picha ile kwenye huu mtandao. ukiangalia maandishi yale yapo kwenye rangi chakavu, ina maana yalikaa muda mrefu, siyo kama walivosema uongozi wa kiwanja ya kwamba yalifutwa mara baada ya kukosewa.

    ReplyDelete
  16. ATI JITU NA USOMI WAKE SIJUI WA KUUNGAUNGA LIKIONGIZI LA TAASISI YA UMMA LIMEKURUPUKA USINGIZINI NA KUMFANYA ANKAL MICHUZI NDIO 'TARGET' YAKE...! YANI BADALA UBORESHE SEHEMU YAKO YA KAZI AMBAYO NI KIOO CHA TAIFA MAENEO HAYO UNALETA MIPASHO YA ALAMBA ALAMBA AUMMM HUMU KWENYE GLOBU YA JAMII? IDIOTAS KABISA! FANYA KAZI WEWE, ACHA BIASHARA ZA KUJITETEA KAMA MTOTO ALIYEKAMATWA ANAKULA SUKARI AKAFICHA MIKONO NYUMA.

    HAKYANANI TENA ANKAL UTAANZA KUCHUKIWA (KAMA HUJAANZA BADO). MITUNTUFYE MINGINE HAINA AKILI HATA KUKUMBUSHANA MAMBO YA KHERI KABISA YENYEWE HUANZISHA BIFU TU...

    HILO JAMAA LILILOJIBU NA KUJIITA UONGOZI WA EAPOTI YA KIGOMA AIRPORT NINA WASIWASI NA UWELEDI NA UELEWA WAKE WA MAMBO. KWANZA UMEPEWA PR YA BURE KWENYE KUMBUSHO, INGEKUCOST SI CHINI YA MIL 10 ZA HARAKAHARAKA HAPO, UNAZO KWA PUBLICITY TU? KAMA UNA AKILI ULITAKIWA UCHEKE
    (STRATEGICALLY), UREKEBISHE HALAFU ULETE TASWIRA KURINGA HUMU NDANI KUWA MAMBO SASA SAFI! LIMEFUTA LIKAKURUPUKA USINGIZINI NA KUMVAMIA MITHUPU, SASA HUO MLANGO NI WA KUINGIA WAPI? CHOONI AU JIKONI? MPELEKE MAHAKAMANI BASI, NINCOMPOOP KABISA!

    ReplyDelete
  17. Kwani wee meneja hukuangalia kazi imeendaje baada ya huyo mtu wenu kuandika hapo? au ulimlipa tu basi biashara kwisha! ingekuwa ni biashara yako nadhani ungekuwa makini zaidi ili wateja wasikushangae, lakini kwa vile ni mali ya umma wala hukufuatilia hadi ulipowanikwa humu ndani ndiyo unakuja juu. tunataka maandishi mengine hadi jumatatu acheni longolongo wakati mnapokea mishahara kila mwezi halafu kazi kusuasua tu! na hakika hayo maneno uliyaona sana ukapuuzia yaani hadi msukumwe ndiyo mnawajibika, libeneke oyeeeeeeee, sio wewe tu na wenzio wengi walianikwa hapa wakaweka mambo kwenye mstari fasta bila kulalamika maana waliona makosa yao! narudia tena jumatatu maandishi mengine yawepo hapo sio ombi ni amri!

    ReplyDelete
  18. kama hayo maandishi yalifutwa toka january mbona hakuna marekebisho ya maandishi mengine baada ya hapo? au uongozi haukuona umuhimu tena wa maandishi hayo. Mimi ninavyoona maandishi hayo yamefutwa baada ya hiyo habari, na kupiga picha tena, jamani Tanzania tutaendelea lini? uongozi hembu jipangeni upya na wajibikeni kwa hilo na andikeni maandishi mengine na pigeni picha mturushie, sio ujinga hapa, CIO

    ReplyDelete
  19. Jinsi navyosoma michango ya wadau nazidi kushangaa sisi watanzania na tatizo la lugha. Mdau aliyekumbushia kujitoa boriti kabla ya kutoa kibanzi katika jicho la mwenzio kapatia sana maana michango mingi hapa imejaa makosa ya kisarufi na kiuandishi. Tujenge haiba ya kujisahihisha kabla ya kukurupuka kusahihisha wenzetu. Sasa hawa nao wanakosoa lakini angalia mambo yale yale katika maandishi yao. Mdau wa kwanza,(makosa kibao), wa tatu (kiomgozi), wa tano (kulaume,luhga,kingeraza), wa sita (gogana), wa nane (saswasawa, niwa) wa kumi (popte, wasionyesha),wa kumi na mbili (waioifahamu, zilitumikam), wa kumi na tatu (kaundika, uomgozi, name). Je mkipewa kazi ya mwandishi mchovu wa uwanja wa Kigoma kutakuwa na ahueni?

    ReplyDelete
  20. michuzi huyo kiongozi hana hata aibu kusema kuwa alilifuta jan, na hii ni september bado hata hawajaweka mwongozo mwingine, wanafikiria nini? na muda huo wote waliofuta hakuna hata maelekezo yoyote kwa wageni wakifika uwanjani hapo, hebu waweke sasa tangazo lingine tumwone anafuatilia kazi yake, michuzi juu zaidi!!!!!!!

    ReplyDelete
  21. Kwanza wahusika wa Uwanja huo wa ndege, kabla ya kuanza kujitetea eti kuwa maandishi yalifutwa, wanatakiwa wawaombe msamaha watanzania kwa kuwaaibisha namna hii. Hivi inawezekana watumishi wote wa hapo uwanjani hawakugundua makosa hayo mara tu ama wakati yakiandikwa? Hakuwa na mtu ambaye alitakiwa kuhakiki kazi iliyofanyika baada tu ya muhisika kuweka maandishi hayo? Au wafanyakazi wote pale lugha inawapa shida? Hii picha ya maandishi ya ajabu ajabu itaendelea kusambaa tu dunia nzima, na wala wahusika wasitegemee itakwisha leo ama kesho. Hiyo ndio raha ya internet..na ni fundisho wote kuwa tunatakiwa kuwa waangalifu kwani hizi ndio consequences zake, ukizingatia utandawazi uliopo dunia ya sasa.

    ReplyDelete
  22. watanzania tusipende kulaumu na kuwa watumwa wa kiutamaduni tukumbuke lugha yetu ni kiswahili na hayo ni makosa ni wakati wa kutoa ushauri nini kifanyike sio kulaumu...
    mdau norway

    ReplyDelete
  23. Nimejikuta nikicheka mwenyewe, si kutokana na utetezi feki wa uongozi wa uwanja, bali kutokana na michango ya wadau. Mdau wa China sijui anatuambia nini hapo, maana tunajadili kuhusu kuandika maneno kiusahihi, lakini yeye kaja kutuvurugia Kiswahili chetu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...