Kaka michuzi,kwanza pole kwa kazi ya ujenzi wa Taifa.

Pili hongera kwa kutuhabarisha wana jamii wa ulimwengu huu kuhusu yale yanayojili  kwenye sayari yetu hii ya tatu.

Kaka michuzi naomba kwa heshima kubwa unisaidie kwa hili langu.
Mimi ni kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 31.

NINAMTAFUTA MCHUMBA mwenye umri husiozidi miaka 25 ya kuzaliwa.
Namtafuta mchumba atakayekuwa mama wa familia yangu.

Naomba kwa dada aliye huru na mwenye kujiheshimu na kumuheshimu mungu na aliyetayari kuolewa awasiliane na mimi kupitia mail address hii thejunior.global@gmail.com bila kusita.

[1]Namhitaji dada ambaye ni mkiristo wa dhehebu la Seventh Day Adventist[SDA] kwa yule asiye wa dhehebu hili awe tayari kubadili dini.

[2]Awe ni mzaliwa wa mikoa ya kanda ya ziwa Victoria,Mwanza,Shinyanga,Mara na Kagera.

[3]Awe na elimu kuanzia kidato cha sita.[Form six] na kuendelea haijalishi awe amepata kazi au la!!

[4] asiwe amesha zaa.
[5]Awe mrefu au mrefu wa wastani,awe na mwili wa wastani,awe maji ya kunde au weusi wa kung'ara.

            Mwisho naomba atakayewasiliana namimi hasiwe mbabaishaji au mjaribu bahati.

Mawasiliano zaidi yatafanyika mara tu ya kumpata aliye tayari.
Asante kaka Michuzi na kazi njema na Mungu atubariki sote.

Mdau.


Sifa za ziada:
1. Maji ya kunde au mweupe
2. Uzuri ni kigezo muhimu
3. Urefu wa wastani
4. Wa Dar atapewa kipaumbele zaidi.(Mi niko Dar pia).

Kwa vigezo hivyo vichache muhimu nina hakika ya kuwa nawasiliana na mwanamke ninayemuona.

Kuhusu wasifu wangu, huyo mwenza asiwe na sababu ya kutilia shaka


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Ndugu thejunior.global@gmail mimi ni msichana mwenye sifa zote ulizozitaja hapo juu. Lakini tatizo ni kwamba wewe umetaja sifa yako moja tu ambayo ni umri wa miaka 31. Hujataja sifa nyingine yeyote. Sasa nadhani ni muhimu pia ukataja sifa ulizonazo kama ulivyoainisha sifa za msichana unayemuhitaji. Maana mimi binafsi pamoja na kwamba nahitaji mchumba lakini pia nahitaji kumjua huyo mchumba ni mwenye sifa gani. Naomba urekebishe tangazo lako uweke pia CV yako.
    Ni mimi
    Grace Waitara
    Email: gwaitara@yahoo.com, simu: 0713821672. Naishi Mbezi, kazi yangu mwalimu wa Secondary.

    ReplyDelete
  2. Usibague mikoa bwana mzuri na anayejiheshimu anaweza kutoka mkoa wowote. Au unataka muongee kilugha kitupu nyumbani kwako?

    ReplyDelete
  3. jamani huyu jamaa mbona hajatoa wasifu wake? ana elimu gani, kazi anayo n.k

    ReplyDelete
  4. mi ningekushauri uende huko huko kanisani kwenu mnapoabudi kutafuta mchumba na inaonekana ni mtu mwenye hila na gubu na unayetengeneza binadamu wenzio.

    ReplyDelete
  5. Kwa qualifications hizo itabidi utengeneze wa kwako (man made).

    Jee wewe una sifa gani maana na mabinti wangependa kukufahamu pia.

    ReplyDelete
  6. Wanaume wa siku hizi hawajui kutongoza au ni balaa gani hili???

    ReplyDelete
  7. That is why you are still single, with that altitude you will remain single for a very long time.
    Just a small piece of advise, you need to be open minded if you real want to meet someone to spend the rest of your life together, who the hell do you think you are ? are you prince Williams or Bill Gate son ?

    ReplyDelete
  8. wewe bwana unachekesha sana , yani unavyo jipendelea kwa viwango vya ubora unavyo vitaka utazani wewe mungu. mimi naomba kuuliomba na wewe naomba uweke quality zako atharani, usijifanye hapa unapenda vizuri wakati wewe mwenyewe BUSHELELE !!!

    MDAU PARIS

    ReplyDelete
  9. wewe bwana unachekesha sana , yani unavyo jipendelea kwa viwango vya ubora unavyo vitaka utazani wewe mungu. mimi naomba kuuliomba na wewe naomba uweke quality zako atharani, usijifanye hapa unapenda vizuri wakati wewe mwenyewe BUSHELELE !!!

    MDAU PARIS

    ReplyDelete
  10. Miss Vodacom itafanyika karibuni, nenda ukajichagulie huyo mwenye hizo sifa zako!! Mtu anaoa au anaolewa na ampataye!!

    ReplyDelete
  11. mijitu mingine inaboa mpaka basi we mtu atake kufaa nafikiri ni dada yako may anasifa hizo, kuwa flexble man acha huo ukabila na udini ambao haumake hata sense bado upo karne ya ngapi wewe chizi hebu kwanza tutokee hapa hii sio web ya mapenzi

    ReplyDelete
  12. Thejunior.Global@gmail.com.[NINAYETAFUTA MCHUMBA]
    Naomba nitoe wasifu wangu kwani wadau mmeonekana kulihitaji hili.
    1].Nina elimu ya chuo kikuu[digirii 2]
    2]Nina kazi-Serikalini
    2].Ni mrefu wa wastani.
    3]Si mnene si mwembamba.
    4]Weusi wa kawaida.
    Asanteni.

    ReplyDelete
  13. kazi serikalini haitoshi, tuambie wewe uko takukuru ama TRA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...