Mshiriki wa shindano la Guinness Football Challenge,Nelson Allen  akishiriki kuonyesha kipaji chake cha mpira mapema leo kwenye shindano hilo lililowavutia vijana wengi kutoka sehemu mbalimbali ya jiji la Dar.
 Mmoja wa washiriki wa shindano la Guinness Football Challenge,Catherine Nathanel akishiriki kuonyesha kipaji chake cha mpira mapema leo kwenye shindano hilo lililowavutia vijana wengi kutoka sehemu mbalimbali ya jiji la Dar.
Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya SBL,Ephrahim Mafuru sambamba na Waratibu wa shindano la Guinness Football Challenge ,Masoud Maestro pamoja na Shaffii Dauda wakishangilia jambo.
Pichani kulia ni muwakilishi wa kampuni ya Endemol ya nchini Afrika Kusini,Warren akiwa na Muwakilishi wa kampuni ya Carberry Commonication,Tom wakishuhudia mashindano hayo leo mchana.
Pichani shoto ni Meneja wa kinywaji cha Guinness Moris Njowoka akimuelekeza jambo Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Serengeti Breweriers Ephraim Mafuru wakati wa shindano hilo leo lililofanyika kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar..
Baadhi ya Washiriki waliojitokeza na kujisajili kwenye shindano la GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE wakiwa katika picha pamoja mapema leo mchana kwenye viwanja vya Lidaz Club.

Leo wamejitokeza Washiriki wengi kujisajiri na kuonyesha maajabu ya mpira wa miguu katika kipindi hiki kabambe cha Televisheni ambacho kinaangaliwa na kuwavutia watu wengi barani Afrika,Shindano hilo la GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE,litawapatia mashabiki nchini Tanzania nafasi ya kujitokeza na kuonyesha mapenzi yao ya dhati katika mpira wa miguu na kushindana na mashabiki wakubwa wa mpira wa miguu kutoka Kenya na Uganda huku wakijishindia mamilioni ya fedha.

Baada ya kupatikana timu nane zitakazokuwa na watu wawiliwawili , timu hizo zitashiriki katika shindano hilo kupitia Luninga (Television) likirushwa mara moja kila wiki Televisheni kwa muda wa wiki nane, na kila wiki atapatikana mshindi mmoja atakayejishindia Dolla za Kimarekani 50.000,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...