Frank akijadiliana na Mish wakati wa kipindi cha chemsha Bongo
 Mish akikamua ndani ya Sporah show
Picha ya pamoja baada ya show
 Urban pulse Ndani ya sporah show
Salam,

Kwa mara nyingine tena Frank toka Urban pulse na msaniii makini Fyah Sister wakiwa ndani katika studio za Televisheni zinazotengeneza kipindi mashuhuri cha Sporah Show.

Kipindi hiki  maarufu kiendeshwacho na Dada yetu Sporah hapa UK kinapatiakana katika Sky TV  chaneli 184. Frank na Fyah Sister walialikwa kwenye exclusive interview na Dada Sporah kuzungumzia hali ya promotion ya nyimbo na mixtape ya fyah sister iliyopo mtaani hivi sasa. Vilevile walizungumzia hali ya uhusiano wa ma promoter na wasanii pamoja  na mitihani gani wanakumbana nayo.

Album ya Fyah Sister ambayo imetengenezwa katoka studio za urban pulse, ni moja ya albamu zinazokuja juu sasa hasa katika kundi la wasanii wa kike, kwani England kuna wasanii wachache sana wazuri wa kike. Pia kipindi kiliongelea hatua na mafanikio ambayo urban pulse wameyapata mpaka hivi sasa kwenye masuala ya mbalimbali. Unaweza kudownload au kusikiliza mixtape ya Mish inayoitwa Fire Brigade kupitia link hapo chini.


Mish ni msanii mkali wa kike anaekuja juu hapa UK, amefanya maonyesho mengi ikiwepo Notting Hill Carnival, Derby, Centre Hall Westminister jijini london n.k. Pia amechaguliwa kuingia katika mchakato wa kumtafuta best MC katika shindano linaloitwa OPEN MIC litakalofanyika mwezi wa kumi na fainali zake kufanyika katika O2 Arena london.

Spora show imekuwepeo mstari wa mbele katika kusaidia, kuwahamisha  wafanyabiashara na wanaharakati wa Kiafrika hapa UK. Vilevile ni kipindi kinachopigania na kuangaza mapambano kuhusu maswala yanayowakabili jamii za kiafrika  uk, kama vile, domestic violence,child abuse,rape, teenage pregnancy na masuala mengine yanayoathiri jamii zetu.

Kipindi Hiki kitakuwa hewani mda sio mrefu kupitia Ben TV sky channel 184. Kwa maelezo zaidi tembelea Sporah Show Blog


Asanteni,

URBAN PULSE CREATIVE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. huyu frank naye kazidi kuuza sura!

    ReplyDelete
  2. I Love Sporah Jamani uwiiiiiiiiiii.

    ReplyDelete
  3. sasa bila huyo frank ungemuona huyo sporah? acha ujinga wewe!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...