Mzee Kipara wakati akiwa bado na nguvu zake

 
Mzee Kipara enzi zake wakati bado ana nguvu
 Mzee Kipara akijaribu kushuka kitandani
Akisaidiwa kusimama na wageni waliokwenda kumjulia hali

Napenda nitoe masikitiko yangu kwa wasanii wa Sanaa ya Maigizo wote Nchini kwa kutoonyesha msimamo wa pamoja ili kuweza kumsaidia Mzee wetu Mzee Kipara (Fundi Said) ambaye kwa sasa ana afya ambayo sio nzuri pamoja na uzee lakini hali ngumu ya kimaisha ndio inayochangia zaidi.

Mzee Kipara ni msanii wa muda mrefu sana katika Tasnia hii ya sanaa ya Uigizaji, ni muigizaji mkongwe sana katika Taifa letu, kwa wale wasiomjua alianza kuigiza sanaa toka mnamo mwa miaka ya 1964 enz za RTD (Redio Tanzania) kwa sasa TBC hii kwa faida ya vizazi vya sasa msio fahamu hili.

Baadae Mzee kipara walianzisha kikundi cha maigizo ambacho kikawa kinarushwa na kituo cha ITV ambacho amedumu nacho kwa muda mrefu sana kikiitwa Kaole. 

Katika kipindi chote hiki cha Kaole aliwafundisha wasanii wengi sana ambao kwa sasa wengi mnawasikia au mnaziona kazi zao kwenye Luninga zenu.

Cha kunisikitisha wengi wao hawajaonyesha upendo wao hata kidogo kwa mzee huyu, nitakua mnyimi wa Fadhila kama sita mshukuru sana Stephen Kanumba nakumbuka alikua msanii wa kwanza kwanza kwenda kumsaidia huyu Mzee; namshukuru sana, najua wapo wengine ambao pia walikwenda kwa nyakati tofauti tofauti kuweza kumuona huyu mzee au hata kumsaidia kwa chochote kile.

Mimi binafsi kama mwakilishi wa KAPINGAZ Blog napenda kuwashukuru wote waliofanya hivyo, ila ombi langu kwenu ninyi wasanii wa sanaa ya Maigizo ni kwa nini msiandae tamasha lolote ambalo mnaweza mkakusanya kiasi kikubwa cha fedha kikaweza kumsaidia huyu Mzee wenu badala ya kwenda mmoja mmoja kumuona huyu Mzee, kumbukeni na nyie ni vijana kwa leo itafika wakati mtazeeka kama huyu mzee na watatokea wengine mmewafundisha hiyo sanaa naamini na nyie mnaweza mkasikitika kama mzee huyu.

Naomba niwape mfano wa Dada Asha Baraka, Mkurugenzi wa African Star (Twanga Pepeta) nampongeza sana huyu dada aliweza kuandaa tamasha la Dansi kwa ajili ya kukusanya michango ya kumsaidia Mzee Muhidin Ngurumo ili aweze kupata matibabu vizuri, na mpaka leo naandika masikitiko yangu, Mzee Ngurumo leo anapanda kwenye stage kuimba na wenzie katka tamasha la sikukuu ya Idd el Fitr.

Nawaomba wasanii wote katika sanaa ya maigizo muweze kulitazama hili la Mzee Kipara kama ni jambo lenu wote, na hata mnapokua mnakwenda kwenye vikao vyenu na BASATA muweze kuliongelea hili, ili muweze kua na umoja wenye nguvu wa kuweza kusaidiana kwenye matatizo kama haya. Tunawaona mara kwa mara mnaenda kufanya shughuli mbali mbali sehemu tofauti, hasa za kujipongeza katika mafanikio flani ni vema mnapokua huko mkumbushane la mzee huyu msimuache aishi maisha haya ni aibu kwenu wasanii wote hasa zaidi nyie mliopitia Kaole.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Ama kweli maisha ni mafupi. Naona kama ni jana tu huyu mzee alikuwa kiigiza kwenye luninga na akina Swebe. Sasa hivi ndio ameshazeeka kiasi hicho hata kushuka kitandani inakuwa tabu!!

    Wenye kuponda maisha pondeni kwa kuwa ni mafupi lakini msisahau kuwa uzeeni nako kuna maisha.

    ReplyDelete
  2. uncle tutaftie acc yake tumsaidie chochote!

    ReplyDelete
  3. Huyo mwenye baibui anaemsaidia Mzee Kipara ni msanii wa Kaole anaitwa Kalunde, na anaishi nyumba hiyo hiyo na Mzee Kipara, na nyumba hiyo imepangishwa na wasanii wa Kaole, na makala hii inaonyesha kama vile wasanii hawajafanya lolote huko ni kudanganya umma

    ReplyDelete
  4. Nimeona kwenye vyombo mbalimbali wanaweka ngonjera na mashairi kuhusu Mzee Upara. Kinachotakiwa ni akaunti ya kutoa michango yetu na mtu wa kusimamia hiyo pesa ili apate mahitaji yake muhimu pamoja na dawa. Tukipunguza siasa na kumlaumu yeye kutojijenga mwenyewe Haitakuwa faida kwake. Ametupa raha sana ni zamu yetu kumzawadia. Tunaomba akaunti na msimamizi na mengineyo na mimi nipunguze ngonjera, mashairi na siasa. Degelavita.

    ReplyDelete
  5. Kwa kweli ni Mzee wa zamani na amefundisha mengi kwa kupitia michezo yao yeye na wenzake.

    Ni vyema ikaanzishwa account watu tukawachangia hawa wasanii wa zamani?

    ReplyDelete
  6. Nawashukuru wote mliochangia mawazo yenu kupitia kwa Mwana Blog mwenzangu Michuzi, naamini wote mliochangia mawazo yeni ni mema na mnamtakia mema Mzee huyu. Mimi kama Mwakilishi wa Blog ya KAPINGAZ kwa kupitia Global Publisher nitajitahidi kufanya mawasiliano na wale ambao wanahusika na nitawajulisha ni jinsi gani mnaweza kumpata huyu mzee au mnaweza mkamfikishia vipi michango yenu iwe ni kwa Bank a/c au kama ana simu basi mnaweza mkamtumia kwa njia hiyo iwe ni M-PESA au TIGO PESA. Tumsaidie huyu Mzee. Napenda pia nimshukuru huyo Mdau aliechangia hapo kua Kaole wamempangia Nyumba na mambo mengine natanguliza shukrani zangu kama ni hivyo, ingawa nadhani anahitaji msaada zaidi. kama kuna mdau ana swali lolote anaweza akaniandikia kwenye Email yangu kapingaoh@gmail.com. From http://kapingaz.blogspot.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...