Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa, Profesa. Nicholas Bangu anawaalika wahitimu wa mwaka 2011, familia, ndugu, jamaa, marafiki na umma kwa ujumla kwenye mahafali ya 14 ya chuo hicho yatakayofanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 29 Oktoba mwaka huu. Mahafali yataanza saa 3:00 asubuhi chuoni hapo.

Mahafali yatatanguliwa na kongamano la wanataaluma (convocation) litakalofanyika siku ya Ijumaa ya tarehe 28 Oktoba, kuanzia saa 3:30 asubuhi chuoni hapo.

Wahitimu wote wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao na kuhudhuria mazoezi ya mahafali (rehearsal) bila kukosa. Wanafunzi wasiyohudhuria mazoezi hayo yatakayofanyika siku ya Ijumaa tarehe 28 Oktoba, saa 10:00 Jioni hawatashiriki kwenye mahafali.

Tafadhali thibitisha ushiriki wako kwa kutuma ujumbe (SMS) kwa simu namba 0767888596 ama barua pepe (email) pro@tumaini.ac.tz. Mwisho wa kuthibitisha ushiriki ni tarehe 23/10/2011.

Majoho ya mahafali yataanza kutolewa tarehe 24/10/2011. Mwisho wa kutoa mahojo ni tarehe 28 Oktoba 2011 saa 10:00 jioni. Majoho yatatolewa na ofisi za wakuu wa vitivo husika.

NYOTE MNAKARIBISHWA 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Aise PRO mimi najitolea kuwatengenezea logo bure maana nimeiangalia hio nembo yenu naona kama haiendani na 2011!! Michu atakupa contacts zangu.

    Che.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...