Na Francis Dande
Mabaki ya gari aina ya Hyundai ikiwa imeharibika vibaya baada ya kuparamiwa na Lori lenye namba za usajili T269 BRQ eneo la River Side Ubungo jirani na Kiwanda cha Azania jijini Dar es Salaam katika barabara ya Mandela leo mchana na kusababisha vifo vya watu wawili waliokua katika gari dogo aina ya Hyundai.
Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela ambapo jumla ya magari saba yamehusishwa katika ajali hiyo. “chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Lori ambaye alikua katika mwendo kasi na kupoteza mwelekeo hadi kusababisha ajali hiyo ambapo kabla ya kuparamia magari hayo alilikwepa daladala na kisha kuyavaa magari hayo”
Aliyefariki na kutambuliwa ni mwanaume Venon Sebastian mwenye umri kati ya miaka 35-38 na Mwanamke ambaye hakuweza kufahamika mara moja ambaye kichwa chake kilitenganishwa na kiwiliwili kufuatia ajali hiyo.
Aidha Kenyela aliongeza kuwa majeruhi wanne walikimbizwa hospitali baada ya hali zao kuwa mbaya ambao ni, Mussa Charles, Prosper Mwakitalima, Abbas Julius na Yahaya Makame Mwalimu wa Chuo Kikuu.
sikumbuki hata kama barabara zetu
ReplyDeletezina alama kila sehemu zinazoonyesha dereva anaweza
kwenda kwa mwendo kasi gani, maana
najitahidi kupata picha ila siwezi,
loli lilikuwa mwendo kasi na kukwepa dala dala
tanzania kuna haja ya kubadilisha sheria za babara na lincence naona tutamalizika kinyama kwa staili hii tunayoenda nayo,
ReplyDeletemagazeti yameandika dereva wa lori alikuwa anajaribu kukwepa daladala lililokuwa limepaki nje ya kituo ndio ajali ikatokea. Jamani hawa madereva wa daladala ndio tabia yao kupaki magari yao nje ya kituo ama hatua chache kabla hawajafikia kituo. Kwa nini wasishughulikiwe kwa hilo maana wanauzi kweli unakuta wanapaki barabarani na wanaacha kituo kikiwa na nafasi kubwa ya kutosha. Kwa nini kazi hii ya udhibiti wasipewe majembe auction kama ulinzi shirikishi ikiwa askari wetu wa kikosi cha usalama barabarani wameelemewa na mzigo. Itolewe adhabu kali ikiwa ni pamoja na kuwafutia leseni za biashara wamiliki na madereva kufutiwa leseni zao. Hili likifanyika kwa dhati sidhani kama tabia hii itaendelea. Watatumaliza hawa jamaa.
ReplyDeleteHivi chanzo hasa ni nini kilichopelekea hilo loli kuacha njia?maana wengine wanasema mwendo kasi,mara alikuwa anamkwepa mtembea kwa miguu mjamzito,mara daladala iliyopaki nje ya kituo.Pole sana wafiwa na majeruhi,tupo pamoja katika kipindi hiki kigumu.Mungu awafanyie wepesi mpone haraka majeruhi na waliotangulia awapumzishe kwa amani!!
ReplyDeleteNaungana na Anonymous wa hapa juu,kama kuna jamii ya watu ninaowachukia katika maisha yangu ya hapa Mjini (Dsm) ni madereva wa dalala,Jamaa ni Was***e sana,kila siku wanasababisha ajali,juzi kati bado kidogo waniingize Mtaroni barabara hiyohiyo ya Mandela,pu***vu sana,mimi namlaumu sana dereva wa Lory la jana,anakwenda kuparamia Gari 7 za Raia wasio na hatia ksbb daladala imechomeka,ona sasa hasara ya mali na roho aliyoisababisha,hapo utakuta daladala iliendelea na safari bila hata wasiwasi,mimi nasema siku napata Lory hlf daladala inajipendekeza eti inachomeka Jamii yote itasikia,nakwenda kulenga palepale kwa dereva tena kwa kishindo kikuu,potelea mbali
ReplyDeleteKinachoniboa ni tabia za waendesha daladala ---wengi wao si proffessional kabisa maana wanapaki mahali popote pale wanapojisikia as if nchi walishainunua.Na nina uhakika aliyesababisha kitokee kilichotokea ni daladala.Mie nadhani kuna haja ya kuwachukulia hatua hawa watu.Afu huyo jamaa wa Lori alikuwa ana haraka gani wakati anafahamu fika barabara zetu ni finyu maana seems alikuwa katika speed akijua fika kuna vichaa wa daladala wanapaki.
ReplyDeletedereva wa daladala amepaki gari vibaya, mmiliki afutiwe leseni? mmiliki ndiye aliyepaki vibaya? kosa kafanya dereva, mmiliki au biashara yenyewe? sheria za tanzania nyingi hasa za barabarani zinatoa adhabu kwa mwingine na sio mtenda kosa, ndio maana inakuwa ngumu watenda makosa kuzitii. watanzania wengi ni wavivu kufikiri kama ilivyo kwa mtoa maoni wa tatu hapo juu. bora njaa ya tumbo kuliko ya kichwa hasa ambapo mtu hajui kama ana njaa ya kichwa. kamata dereva mhusika adhibu yeye for F sake.
ReplyDeleteJamani mbona tunaambiwa chanzo cha ajali ni daladala ilijichomekea barabarani na lori ndi ktk kumkwepa haya yote yakatokea???!1
ReplyDeleteJamani jamani yaani basi tu kwa nini vifo vya barabarani vimekuwa hivyo kwanini wakati sisi tuna soma kwenda makwetu(70s) usafiri ulikuwa ni wa barabara na hakuna ajali za kijinga hivyo? kila siku iendayo kwa mungu lazima unasikia ajali mbaya tatizo ni nini? serekali na wasomi hawawezi kutafakali na kupata solution ya kupunguza ajali hizi au kwa sababu tanzania tumekuwa watu wengi,hivyo imekuwa kampeni mpya ya kumaliza watu kisirisiri?
ReplyDeleteJamani poleni sana majeruhi wa ajali hii na Mungu baba awajalie mpone haraka. Vilevile poleni wafiwa Na Mungu baba awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu. Ila mimi nalaumu sana polisi wa barabarani hasa wanaokaa makutano ya Ubungo wamekuwa wanaweka foleni ndefu sana.Kama isingekuwa foleni ajali hii isingehusisha magari mengine.Sasa jamani tunaomba hawa mapolisi wajitahidi kuachia magari mengi hasa yatokayo Buguruni kwenda Ubungo hasa saa za jioni maana huwa kuna malori mengi yanasafiri, sasa hizi foleni ni hatari sana hasa kukaa karibu na haya makontena yaeendayo nje ya nchi.
ReplyDeleteJAMANI HIVI SERIKALI TANZANIA NA VIONGOZI WAKE WACHUKUE HATUA KALI HASA KWA MALORY MAKUBWA NA MADALADALA. MAANA HAYA MALORY NDO MCHEZO WAO YANAKUWA KATIKA MWENDO KASI HATA KATIKATI YA MJI HALAFU HAYANA BREAK.
ReplyDeleteNilikuwepo katika eneo la tukio tangu linaanza mimi ni mpenzi sana wa Glob ya michuzi sijafurhishwa na wanahabari wetu kuna eneo la maelezo halijakaa vizuri, ni kwamba katika magari yote hakuna aliyefariki ila wote wliofariki ni wale waliokuwa wnatembea kwa miguu ambao ni wamachinga wawili na mama mjamzito aliyekatwaa kichwa,kwa mawazo tu!eneo la riverside kwa sasa madereva wa daladala na malori wamekuwa sio wastaarabu nahauri kuwa ni bora kuwe na mtuta jpo mawili kuweza kunisuru maisha ya watu.
ReplyDeletejamani chanzo ni daladala lori lilivyokuwa linakuja daladala (akachomoa)yaani akatoka kando ya barabara na kuingia barabarani na ndipo yule dreva wa lori akamkwepa kwa kuogopa kuua watu wote ambao walikuwa kwenye ile daladala. kwa hiyo kama alivyosema hapo juu udhibiti wa daladala wapewe majembe. tutakwisha!
ReplyDelete