African Stars Band ambao wanajulikana pia kwa jina la  “Twanga Pepeta” walikuwa  kivutio cha sherehe za miaka 50 ya Uhuru London juzi Jumamosi. Kikosi hiki cha watumbuizaji maarufu wa Kibongo kilikaribishwa na  Urban Pulse, Jestina George wakishirikiana na Ubalozi wa Tanzania mjini hapa. Pichani juu ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter Kallaghe akizindua sherehe hizo za miaka 50 jijini London wikiendi ilopita ambapo Twanga walipepeta hadi liamba. Ijumaa hii mambo yote yatakuwa Milton Keynes. Ukikosa usije kulalamika oooo sikuambiwa....
 Balozi Peter Kallaghe na mkewe pamoja na Mh Aggrey Mwanri na Mwenyekiti wa CCM Uingereza Ndg Maina Owino wakipozi na wana Twanga Pepeta kabla ya shoo kuanza
 Mpiga ngoma maarufu wa Twanga Pepeta Kibosho akiwa tayari kuanza kazi
 Amigoras na mnenguaji wa Twanga wakipepeta
 Shoo ikiendelea
 palikuwa hapatoshi
 Nyomi si ya kawaida
Twanga ikipepetwa jukwaani
Picha na habari na mdau mkuu wa Globu ya Jamii UK, Freddy Macha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kazi sasa inaelekea kwa watoto wa Mji NORTHAMPTON na wana Mtandao CCM UK kama kawaida yao hachajiwi mtu kiingilio mlangoni tarehe 03/12/11. Asiye na tumbo aazime. Kunywa ni kwa kuogolea naona stoo 2 zimefurika. Kazi kweli kweli.

    Issa bin Jumaa.
    mpapasa ngurumo.

    ReplyDelete
  2. Ama kweli bata ataliwa kwa mrija hapo NORTHAMPTON kwa watoto wa mujini..Du, kwa mtaji huo wa kiingilio na kunywa kwa Udhamini nitakuja hata kwa miguu!

    ReplyDelete
  3. Mnhhh kaka Amigolas picha ya 4 kutoka juu, pole kwa kulisakata rhumba na msala mzito kiunoni...hahahahah ila ,wanenguaji wa kike wengi micharuko!

    ReplyDelete
  4. Hahahahahah,, Amigolas mukubwa picha ya 4 kutoka juu, ila ubebaji huo wataka moyo na uaminifu...kwa mtu KACHALA anaweza piga kitendo bila makosa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...