KAKA ZA KAZI,

MIMI NI MDAU WA HABARI WA MUDA MREFU PIA NI MTUMISHI WA MUNGU KATIKA HUDUMA YA KICHUNGAJI. NAOMBA UWAHABARISHE WADAU KUHUSU KUCHANGIA KWENYE UJENZI WA HEMA LA KUKUTANIA KWA AJILI YA MAOMBI YA TAIFA LETU NA MAOMBEZI KWA AJILI YA WENYE SHIDA MBALI MBALI. 

UJENZI WA HEMA HILO UNAFANYIKA BOKO-MIVINJENI NJIA YA KUELEKEA MBWENI HOSPITALI. TUNAOMBA MUNGU AKUWEZESHE ILI UWEZE KUCHANGIA VIFAA KAMA VILE CEMENTI (SARUJI), BATI, MBAO ZA KENCHI KWA AJILI YA KUPAULIA AU HATA PESA TASLIMU ENDAPO UTAONA NI VIGUMU KUBEBA VIFAA HIVYO.

WAWEZA KUTUFIKISHIA MCHANGO WAKO KWA NJIA ZIFUATAZO: M-PESA KWA NAMABA 0754 461253, TIGO PESA 0715 461253

AU AKAUNTI YETU CRDB BANK, KIJITONYAMA BRANCH, AC. NO. 01J 2013277900.

MUNGU AKUBARIKI KWA UTAYARI WAKO KWANI MAANDIKO YANASEMA KATIKA MITH. 3:9 "MHESHIMU MUNGU KWA MALI ZAKO.


MAWASILIANO ZAIDI:

JONAS KAMALEKI
MCH. KIONGOZI WA HALELUYA MINISTRY
P.O. BOX 68070
DAR ES SALAAM

jkamaleki@yahoo.co.uk

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. kanisa linaitwaje? maana siku hizi makanisa mengi sana, wengine wanadondoka kina Mwingira wengine wanaibuka

    ReplyDelete
  2. Kukosekana kwa uadilifu kwa watu wanaojiita watumishi kumeharibu imani ya jamii kuwa hicho ni kichochoro kingine cha ulaji na ufisadi.

    ReplyDelete
  3. Ni kweli inabidi tujiulize huu utitili wa dini unatoka wapi? ukiangalia kwa undani utakuta ni madaraka na fedha kwani inaanza kanisa au msikiti mmoja na unaendelea kugawanyika siyo kwa kukua bali kumeguka vipande vipande kutoka na masilahi binafsi. Haya changeni na huyo aongezewe ulaji

    ReplyDelete
  4. Jonas Kamaleki (Rev)January 20, 2012

    Mpendwa tunakushukuru kwa kusoma Tangazo hili jina la Kanisa ni HALELUYA MINISTRY. NI HUDUMA INAYOHUDUMIA WATU WA DINI ZOTE BILA UBAGUZI. NI HUDUMA YA KIROHO KWA MASUALA MBALI MBALI YANAYOLISIBU TAIFA, FAMILIA NA JAMII KWA UJUMLA. KWA MAELEZO ZAIDI TEMBELEA TOVUTI YETU. TUMEKUWEPO TANGU 2006. www.haleluyaministry.yolasite.com.
    MUNGU AKUBARIKI KWA MCHANGO WAKO.

    ReplyDelete
  5. Acha hizo mtumishi, Pesa haitafutwi hivyo kwa kusingizia ujenzi wa HEMA LA MUNGU.Kama unahitaji pesa inabidi utubu kwa MUNGU wako, halafu umuombe MUNGU akupe hilo hitaji lako.

    ReplyDelete
  6. Kumbe bado una ile ya baba kasema ukija nikuambie hayupo?Wanaanza kuzungusha mifuko ya sementi KWANZA,halafu ghafla jengo la kuishi wewe na familia uponyaji wa MIUJIZA ukishika kasi na waumini kufurika ndipo mifuko inayeyuka na ,gari la kutumia mtumishi,matangazo ya miujiza tuuu,bila mahubiri yenye mwongozo katika vyombo vyote vya habari.Kama hakuna atakayestuka mwisho jengo la ibada linaonekana.
    Mpe kwanza Muumba anachostahili na umuinue na kumsujudu.Kwani ulikuwa unaabudu wapi kabla ya kutaka hilo kambi?Kulikoni wana wa Mungu?Kapige kambi kule ulikokukimbia na utafunuliwa zaidi,Mungu wetu wa uweza yuko pale atakusikia nakukuona na hitaji lako,acha kufanya biashara katika hekalu la Bwana.Ubarikiwe na ufunuliwe katika jina lipitalo majina yote,AMEN

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...