Familia ya Kusaga inawaomba watanzania wote walioko Marekani na hasa eneo la Washington DC na vitongoji vyake kushirikiana nao katika harambee (fundraising) ili kupata pesa ya mazishi ya mtanzania mwenzetu Christavina Kusaga Cryor aliyefariki February 7, 2012 kwa saratani ya utumbo (Colon Cancer)

Marehemu alikuwa akiishi Landover, MD. Ameacha mume na watoto wawili- mvulana wa miaka 4 na msichana wa miaka 2. Alikuwa akisumbuliwa na cancer ya utumbo.

Tafadhali fika tushirikiane kumsaidia mume wake na watoto na familia wamzike mpendwa wao. Jumla ya gharama za mazishi ni $11,000, na mpaka sasa ni $2,000 tu imepatikana. Tunashukuru kwa waliokwisha saidia.

Harambee itakuwa Jumapili February 12, 2012, kuanzia saa 8.30 mchana (2.30pm).
Anuani ni: 3621 Campus Drive, College Park, MD 20740.

Kwa wale wa mbali au wasioweza kuhudhuria tafadhali tusaidie mchango wako kwa kutumia Capital One Bank, Account# 1351500235; Routing # 255071981. Tafadhali eneza habari hii kwa ndugu na marafiki wote. Asanteni sana kwa ushirikiano wenu katika wakati huu mgumu.

Kwa habari zaidi mpigie: Magoma (202.607.1976); Adelaida (240.602.3183); Matinyi (301.792.2832); Mkakile (240.938.3177); Teddy (301.25441696); Makaya (202.460.1044); Latifah (240.603.7353); au Rebecca (202.580.4648).

**********R.I.P Christavina*************

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. RIP Christavina, tulisoma pamoja St Anthonys Sec School Mbagala Dsm A Level mwaka 2001- 2003 ukiwa Head Girl.. Poleni sana familia, ndugu, jamaa na marafiki wote. Tutaungana nanyi huku nyumbani kwa hali na mali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...