KATIKA hali isiyo ya kawaida, wabunge kutoka Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni leo wameiunga mkono Serikali iliyo madarakani na hata mmoja wao kudiriki kusema bungeni kuwa Mbunge atakayepinga mapendekezo ya Serikali katika Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ni muasi.

Msemaji wa Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu amemsifu Rais Jakaya Kikwete kuwa amekuwa msikivu sana kwenye jambo hilo, na hakuangalia maslahi ya chama ila maslahi ya Taifa.

Amesema, Rais Kikwete amefanya kazi kubwa kushughulikia suala hilo , na kwamba kambi hiyo inaunga mkono mapendekezo ya Serikali.

Kambi hiyo imewaomba wabunge wote wamuunge mkono Rais ili kulipatia Taifa utaratibu wa kutengeneza Katiba mpya wenye mwafaka wa kitaifa.

“Mheshimiwa Spika, kwa mara ya kwanza, naomba kuunga mkono hoja hii” amesema Lissu bungeni mjini Dodoma na ameunga mkono mapendekezo yote ya Serikali kwenye muswada huo.

Spika wa Bunge alionesha kufurahishwa na kauli za Lissu na kuwaeleza wabunge kuwa, alivyofanya Mbunge huyo wa Singida Mashariki (Chadema), ndivyo inavyotakiwa.

Aliwataka wabunge waache chuki, hila na uhasama, wasibishane kwa misingi ya vyama, wabishane kwa hoja na kwamba, jambo hilo linamuhusu kila Mtanzania hivyo pia walijadili kwa makini.

“Huu muswa ni very tricky, hatujadili muswada wa mabadiliko ya Katiba, tunafanya amendments ya sheria iliyopo” amesema.

Makinda amewataka wabunge waujadili muswada huo wakiwa wamoja, na wananchi wajifunze kutoka kambi ya upinzani ili Watanzania wasonge mbele wakiwa na utulivu, umoja na upendo.

Wakati anatoa maoni yake kuhusu muswada huo, Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR- MAGEUZI) alimpongeza Rais kwa namna alivyoshughulikia muswada huo na akasema, wabunge watakaokataa mapendekezo ya Serikali ni waasi.

Baada ya kauli hiyo, Mbunge wa Viti Maalum, Anna Abdallah (CCM), aliomba mwongozo wa Spika akasema, lugha aliyoitumia Machali ni ya kuudhi hivyo afute kauli yake.

Alisema, si sahihi kuwaita wabunge hao waasi, na kwamba, kama ni uasi, waliuafanya wao mwaka jana, akimaanisha wabunge wa Chadema.

Spika wa Bunge alimtaka Machali afute kauli yake, Mbunge huyo alikubali kuifuta lakini akamtaka Anna Abdallah naye afute kauli yake kuwa wabunge wa Chadema waliasi mwaka jana.

Machali alifuta kauli yake lakini wakati anamalizia kuchangia alirudia maneno yale yale kwamba, “Na mtu yeyote atakayepinga hoja hii atakuwa muasi”.

Mbunge huyo pia alipinga kuli ya Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM) kuwa, wabunge wa Chadema hawakuwatendea haki Watanzania waliposusa na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge wakati Bunge likijadili Muswada wa Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011.

“Huu si muda wa kulalamika, kulalamika lalamika hakutusaidii” amesema Machali.

Chenge amewapongeza wabunge kutoka kambi ya upinzani kwa kutambua umuhimu wa Rais katika mchakato wa mabadiliko ya Katiba.

CHANZO: HABARI LEO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. SPIKA NA CHENGE WANAGEUKA KAMA VINYONGA: KINA LISU NA CHANDEMA WALIUKATAA MSWADA KWASABABU ULIACHA MAMBO MUHIMU MAKUBWA IKIWEMO KUWAACHA WANANCHI KWENYE MCHAKATO MPANA, NDIO MAANA WAKAUKATAA. LEO WAMEONGEA NA RAIS AMELIONA HILO, AMEKUWA MUUNGWANA KWA MASLAHI MAPANA YA TAIFA, AMEINGIZA MAPENDEKEZO YAO.

    HAO KINA CHENGE NA SPIKA WALIOPITISHA MWAKA JANA WANASEMA UPINZANI NDIO UNATAKIWA KUWA HIVYO, WANAWAPONGEZA!! SAWA, LAKINI WAKATI WANAYAKATAA NA KUTOKA NJE MWAKA JANA HAMKUYAONA MAPUNGUFU HAYO?.´MLIPOWAKEJELI MWAKA JANA HAMKUONA UBOVU WA SHERIA MLIYOIPITISHA?. LEO RAIS AMETUMIA BUSARA ZAKE BAADA YA KUONGEA NAO, TENA KWA KIREFU, MNAWAPONGEZA!!. ANGALIENI SANA WANANCHI WASIJE WAKAWAONA MNAFUATA UPEPO TU. MAANA RAIS AMETUMIA BUSARA ZAKE BAADA YA KUONA HAMJAMSAIDIA.

    ReplyDelete
  2. Kutokana kwa nchi maskin na ukubwa wa rushwa na viongozi waliokuwa si wazoefu na Democrasi ninakubaliana na Wabunge serikali ya kikwete imejitahidi!

    ReplyDelete
  3. Well done Hon. Jakaya Mrisho Kikwete!

    ReplyDelete
  4. I would like to take this opportunity to congratulate the members of parliament regardless their political interests for deciding to stand together in this issue of constitution bill amendments. Thanks very much for focusing to the destiny of Tanzanians and not your parties. This has been my prayers day and night we put the interest of our country first and our parties later. You are Blessed. God Bless Tanzania.

    ReplyDelete
  5. Vizuri sana ndugu yetu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete!

    Mengi mabadiliko umeyafanya, zaidi ya mchakato wa Katiba nimeongea na rafiki yangu hapa tukajaribu kulinganisha hali ya Ofisi za Ubalozi zilivyokuwa zina ogopwa Ughaibuni kipindi cha nyuma,,,lakini sasa zimekuwa ni Sehemu ya Nyumbani Nje ya Nyumbani Tanzania!

    Hii ni kutokana na Dira na mwelekeo wako ndugu Raisi!

    ReplyDelete
  6. Ahsante sana tuko pamoja Mhe. Raisi JK!

    ReplyDelete
  7. Mhe. Rais JK huo ndio urithi bora utakaofanya ukumbukwe kwa kuwaunganisha waTZ bila kujali itikadi zao mbalimbali. Siku zote umekuwa msikivu na mvumilivu kwa watu wako. Huyu ndiye Rais tunaye mtaka anayeweza akashauriwa hata na watu wa kawaida katika jamii hatimaye akaufanyia kazi ushauri wao kwa maslahi ya taifa. Mungu akupe afya njema uendelee kututumikia waTZ kwa moyo mmoja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...