Wizara ya Maliasili na Utalii inawakambusha wananchi wote kuwa tarehe Mosi Aprili kila mwaka ni SIKU YA TAIFA YA KUPANDA MITI. Mwaka huu maadhimisho ya kitaifa yatafanyika mkoani Singida.
Kama ilivyo kawaida tarehe Mosi Aprili ni siku ya uhamasishaji, na kila mwananchi anatakiwa kupanda miti michache kama hakutakuwa na mvua za kutosha. Miti mingine ipandwe wakati muafaka kadri majira ya mvua yatakavyoruhusu.
Chimbuko la Siku ya Taifa ya Kupanda Miti ilikuwa ishara ya  kuikaribisha Milenia mpya kwa kupanda miti ambapo Serikali iliwahamasisha wananchi kupanda miti milioni mia moja mwanzoni mwa mwaka 2000.
Mwaka huo huo wa 2000 Waziri Mkuu ilitoa Waraka wa Serikali Namba 1 wa mwaka 2000 ambao ulielekeza kuwa Januari mosi kila mwaka ni Siku ya Taifa ya Kupanda Miti. Hata hivyo, kwa kutambua kuwa siyo kila mkoa unapata mvua mwezi Januari Waziri Mkuu alitoa waraka mwingine Namba 1 wa mwaka 2009 ambao uliibadili Siku ya Taifa ya Kupanda Miti kutoka tarehe mosi Januari kuwa tarehe mosi Aprili kila mwaka.

Wizara inasisitiza kuwa mwaka huu shughuli za kupanda miti zitaambatana na kutenga maeneo na kuyatunza ili miti ya asili iweze kuota yenyewe. Njia hii imefanikisha maendeleo ya misitu mkoani Shinyanga ambapo wananchi wanastawisha misitu kwa kutumia uoto wa asili, njia ijulikanayo kama ‘ngitili’.

                                                                  George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
26 Machi 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Huyo mama alieinama zaidi ya 90 degree afahamishwe kwamba bi against health and safety na inadamage uti wa mgongo. ninawasilisha Thanks.

    ReplyDelete
  2. Mama anajua kupanda mti.

    ReplyDelete
  3. Mama anajua kupanda mti kweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...