Nchi yetu itasitisha rasmi matumizi ya teknolojia ya utangazaji ya analojia na kuhamia teknolojia ya dijitali ifikapo tarehe 31 Desemba, 2012 saa sita usiku.

Lengo la kufanya hivyo ni kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano duniani kote. Miongoni mwa faida za kutumia teknolojia ya dijitali ni kuongezeka kwa ubora wa matangazo ya televisheni, ongezeko la chaneli za televisheni litakalotokana na matumizi bora ya masafa, kuwepo kwa masafa ya ziada yatakayopatikana baada ya kuzimwa kwa
mitambo ya analojia inayotumia masafa mengi, kuongezeka kwa watoa huduma wa mawasiliano ya simu, matangazo ya televisheni kupatikana katika vifaa vingi zaidi vya mawasiliano kama vile simu za mkononi na kompyuta kupitia mtandao wa intaneti.

Hivyo, nachukua fursa hii kuwajulisha na kuwahimiza wananchi wote kufanya maandalizi ya kukabiliana na mabadiliko hayo kwa kutumia ving’amuzi vitakavyowezesha televisheni za analojia zinazotumika kwa sasa kupokea matangazo ya dijitali au kutumia televisheni za
dijitali ambazo hupokea matangazo ya digitali moja kwa moja.

Kwa taarifa zaidi piga simu namba 0784 558 271 
au tembelea tovuti zifuatazo:

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. In ur dreams Zitto,Watanzania siyo wajinga kiasi hicho, you will never ever be our president, fact.

    ReplyDelete
  2. tushawazoea hao ikifika Dec 31 wataongeza muda hadi Juni 30 2014.
    ngoja tuone mchezxo wao mana kwenye simu kusajili line kulizungushwa weee na matokeo yake pamoja na kusajili asiyesajili anapeta tu na bado watu wanaendelea kutukanwa na kukukashifiwa kwa kutumia simu na hawakamatiki.bongo tambalaleeeeeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  3. Hahaha kila mtu anataka kuwa Raisi. Hivi kwanini, kuna nini IKULU cha kukimbia?

    ReplyDelete
  4. Napingana na hilo kwa asilimia mia moja. Huko ni kuwaonea watanzania wengi wasio na uwezo. Wewe unataka kuniambia wakulima waliopo maeneo ya kijijini wamejitosa kununua madishi na kuendesha tv zao kwa kutumia umeme wa jua, leo hii unamwambia ile dishi aitupe jalalani?. Huu ni ujinga, na tena nahisi huu ni mradi wa mtu fulani..... ndani ya serikali.

    Hata nchi zilizoendelea bado zina tumia mifumo yote ya analog na digital. Hivyo muwaachie watanzania uhuru wa kuchagua kutegemeana na uwezo wao. Tuacheni kubweteka kwa mambo madogo madogo.

    Je gharama za hizo decoder mkulima na mtanzania wa hali ya chini atawezaje kumudu!

    Naishauri serikali ifanye mambo kwa priority, ningeomba kwanza serikali ipeleke umeme kote nchini. Ihakikishe umeme unapatikana katika vijiji vyote vya Tanzania badala ya kufikiria ndoto ya kuzima TV za analog.

    ReplyDelete
  5. Haya Mabadiliko ina maana pia gharama za huduma ziwe ni za chini zaidi .

    TATIZO LILILOPO AFRIKA NA AZAIDI HAPA (NCHINI TANZANIA) NI GHARAMA ZA AJABU AJABU ZA HUDUMA AMBAZO ZINASHANGAZA HAZIINGII AKILINI NA HAZI NYAMBULISHIKI KTK MAHESABU HALISI.

    MFANO UNAWEZA KUKUTA KITU KAMA HIKI:

    KUSAFIRI KWA NDEGE KUTOKA ULAYA HADI MAREKANI NI CHINI YA DOLA (US$ 300) HUKU UREFU WA SAFARI NI MUDA WA MASAA NANE (8),,,UTASHANGAA SAFARI KUTOKA TANZANIA (AFRIKA) HADI ULAYA NAULI NI ZAIDI YA DOLA (US$ 1,500) NA UREFU WA SAFARI MASAA HAYO HAYO NANE (8)....

    SASA JE HUKU TANZANIA (AFRIKA) NI SHAMBA LA BIBI AU NDIO KWA WAJINGA WENYE HELA ZA BURE????

    ReplyDelete
  6. Ninawashangaa sana hawa jamaa wa digital tv...mbona ving'amuzi venyewe havikamati..... naona viko dar peke yake...kama hata hapa Pugu havifiki si uzushi huo....wanatuletea yale yale ya usajili wa simu....miradi ya watu hiiiiii....tunachoka kuburuzwa...........

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...