Miss da ball, get da mannn....
 Okwi akifanya vitu vyake
 Mshambuliaji wa Toto African, Musa Musa akimiliki mpira huku akizongwa na mshambuliaji wa Simba, Felix Sunzu wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana. Timu hizo zilitoka suluhu.
 haftaimu - bila bila....Nahodha wa Simba, Juma Kaseja, Felix Sunzu na Juma Nyoso wakitoka mapumziko wakati timu hiyo ilipopamba na Toto Africa katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Boban na mpiraaa....


Picha na habari na Francis Dande
WEKUNDU wa Msimbazi Simba, leo wamevutwa mkia na Toto Africa baada ya kulazimishwa kutoka nayo sare ya 0-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Nashno Stedium jijini Dar es Salaam.
Simba imebaki kileleni mwa msimamo wa Ligi baada ya kuwa na tofauti ya magoli ya kufunga ambapo Simba imetumbukiza nyavuni mabao 30 wakati timu ya Azam inashika nafasi ya pili kwa kuwa na idadi ya mgoli 29 ya kufunga.
Pambano hilo lilianza kwa kasi na kila timu ikionesha uchu wa kutaka kupata magoli, jitihada za Simba zilizoonekana kudhibitiwa vema na safu ya ulinzi ya Toto kutokana na vijana hao wa jiji la Mwanza kuonesha kukamia mchezo huo.
Dakika ya 24 Saidi Nassor ‘Cholo alionywa kwa kadi ya njano baada ya kucheza ndivyo/sivyo, dhidi ya Kamana Bwiza wa Toto. Dakika tatu baadaye, Emmanuel Okwi akakosa bao, baada ya shuti lake kupanguliwa na kipa, kabla ya Patrick Mafisango kufumua shuti jingine lililookolewa na mabeki.
Toto nusura ijipatie bao mnamo dakika ya 35, ambapo mpira uliokuwa dhahiri ukielekea nyavuni, ulipoondoshwa na Cholo na kuinusuru timu yake.
Felix Sunzu dakika ya 37 akashindwa kumalizia pande la Haruna Moshi Boban, kabla ya Bwiza wa Toto kuikosesha timu yake bao mwishoni mwa kipindi cha kwanza alipobaki yeye na Juma Kaseja na mpira kupaa juu.
Hadi filimbi ya mapumziko ya mwamuzi Nathaniel Lazaro kutoka Kilimanjaro inapulizwa, timu zilitoka dimbani kwa sare ya 0-0.
Licha ya mabadiliko ya hapa na pale, ukame wa mabao ukaendelea hata baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, kilichoshuhudiwa beki wa Simba Kevin Yondan akilimwa kadi ya pili ya njano na kutoka nje kwa nyekundu.
Yondani alipewa kadi nyekundu hiyo baada ya kujiangusha kwenye boksi la penalti.
Njano ya kwanza kwa Yondani ilitokana na kudondoka na kuukumbatia mpira kabla ya filimbi ya mwamuzi.
Dakika ya 85, Simba nusura ipate bao, baada ya shuti la Salum Machaku kupanguliwa na mlinda mlango wa Toto.
Toto ikahitimisha mashambulizi yake kwa Simba dakika ya 87, ambapo Phabian Ngwase, alifumua shuti kali na lililokosa umakini na kwenda nje. Hadi mwisho, Simba na Toto zikagawana pointi kwa sare hiyo iliyowaacha Wekundu hao nafasi ya pili nyuma ya Azam.
Simba imefikisha pointi 39, moja nyuma ya vinara Azam FC, huku Toto African ikibaki katika ukanda wa kushuka daraja, kwani nyongeza ya pointi moja imewabakisha nafasi ya 12 kwa kufikisha pointi 17.   

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kiama cha Fani ya Mpira jamani,,,unakuta mtu anashindwa kucheza Mpira nchi za mbele huko Sweden anarudi kucheza kwenye Makombe ya Mbuzi na mechi za Mchangani za Maharage!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...