Tangazo lipo katika moja ya mahoteli makubwa ya kitalii ufukwe wa kaskazini wa Dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. hapo 100% lugha gongana

    ReplyDelete
  2. Hiyo inaitwa kufotoa maneno ya Kiswahili kwenda kiinglish..Jamaa yuko juu aibu!!

    ReplyDelete
  3. Tatizo ni nini? mie sijaona hapo maana mie nimeelewa kwamba boti yetu ina imewekewa bima,sisi hatuwajibiki kwa upotevu wowote wa mali za abiria,
    gharama zetu kwenda na kurudi ni tsh 20,000/=
    Ndio maana nasema sijaona tatizo kama wewe unafahamu hiyo lugha ya kwa bibi utakua tu umeelewa jamaa wanamaanisha nini kwani lugha ni mawasiliano wawili muelewane tu

    ReplyDelete
  4. Mradi inaeleweka sioni tatizo vilevile. Wachina wanabomo a kiswahili lakini wanaelewana na wafanya biashara wenzao pale kariakoo.

    ReplyDelete
  5. Hapo hamna tatizo ujumbe umefika kwani kiswahili unaweza kufikisha ujumbe na watu wakakuelewa. Mfano mchezaji wa Bolton Fabrice Muamba alipoanguka uwanjani na kuzimia unaweza kusema Job Hundred, kwamaana ya kazimia.

    ReplyDelete
  6. sasa na wewe mdau wa 9.42pm utaua watu kwa kicheko.yani umeona mfano hai ni wa Muamba, alijob hundred uwanjani..kwi kwi kwi. not funny lakini umefikisha ujumbe kwa wanaosema lugha gongana!!!kula tano.

    ReplyDelete
  7. Hapa kuna utata mkubwa si wa Kiingereza, tangazo linasema Boti ina bima kwa tatizo lolote, kisha mstari unaofuata linasema halitahusika na vitu binafsi, hapa ni kwamba si kweli kuwa bima ni kwa tatizo lolote, kuna baadhi ya matatizo hawtayashughulikia

    ReplyDelete
  8. Ode cho! kiki wandu wajifanyia weechi sana kisungu wai? Matondo kuchu! lugha ni maelewano kama inaleweka poa we unataka aandike slang ili ujue anajua? ili iweje?

    ReplyDelete
  9. Angetumia hata Goolge translation angalau angepata lugha iliyonyooka.

    Ni tatizo kubwa sana kwetu kwa kupenda kujiamini sana kwa ufasaha wa Lugha bila hata kuuliza watu wahakiki kabla ya kuweka hewani.

    Pia ni ubahili na kudharau kuwapa kazi wanaojua Lugha fasaha !

    ReplyDelete
  10. Mimi Mwamgongo nadhani hakuna lugha gongana hapo zaidi ya kosa moja tu la kuandika servise badala ya 'service'. Kwani tafsiri inaonesha boti lina bima dhidi ya tukio lolote la bahati mbaya lihusishalo chombo hicho (mishap) kama ajali, lakini si vitu binafsi vilivyoachwa au kusahauliwa na abiria.

    Mwamgongo,
    Mwenyeji wa Tanga

    ReplyDelete
  11. Matondo kuchu, wajifanya waichi kila kindo, wandu cha iwo waichi kindo kabisa vo mai! CHA MAANA NI MAELEWANO...

    ReplyDelete
  12. Hamna tatizo, uliza wale wanaotembelea sehemu kama uchina, japan, india nk uone hiyo mnayoita lugha gongana, cha msingi ni kupata ujumbe. Na hapo ujumbe umetulia!

    ReplyDelete
  13. Hilo swala ni sawasawa kabisa mkumbuke kwamba lugha yetu ya taifa ni KISWAHILI sio kiingereza ndio tunatakiwa tutie mkazo lugha yetu mkazo ili tuwape ajira ndugu zetu wengine(WAKALIMANI)maana akija mgeni na akikuta tangazo la kiswahili inabidi atafute mtu wa kutafsili, kama huku kwa wenzetu wao pia wanaandika lugha yao moja tu kutokana kwa wageni wote wasiojua lugha yao wameshatayarishiwa wakalimani na wakalimani ni wazawa inamaana mzawa tayari kashapata ajira hapo nasisi inabidi tufate mfano huo na tena hizo nchi zimeendelea kuliko sisi ulimwenguni,fanyeni tuwekelugha yetu ya kiswahili juu sawa ndugu zangu.

    ReplyDelete
  14. Wenzetu nchi zote zinazoendelea DUNIANI zinatoa AJIRA kwa watafsili wa lugha sisi hatutaki tunakazania mgeni apate kila kitu bure hili swala serikali lifikilie au lugha yetu kuu ni HIPI?naona swala hili ndilo linazidisha kutapeliwa na UMASIKINI na kunyanyaswa na kadhalika na kwanini?wakati tunapewa UHURU tumepewa lakini hatukulazimishwa na hao waliotupa uhuru kwamba lazima tuzungumze kiingereza,JAMANI TUWAJIBIKE TUWEKE SAWA JAMBO HILI TUONDOE ULIMBUKENI TULIONAO,maendeleo ya nchi yataletwa na lugha yako rasmi, tuangalie TANZANIA asilimia ngapi ya raia wanauzungumza kiingereza fasaha pamoja na kuandika na kusoma na na kuelewa? wangapi wanao zungumza kiswahili fasaha pamoja na kusoma na kuandika na kuelewa?mdau bwegenaz

    ReplyDelete
  15. Eti wakalimani! Amini usiamini ukiangalia karibu maoni yote yaliyotolewa hapo juu kiswahili chake si sanifu yaani nacho lugha gongana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...