Majaji Mustafa Hassanali, Madame Rita Paulsen (kulia), Aminat  Ayinde na Doreen Noni (shoto) wakipozi kabla ya kuanza zoezi hilo leo hoteli ya Serena jijini Dar es salaam
 Millen Magese, Mdau, Madame Rita Paulsen na Mustafa Hassanali

 Millen Magese akiwakaribisha mamodo watarajiwa
 Aminat  Ayinde kutoka America  Next top model cycle 12 ya Tyra  akisaidia katika zoezi hilo
 Mamodo watarajiwa wakisubiri kusailiwa
 Palijaa






Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Millen Happiness Magese leo ameendesha zoezi la kutafuta wanamitindo watano (wa kike watatu na wa kiume wawili) watakoshiriki kwa mara ya kwanza katika  maonyesho  ya wiki ya Mavazi ya Afrika Kusini (South Africa Fashion Week) tarehe 1 April mwaka huu.
Mamia ya wasichana na wavulana wamejitokeza katika zoezi hilo hoteli ya Serena ambalo Millen ameliandaa kupitia kampuni yake ijulikanayo kwa jina la Millen Magese Group Company Limited chini ya mpango wake wa kuitangaza Tanzania kupitia fani ya mitindo (Tanzania International Fashion Exposé (TIFEX).
Millen  anaamini kuwa wanamitindo wa Tanzania watakaopatikana katika zoezi hilo wataiwakilisha Tanzania vyema katika wiki ya maonyesho ya mavazi ya Afrika Kusini na kuitangaza Tanzania kimataifa kama anavyofanya yeye kwa hivi sasa.
Wanamitindo waliotakiwa walitakiwa kuwa  na vigezo vifuatavyo vya:- Umri miaka 18 mpaka 24, urefu 1. 75m, hips 37cm (ukiwa na nywele zako za asili) na kwa wanaume urefu ni 1.82m.
“Naamini kuwa zoezi hili litawanufaisha wana mitindo wa kike na wa kiume wa Tanzania na vile vile ushiriki wao katika SAFW na katika maonyesho mengine ya mavazi nje ya Afrika na kusaidia kuitangaza nchi kimataifa,” alisema Millen.
Alisema kuwa lengo kubwa la kampuni yake ni kuendeleza fani ya uanamitindo na vile vile kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake kwa kupitia fani ya mitindo na hata kwa njia ya utalii.
Aliongeza kuwa japo Tanzania ina wanamitindo wengi na wabunifu, bado kuna pengo kubwa ukilinganisha na maendeleo ya fani hiyo katika nchi ya Afrika Kusini na Nigeria.
Alisema kuwa nchi hizo zimepiga hatua kubwa sana na yeye kuhamasika kuanzisha kampuni yake iliyozinduliwa mwezi Machi mwaka jana kwa lengo la kuziba pengo hilo na kuleta maendeleo ili wahusika wafaidike na matunda ya fani yao.
Majaji wa zoezi hilo ni Ritha Poulsen, Mustapha Hassanali na Khadija Mwanamboka na katika kuwekea umuhimu zaidi mchakato huo, MMG imemkaribisha mwanamitindo maarufu, Aminat  Ayinde kutoka America  Next top model cycle 12 kushuhudia zoezi hilo lililodhaminiwa na Clouds FM na Benchmark production.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...