• Masharti yametimizwa; wabunge 73 wazalendo wamesaini
  • Ni mwendelezo wa ‘operesheni uwajibikaji’
Mnamo tarehe 19/04/2012 wakati nahitimisha hoja ya Kamati ya Mashirika ya Umma nilieleza kusudio langu la kuwaomba waheshimiwa wabunge waniunge mkono katika kutia saini zisizopungua asilimia 20 ya wabunge wote ili kuweza kutimiza matakwa ya Katiba ibara ya 53A kwa ajili ya kuwasilisha Bungeni hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Mnamo tarehe 20/04/2012 niliandaa orodha ya waheshimiwa wabunge wote na kuisambaza ndani na nje ya ukumbi wa Bunge ili waheshimiwa wabunge wote waweze kutia saini hizo, na mpaka leo tarehe 22/04/2012 orodha hiyo imetimiza idadi ya wabunge wazalendo wanaopigania uwajibikaji 73 kutoka vyama vyote vyenye uwakilishi Bungeni, isipokuwa chama cha UDP ambacho kina Mbunge 1 na hajatia saini waraka huo mpaka sasa.

Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kifungu cha 133 (1) kinasomeka “Mbunge yeyote anaweza kutoa taarifa ya maandishi kwa Spika ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 53A ya Katiba” na kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (3) kinasomeka “hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitajadiliwa na Bunge isipokuwa tu kama;

“taarifa ya maandishi iliyowekwa saini na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku zisizopungua kumi na nne kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa Bungeni;”

Hali kadhalika kanuni za Bunge Kifungu cha 133 (4) kinasomeka kuwa “hoja inayotolewa chini ya Kanuni hii na iliyotimiza masharti ya Katiba,itawasilishwa Bungeni mapema iwezekanavyo na itaamuliwa kwa kura za siri”.

Hivyo basi baada ya kutimiza matakwa ya kikatiba na kanuni za Bunge leo tarehe 23/04/2012 nitawasilisha rasmi kwa Spika Taarifa ya Maandishi kwa mujibu wa kanuni 133 (1) na (3) ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa kushindwa kusimamia uwajibikaji wa Serikali bungeni kwa mujibu wa ibara ya 52 na hivyo kulinda mawaziri wenye kusababisha matumizi mabaya ya fedha za umma na kulisababishia hasara taifa.

Tunatarajia kwamba siku kumi na nne baada ya kuwasilisha hoja hiyo bunge litakutana kwa haraka kujadili hoja hiyo ili kuwezesha uwajibikaji na hatua kuchukuliwa za kuhakikisha mapendekezo ya ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na maazimio ya Bunge yanatekelezwa. Hoja hii ni mwendelezo wa ‘operesheni uwajibikaji’ hivyo tunaomba wabunge na watanzania wote waiunge mkono ili kunusuru uchumi wa nchi na kuchangia katika ustawi wa wananchi.

Kwa niaba ya wabunge waliotia saini kuunga mkono taarifa ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu;

…………………………….

Kabwe Zuber Zitto.
Mbunge Jimbo la Kigoma Kaskazini.

22/04/2012.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. KAMUA BABA PIGANIA HAKI ZA WANYONGE BABA NA MUNGU AKUONGEZEE NGUVU,IMANI KWA NCHI YAKO,STRANGE ENOUGH.NCHI TAJIRI WATU MACKINI KWA ASILIMIA 90 NA HIYO 10 NDO HAO VIGOGO NA JAMII ZAO? NA CC WANYONGE TWAKUOMBEA UCKU NA MCHANA

    ReplyDelete
  2. CCM kwanini hamtaki kubadilika?Na wakiachia ngazi wataifishwe mali zao..Nina hasira sana wiki kadhaa zilizopita nililipa mkopo(deni?) niliopewa na serikali wakati nasoma chuo kikuu cha Daresalaam miaka ya 90..Ubadhirifu haujaanza leo,kumbe ningeweza kusomeshwa na serikali bure wakati huo?.Rafiki zangu wengine wameniambia..'kwa nini umelipa'??Kazi ipo

    David V

    ReplyDelete
  3. CCM kwanini hamtaki kubadilika?Ile 'staili' yenu imeshapitwa na wakati..vijana wanakua,wanasoma,teknoljia,nk.Na wakiachia ngazi wataifishwe mali zao..Nina hasira sana wiki kadhaa zilizopita nililipa mkopo(deni?) niliopewa na serikali wakati nasoma chuo kikuu cha Daresalaam miaka ya 90..Ubadhirifu haujaanza leo,kumbe ningeweza kusomeshwa na serikali bure wakati huo?.Rafiki zangu wengine wameniambia..'kwa nini umelipa'??Kazi ipo

    David V

    ReplyDelete
  4. Katumwa huyo.

    ReplyDelete
  5. kabwe hukuna anayeweza kukufikia kwa kiwango chako kwanza cha kujua ulichokifuata hapo dodoma, pili kuwa mzalendo zaidi-mungu akuongoze usije kubadilika maaana zilishaanza tetes kuwa umepewa mlungula na hao magamba ccm ili ukae kimya, tatu una ushawishi sana kijana nikimaanisha unakubalika ile mbaya-kaza kamba na usije ukaacha siku za usoni kugombea urais tafadhali tuombe uzima tu mbona utapata kilaini sana..hakika wazee wako popote walipo hawatajuta kukupeleka shule maana umeenda na ukajua ulichokiendea na matunda yake ndo haya,unatufaa sote sio wazazi wako tu...ushauri wangu wa mwisho ni kutomsahau Allah kamwe maana usije ukawa furahani duniani tu halafu Akhera ya milele ukateseka kaka...hadi kwa umri wangu huu sijapata wa kumkubali kisiasa kukushinda (sio kwa mambo ya imani)lakini sina chama chochote cha siasa ingawa wazee wangu ni ccm..ningefurahi sana sana kama nitapata kadi ya uanachama wa chadema kutoka mikononi mwako..usipuuze hili

    nipo hapa loptz@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  6. Wewe anonymous hapo juu unayesema ''katumwa huyo'' inaelekea wewe ndio kati ya mafisadi na mbinafsi huna hata aibu na uzalendo wa Taifa lako. Unasikia pesa za walipa kodi zimeliwa halafu unafanya mzaha????
    Tuko ughaibuni tunapiga box wenzetu huko wako serious hakuna mzaha na pesa za walipa kodi ndio maana wameendelea. Ona China waliko leo hii, ni kwasababu wako serious katika mambo kama hayo, tena wananyonga kabisa.
    Inasikitisha sana, madini, gas, mafuta, kilimo nk bado tunategemea misaada hadi leo.
    Safi sana Kabwe, endeleeni kuitetea nchi hii, manake kuna wachache wanafikiri ni mali yao. Tuko pamoja nanyi Operation Uwajibikaji.

    ReplyDelete
  7. WISHING YOU ALL THE BEST.

    ReplyDelete
  8. MICHUZI LEO TUNASUBIRI NEWS ZA BUNGE TUSHIBISHE KILA BAADA YA NUSU SAA KINACHOENDELEA HUKO. TUMECHOKA

    ReplyDelete
  9. All the best Muheshimiwa Zitto. Unfortunately Madam Spaker will disappoint not only you, but the Majority in this country. She has got a chance to show the world kwamba she love this country. She will be mislead and ignorant by not giving this motion a chance to be debated. Let the motion pass. Let the wabunge debate it. Many issues will be clarified during the motion debate and speak has chance of giving every one, MPs and Minister a platform to debater and clarify issues. I know, with CCM majority the govt will win. BUT MADAM SPEAKER, lipe heshima bunge lako, wape heshima wananchi wako, put the country first and make history. Serikali haiwezi kuanguka, wananchi tutaona nani mzalendo na nai si mzalendo.

    ReplyDelete
  10. Hongera Zitto tupo bega kwa bega nawe mpaka kieleweke
    Mwai-p

    ReplyDelete
  11. safi sana kaka! tupo nyuma yako!

    ReplyDelete
  12. Anything is possible if you put your mind to it, Yes we can Asante Zitto Mungu akubariki kwa kuwaonesha watanzania kwamba wana uwezo wa kufanya mabadiiliko hakuna kisichowezekana.

    ReplyDelete
  13. safi sana Zitto kila la kheri kaka

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...