Salam sana toka humu jijini Paris. Habari ndugu wabongo nawana-blog babkubwa ya bwana Issa Michuzi. Leo hii waungwana wakitambua haki zao za kiraia walijisogeza katika boksi lakuchagua kiongozi atakayeshika mamlaka ya dola ya nchi kama rais hapa Ufaransa. Nikiwa kama mtanzania, na mhusudu siasa kwakiasi fulani pia kutokana namasomo yangu ya uzamivu-katika falsafa ya siasa sikusita kujivinjari mtaani kudodosa hili na lile.
Duru ya kwanza ya uchaguzi mkuu wa rais wa Ufaransa imefanyika leo, jana jumapili tarehe 22/04/2012 huku ukiwashirikisha wagombea 10 wavyama mbalimbali. Ikumbukwe kuwa hapa wenzetu wanafanya uchaguzi wa rais tofauti na wabunge sio siku moja  kama sisi hapo kwetu bongo, aambapo uchaguzi mkuu hushirikisha wabunge na rais.

Kwa staili hii tumeshuhudia rais Nicolas Sarkozy wa chama cha “Union for a Popular Movement (UMP)” anayemaliza muhula wakwanza wa uongozi miaka mitano akining’inia kwenye uzi mwembamba kwakupata asilimia 27%  na Yule mgombea wachama cha kisoshaliste (Socialist Part)  ambacho hakijaongoza tangu mwaka 1988 akitamba kwa kupata asilimia 29%. Marine Le Pen wachama cha mrengo wa kulia nachama chake cha Front National-(FN )chenye msimamo mkali kuhusu sera za uhamiaji nakulinda ajira kwakutoa kipaumbele kwa wazawa alifuatia kwa kupata asilimia 20% yakura zote.
Nicolas Sarkozy amekuwa akishutumiwa kwa kushindwa kuimarisha hali uchumi wanchi huku hali ya ajira ikiwa tete. 

Ndugu Mbongo pengine utakumbuka pia hotuba yake aliyoitoa pale Dakar Senegal- mwaka 2007 akishutumiwa kuwadharau waafrika, hali hiyo na yale matukio ya nchini Libya na Ivory Coast ambapo alishiriki kwa karibu sana pia yamemfanya akose mshiko na hata jeuri ya kukutana na waafrika waishio hapa ambao hufanya wastani wa asilimia 15 ya wafaransa. Staili yake yauongozi na matumizi mabaya ya nguvu hasa zakijeshi pia siasa zake zakimataifa haziwafurashi wenyeji wengi hapa.
Wasomi hao wenye asili ya Afrika waliitisha mkutano wao huku wakimualika François Hollande ambaye anaonekana kupendwa na watu wengi hasa wale wa maisha ya kawaida-huku akitumia mbiu ya “MABADILIKO NI SASA” kuja kuwasalimia. Hakika Hollande ameonekana kuwa na mshiko na mvuto kwa rika na watu wakima cha wastani na wale watabaka la chini na hasa wafaransa wenye asili ya kigeni.
Ikumbukwe pia wa-Afrika hawa ni hasa wale wan chi za “francophone” nchi zitumiazo lugha ya kifaransa. 
Kutokana na mfumo wa uchaguzi nchini humu, baada ya duru hiyo ya kwanza, mchujo sasa wamebakia wagombea wawili ambao watapigiwa kura tarehe 6/05/2012, siku ambayo itaamua nani atashika hatamu ya uongozi kama rais mpya wa Ufaransa.  Ndugu endelea kunifuatilia juu ya hili nitakujuza zaidi kupita blog hii pia kwa picha za mambo yatakavyokuwa. Kwa ufupi nikuwa hali ya rais Nicalas Sarkozy ni ngumu kutabiri kama atashinda au la. Duru za kisiasa zinatabiri ushindi kwa chama cha kisoshialisti, (Socialist Part,) cha bwana François hollande. Kaa karibu nitakujuza zaidi.
 
Imeandaliwa na mpenzi wa Globu ya Jamii mojakwamoja toka katika viunga vya Paris; Frederick Meela-Mtanzania masomoni Ufaransa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nicholaus Sarkozy:

    Bingwa wa Majungu na Mipango ya kutuma Madege ya NATO kung'oa Maraisi ya nchi zingine kwa nguvu za Kijeshi,,,

    Angalia ameratibu matukio ktk nchi zilizowahi kutawaliwa na Ufaransa,kama Tunisia, Ivory Coast,Chad,Guinea,Mali,Libya na kwingineko.

    KWA NGUVU ZA MWENYEZI MUNGU NAYE SASA AROBAINI YAKE IMEFIKA UCHAGUZI WA MWAKA HUU ANARUDI SHAMBANI KULIMA ZABIBU!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...