Rais wa Zanzibar Dkt Mohamed Ali Shein kiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kwenye makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Unguja leo

Watoto wa marehemu wakiweka shada la maua
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka mchanga katika kaburi la Brigedia General Mstaafu, Adam Mwakanjuki, wakati wa maziko yake yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Unguja leo
 Mke wa Marehemu Brigedia General mstaafu, Adam Mwakanjuki, Bi. Ikupa Mwakanjuki, akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu mumuwe, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kwenye makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Unguja leo.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein leo ameongoza Maelfu ya wananchi na viongozi mbali mbali wa Serikali katika mazishi ya aliyekuwa Brigedia Jenerali Msataafu Marehemu Adam Clement Mwakanjuki ambayo yamefanyika Makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar.

Mazishi hayo ambayo yalifanyika kwa heshima zote za kijeshi kwa kupigwa mizinginga 11 baridi, yalihudhuriwa pia na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dk.Gharib Bilal,Rais Msaafu wa Zanzibar Aman Abeid Karume,na viongozi wengine wa ngazi za juu wa Vyama vya siasa na Serikali.

Akitoa salamu za Serikali mazishini hapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed amemuelezea marehemu Mwakanjuki kuwa alikuwa mtu muadilifu na mwenye busara ambapo kifo chake kimetokea likiwa Taifa la Watanzani bado linamuhitaji.

Waziri Aboud amesema Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu alikuwa ni kiongozi Jemedari na shupavu ambapo aliweza kulitumikia vyema Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa uadilifu mkubwa jambo ambalo lilimjengea sifa hata katika siasa.

Amemuelezea Brigedia Jenerali Mwakanjuki kuwa alikuwa ni kisima cha ushauri,nasaha,maelekezo,busara siyo tu kwa masuala ya kisiasa na kijamii bali pia masuala ya kiuchumi.

Marehemu alipata Elimu yake ya msingi Skuli ya St.Paul Kiungani Zanzibar mwaka 1947-54 na kujiunga na Elimu ya Sekondari ya St.Andrew ya Minaki jijini Dar es Salaam na kupata Elimu ya Juu katika Chuo cha Fritz Heckert nchini Ujerumani ambapo alipata masomo ya siasa 1960-1962

Mwaka 1964-1968 Marehemu aliajiriwa Idara ya Mambo ya nje ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya kujiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania mwaka 1969.

Mwaka 1972-1979 alikuwa Mkuu wa Vikosi vya JWTZ na JKT ambapo mwaka 1980-1981 Brigedia Jenerali Mwakanjuki alikuwa Kamisaa wa Divisheni ya 20 ya JWTZ.

Aidha Marehemu alipata mafunzo mbali mbali ya uongozi katika Chuo cha Taifa cha Uongozi Monduli na kupanda vyeo hadi mwaka 1988 alipopata cheo cha Brigedia Jenerali hadi mwaka 1994 alipostaafu Jeshi.

Kabla ya kifo chake Marehemu aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zikiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba na Utawala Bora,Waziri wa Kilimo,Mifugo na Mali Asili,Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi,Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Marehemu amefariki akiwa na umri wa miaka 
73 ameacha Kizuka na watoto saba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...