Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu Brigedia Jenerali Mwakanjuki mapema leo asubuhi katika kambi ya jeshi kikosi cha anga jijini Dar es salaam kabla mwili haujasafirishwa kwenda Zanzibar kwa Mazishi
 Familia ya marehemu ikielekea kupanda ndege

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein kufuatia kifo cha mwanasiasa mkongwe Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki aliyefariki dunia katika Hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo jijini Dar-es-Salaam jana tarehe 19 April, 2012.

Marehemu amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi visiwani Zanzibar zikiwemo za Uwaziri katika Wizara mbalimbali na pia kuwahi kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.

"Pokea rambirambi zangu za dhati kwa kuondokewa na mzee wetu, kiongozi shupavu na mwanamapinduzi imara, ni pengo kubwa kwetu kwani Marehemu amekuwa mshauri wetu mkweli na muwazi, upendo na ucheshi wake pia ilikuwa faraja kwetu wakati wa vipindi vigumu na vyepesi" Rais ameeleza,
"Tutaukosa  ushauri wake, upendo wake na mchango wake katika kila hali"  Rais amesema na kumuomba Rais Dk. Ali Mohamed Shein kufikisha salamu zake za rambirambi kwa familia, wananchi wote na viongozi wenzake ambao marehemu amefanya nao kazi katika idara zote  serikalini, jeshini, na pia katika Baraza la Wawakilishi.

Marehemu Mwakanjuki alianza Siasa kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 akianzia katika Chama Cha Afro Shiraz (ASP) na baadae Chama cha Mapinduzi. 

"hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwa mchango wa marehemu wakati aw uhai wake nasi twamuombea mapumziko mema ya milele, Amina" Rais amemuombea Dua na kuiomba familia ya marehemu kuwa na subira wakati huu wakuondokewa na mpendwa wao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...