Ndugu Issa Michuzi. Asalaam Aleikum Warahmatullahi Wabarakatuh. Mimi ni mfauatiliaji mzuri sana wa blogu yetu ya jamii. Kwanza nakushukuru kwa jitihada zako za kutujuza habari mbali mbali za ndani na nje ya nchi yetu ya Tanzania. Mimi ni mzaliwa na mkazi wa Zanzibar ambaye anapenda amani na muungano wetu

Mosi, napenda kutoa masikitiko yangu makubwa ya uvunjifu wa amani na uharibifu wa mali yaliyotokea hapa Zanzibar, ambayo yalisababishwa kundi la watu waliopoteza mwelekeo na kuficha hila zao chafu nyuma ya dini yetu tukufu ya kiislamu. Tabia za hawa waislamu wachache wakichochewa na wanasiasa wenye hila chafu na huchu wa madaraka Imeikashifu dini yetu tukufu ya kiislamu na kuipa sifa mbaya ya chuki.(Quran 25'63)

Uislamu, Dini ya rehma, hauruhusu ugaidi na umwagikaji damu. Katika Qur-aan, Mwenyezi Mungu Amesema: "Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu Huwapenda wafanyao uadilifu." (Qur-aan, 60:8). Baadhi ya hawa watu walioondoka kwenye maadili ya kiislamu wamechoma makanisa wakidai kutengana

kitendo cha kuchochea khofu katika nyoyo za raia wasio na ulinzi, uharibifu wa majengo na mali, makanisa ulipuaji mabomu na kuwalemaza wanaume, wanawake na watoto wasio na hatia, yote haya yamekatazwa, tena ni matendo ya kuchukiza kwa mujibu wa Uislamu na Waislamu. Hizi ni tabia za kishetani. Waislamu wanaifuata Dini ya amani, huruma na msamaha, na wengi hawahusiani na matukio ya vurugu ambayo baadhi yamehusishwa na Waislamu.

Kadhalika, Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema, Ikiwa Muislamu mmojawapo atajihusisha na kitendo cha kigaidi, mtu huyo atakuwa katika hatia ya kukiuka sheria za Uislamu.Kama wanataka kujiondosha kutoka kwenye muungano, basi wafuate njia za amani na siyo vurgu. 

Napenda kumpongeza na kumshukuru kijana Jonh Mashaka kwa hekima , umahiri busara na ukomavu ambao ameuonyesha katika kuilemisha jamii yetu. Tumwombee Allah Subhaanahu Wa Taala amzidishie ujuzi, elimu na subra ili azidi kutuelemisha na kutumia kipaji chake kwa manufaa ya taifa letu.

Kwa niaba ya watanzania wenzangu , wakirsto na waislamu wapenda amani, napenda niseme kwamba, tatizo la majuzi hapa zanzibar haikuwa ya kidini, bali tatizo la watu wachache wenye akili potofu wanaojaribu kuiteka na kuikashifu dini yetu tukufu ya kiislam. Napenda pia kumuomba Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe, ambaye pia ni mwislamu, kama mwanasiasa, lazima awe mwangalifu sana kwa matamshi yake, kwani kuongea bila kuwa makini kunaweza kutafsiriwa kama uchochezi wakati taifa inapitia wakati mgumu. Nchi Haiwezi kjendeshwa kwa uropokaji. Ili kuwa mwanasiasa bora, siyo lazima uzungumzie kila kitu

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.Tunaomba amani idumu katika taifa letu tukufu la Tanzania. Waislamu hatuna chuki na wakristu popote pale
Udumu muungano

Asalaam Aleikum
Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2012

    asante sana mdau. Umesema ukweli mtupu. hata na sisi wakiristo hatuna chuki na ndugu zetu waislamu. tumeishi pamoja kama ndugu kwa kipindi kirefu bila mtafaruku wa aina yoyote.

    nasikitishwa sana na kauli za huyu mbunge Zitto Kabwe. Zitto ameshajiweka kwamba anajua kila kitu. Hakuna mwingine humu Tanzania mwenye umahiri zaidi yake. Ahachane na mambo ya kuongea ongea hovyo. Zitto anaropoka sana

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2012

    acha kuchanganya dini na siasa wewe.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2012

    HUU NI UJUMBE MZURI SANA KWA ZITTO KABWE. KAZIDI SANA KUROPOKA.
    WATANZANIA HATUJAWAHI KUWA NA CHUKI ZA KIDINI ISIPOKUWA HII INAYOLAZIMISHWA NA WATU KAMA JUSSA NA WAKINA ZITTO AMBAO MIDOMO YAO INAJUA KILA KITU. ILA MWAKA HUU KAZIMWA KAMA SIGARA

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 29, 2012

    Zitto kapata dawa yake mwaka huu, kwa maana kazidi kwa kutafuta umaarufu. facebook yupo, tweeter yupo, kila sehemu Zitto anatoa statement. Yaani mtu mmoja utajua kila kitu, bwana unajiharibia mwenyewe. safi mashaka amefanya kazi nzuri sana kumchambua zitto kisomi hasa

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 29, 2012

    kwanza: haya ndo mambo tunayoyataka. siyo sikuzote kuwaona waislamu kama maadui zetu.

    pili: mashaka akiingia chadema ndoto ya zitto ya urais itakufa kabisa. hachana na wakina mnyika, tishio la zitto ni huyu mashaka ambaye namhisi ni mwana ccm

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2012

    asante sana mdau kwa huu waraka wako mzuri. kweli waislamu hawajausika na vurgu zinazoendelea hapa zanzibar. nimefurahi sana jinsi ulivyo kuwa muwazi.
    ni dhahri kwamba mbunge zitto inabidi abadilike na fundisho alilopewa na mwenzake jon mashaka inatosha kabisa. tunawahitaji vijana makini kama mashaka kuwa katika uongozi wa hii nchi.
    hatuwezi kuruhusu umwagikaji damu hapa zanzibar. damu ya wazanzibari ina thamani kubwa na mwenyezi mungu hatotusamehe tukimwaga damu za watu wasio na hatia

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 29, 2012

    Mdau anaonekana amesikitishwa mno na fujo zinazoendelea unguja, lakini ni kweli hawa ni watu wa chache na agenda zao mbovu na kamwe hawataweza kuuitia uislamu matope kwani sote tunaelewa dini hii ni dini ya amani.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 29, 2012

    WATU TUSIWE KAMA IBILISI KUANZA KUMLAUMU ZITTO KABWE. YEYE NI MWANASIASA TU. KITENDO CHA SISI WAISLAM KUFANYA KITENDO KIOVU AU CHA KUVUNJA AMANI HAKUNA SEHEMU YEYOTE KWENYE HADITH AU QUR-AAN. NAWAHISI NDUGU ZANGU WAISLAM TUFUATE MISINGI SAHIHI YA DINI..TUJIULIZE TUNGEJISIKIAJE MISIKITI KUCHOMWA MOTO??
    NASIKITIKA TENA SANA KUONA KIZAZI KINAELEKEA UPANDE MBOVU. MIMI KAMA MUISLAM NA MWANAFUNZI NDANI YA CHUO CHA KIISLAM CHA KIMATAIFA TUACHE MAFUNDISHO KINYUME ALIYOTUACHIA MTUME WETU SALLAH LLAH ALAYHI WASALLAM AFDHAL ALKHALQ. NA NAOMBA WATU WARUDI KWENYE SIRA YA MTUME JINSI ALIVYODILI NA AHLU ALKITAAB.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 29, 2012

    Mdau nakushukuru vile vile kwa kujitokeza kutoa maoni yako na kutuelezea sisi wakiristo kwamba huna chuki na sisi.

    Lakini, inawezekana kitabu chenu tukufu kinapinga chuki ila nafikiri sehemu kubwa ya wafundishaji wenu wamekuwa wakipotosha Quran na kuleta chuki kati yetu.

    Tatizo la waislamu kuwachukia wakiristo liko sehemu nyingi duniani. Na kama nilivyosema kuna tendency ya wale waliosoma either dini na wanasiasa kutumia dini kuleta machafuko kwa maslahi yao.

    Na hili tatizo haliishi leo wala kesho.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 29, 2012

    hao mujahedeen na ma alshabaab wa zengy wakiachwa basi tutakoma. hao watatuftwe na dola, mmoja baada ya mwingine na kushugulikiwa kisawasawa. wahuni hao wapewe kichapo hata na mchochezi zitto. kwani wa zenji walimwambia wanataka mafuta yao hao gesi yao. watu wengine bwana

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 30, 2012

    You can quote all Koran chapters but the proof is in the pudding. 80% of conflicts or wars in the world are related to Islam religion. The idea that Muslims are being oppressed is everywhere from Hindu, Christian to Buddhist countries. I can caught chapters in the Koran that encourage violence against non-believers. When will they learn to live with people of other faiths?

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 30, 2012

    Watanganyika sisi Wazanzibar hatutaki Muungano,maanake viongozi wenu wa C.C.M wametia pamba masikioni. Huyo aloandika mada hiyo hapo juu nu usalama wa Taifa, sisi Wazanzibar sio wapumbavu tena, wallah tuuweni sote lakini Nchi yetu mutaiwachia.

    ReplyDelete
  13. "WARAKA WA AMANI" that could be the appropriate title. Mtoa waraka umeandika kwa ufasaha mkubwa sana, Allah akubariki sana. Mimi sio muislaam ila kwa waraka huu umenionyesha kuwa bado kuna waislaama wanaitikadi zilizotukuka kama zako tofauti na hao wengine waliokosa kazi na kutaka kuichafua dini yenu kwa mwamvuli wa muungano.

    ReplyDelete
  14. Zito gotta learn something here.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 30, 2012

    HATA NA MIMI NIMEANZA KUMSHUTUKIA HUYU ZITTO. MISIFA ZISIZOKUWA NA MBELE WALA NYUMA ZITAMMALIZA. SASA KAANZA MARA MWALIMU WANGU WA LUGHA, WAZHUMI NI WATU WA KUHESHIMIKA SANA, MARA HOO, SERIKALI 10. MARA MAFUTA, MARA GESI. KWANI WAZENJI WALIKWAMBIA WANATABU YA MAFUTA AU WANATAKA KUJITENGA? WEWE INAONEKANA HII NJAMA MLIPANGA NA RAFIKI YAKO JUSSA. SASA NA UCHUMI WAKO, SIJUI USOMI MBONA UMEANGUKIA KIFUANI. WEWE TAMAA YA MARADAKA YATAKUMALIZA KISIASA. ULIKUWA NA MWANZO MZURI ILA UMEPITILIZA KWA KUTAFUTA MISIFA. JIFUNZE SANA ZITTO SIASA NI MCHEZO MCHAFU NA WALA HATUTAKUVUMILIA UKIWA NI MTU WA UCHOCHOZI. INGETOKEA NDANI YA CHADEMA UNGELIA OHH UDINI, UKABILA, SIJUI KITU GANI. JIFUNZI KWA VIJANA WENZAKO WAKINA MASHAKA WANAOTUMIA USTAARABU NA UMAKINI KUZUNGUMZA KWENYE JAMII. KAMWE HATUTAKUBALI MUUNGANO WETU KUVUNJIKA KUTOKANA NA TAMAA YA WACHACHE. WANASIASA AMBAO HAWANA MBELE WALA NYUMA.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 30, 2012

    Anon May 30, 12:25 AM 2012 Can you quote those chapters? or Verses? Please?

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 30, 2012

    Kinachotakiwa ni zanzibar hayo mengine yalikuja kwa bahati mbaya sheikh! Muungano wa nini wakati Znz tuna uwezo wa kujitegemea?

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 30, 2012

    Je unauhakika kama waliofanya ni waisilamu?au ndio itakuwa yale ya chama fulani kila penye mauwaji huwambiwa chama kiku ndio kimefanya na hili ni lazima tuliangalie sana tusiwe tunavutiwa na hisia tu kuna viongozi wanahofia madaraka yao ikiwa kutatokea mabadiliko na badala yake viongozi kama hao wanweza kusababisha uvunjaji wa sheria ilimradi tu abaki katika madara kwa mfano kuna vitendo vibaya vilishamiri katika makanisa makubwa ya Ulimwengu zidi ya watoto wa kiume lakini huwezi kuwarushia kila mfuasi wa makanisa hayo uovu huo tuwe wenye kuzingatia sana (kikulacho kinguoni mwako)

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 30, 2012

    Zitto, hii iwe ni funzo kwako. jaribu kuwa mtu mnyenyekevu. mashaka ametuonyesha jinsi ulivyomdhaifu wa fikra, mchache wa hekima na muwazi kichwani. hizo digrii zenu za kuungaunga zinawaponza matokeo yake mnaanza kubwabwaja kutafuta misifa isiyo na kichwa wala miguu.hauwezi kujiingiza kwenye anga za wasomi wa kweli.... safi sana. kuanzia siku ya leo, utambue kwamba, kuna watu mahiri zaidi yako ambao wameamua kuwa kimya siyo kwamba hawawezi kuongea, ila wanaongea pale inapostahili. asante sana mdau kutuletea maneno mazuri ya amani. nyinyi ndio wapenda amani ambao dini ya kiislamu inawazungumzieni. inshallah mwenyezi mungu akujalie uishi maisha marefu.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 30, 2012

    zitto mshikaji wangu. ungenyamaza haya yote yasingekupata. Wakuu wako Dr. Slaa, Tundu Lissu, Kamanda Mbowe na wengine wote walinyamaza. Hawakutaka kukurupuka.Walinyamaza ili wakiongea waongee kwa sauti moja tena vitu ambavyo vinagusa watu wote. Wewe kiherehere utadhania mwanamke mwenye mimba kimekuponza. umeonyesha udhaifu mkubwa kama kiongozi, tena mkuu wa kambi ya upinzani bungeni? sijui ilikuwa ni ushindani na mashaka au ilikuwa ni kitu gani kina kuwasha. watu wengi sana wamekuja kwenye hii blog wakitaka kushindana na mashaka lakini wengi wao wamerudi kujificha kwa aibu. mtu tu ambaye naweza kusema alikula sahani moja na mashaka ni US BLOGS. Mwanasiasa mwingine unayeweza kusema yuko kwenye level moja na mashaka ni January Makamba.Yule dogo ni kichwa. ni huyo tu. bora ungenyamaza haya yote yasingekukuta, sasa hona umeingia choo cha kike ukajikuta mwenyewe, kila mtu anakuponda kwa kutafuta attention utafikiri demu. umechemsha mkuu. hata huko magwanda sasa hivi hauna heshima uliyokuwa nayo.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 30, 2012

    Jamani. zungumzieni mada. Mwacheni zitto. Mashaka na zitto hata siku moja wasilinganishwe. Mashaka amesoma vyuo vya hali ya juu marekani. Zitto amesoma UDSM. Kwa misingi hiyo zitto lazima apongezwe kwani pamoja na udhaifu wa vyo vyetu, bado ameweza kuonyesha umahiri mkubwa. Kwanza zitto anauwezo mkubwa zaidi ya mashaka kwa sababu mashaka alisoma na pia bado anaishi kwenye mazingira ambayo yanamuwezesha kwenda na wakati kisiasa. Ila ndugu yangu zitto na wewe pia punguza mambo yako ya kutoa matamko uchwara. tulia bwana

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 30, 2012

    mdau asante sana kwa maneno mazitoyenye wosia mzito. ni kweli dini ya kiislamu imetekwa na wahuni wachache ambao wameamua kuichafua. yote tumuachie mwenyezi mungu, kwani ndiye muumba na mwamuzi wa yote. jamani kama nitakosea mnisamehe? huyu mashaka si ndio yule anayeitwa mwanaharakati? nimewahi kuudhuria kongomano fulani ambako bw. mashaka ndiye alikuwa mzungumzaji mkuu. hii ilikuwa pale kinondoni biafra mwaka 2011. mashaka alihutubia. hotuba ilikuwa nzito, watu walitokwa machozi pale uwanjani. huyu kijana mashaka ana kipaji, nina uhakika kwa mtindo ule, atabadilisha taswira ya kisiasa hapa nchini kama ataingia kwenye siasa jambo ambalo siwezi kumshauri kufanya

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 30, 2012

    Jamani tuache ushabiki. Mtoa mada hii hakika ameonyesha hekima kubwa. Mi si muislamu lkn kanigusa. Kwa mtazamo huu kumbe tunaweza tukaishi na kuvumiliana. Ndugu zangu Wazanzibar kama hamuutaki muungano hakuna haja ya kuchoma makanisa au kuharibu mali. Kwa kufanya hivyo madai yenu ya kutotaka muungano yatakuwa dhaifu kama si kufa. Na kama hayatakufa hakika nawaambieni yanatoa ishara mbaya kwenu kwani hata mkifanikiwa kujitenga, wakristo na watu wa imani nyingine nje ya uislamu hawatakaa salama Zanzibar (si mtachoma nyumba zao za ibada, mkiwaambia warudi bara utafikiri watu wa imani nje ya uislamu waishio Zanzibar wote ni wa bara. Kumbukeni mmeanza na wakristo, eti warudi bara).Mkiwamaliza hao mtakwenda kwa wa imani nyingine na mkiwamaliza mtatafutana wasunni na washia, safari hii sijui mtawaambia hao wasunni au washia hawajui kuswali na pia sijui mtawaambia warudi/waende wapi. Ombi langu ni kwmb hatujachelewa, tukae chini kama ndugu na tuongozwe na busara alizotupatia Mungu (katupa akili na hekima kuliko viumbe wengine) tuyazungumze na tuone ni lipi la kufanya kuhusu hoja yenu ya kutoutaka muungano. Kinyume na hapo nauona mustakabali ulio na walakini wa Tanzania. Nimpongeze tena mdau kwa mada yake nzuri ambayo binafsi imenigusa. Ubarikiwe Mdau na Mungu Ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 30, 2012

    Mdau Anonymous wa Wed May 30, 12:52:00 AM 2012

    ...Watanganyika sisi Wazanzibar hatutaki Muungano,...

    SISI WA BARA TUNACHOTAKA NI USTAARABU, MDAI KUVUNJA MUUNGANO KWA NJIA ZINAZOKUBALIKA NA SIO KWA NJIA ZA MAUAJI NA UHALIFU HUKU MKIITUMIA VIBAYA DINI NZURI YA KIISLAMU!

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 30, 2012

    Anon May 30,12:25 AM 2012, tunasubiri hizo chapters za kwenye Quran zinazochochea fujo!!!

    Am afraid u know nothing about Quran, hakuna sehemu kwenye Quran inayochochea fujo, Uislam ni dini ya amani,unyenyekevu na inamtaka kila mmoja anapoona kitu kiendacho nje ya uislam basi akikemee. Tatizo utakuta mtu anamwangali mtu fulani as an individual then ana generalize 'waislam bwana...' inatakiwa watu waangalie uislam unasema nini sio mtu anafanya nini

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 30, 2012

    Zanzibari ina Wakazi 5 Milioni, wakati ninyi (KUNDI DOGO MSIOTAKA MUUNGANO) hamfiki 1 Milioni ina maana wanaounga mkono kama Mdau aliyeandika watakuwa 4 Milioni.

    Kwa hiyo haiwezekani ninyi watu Milioni 1 (wachache) mtekelezewe Madai yenu halafu (walio wengi) Milioni 4 wasipewe !

    HII HATA KTK KANUNI ZA KIDINI NA PIA ZA KIDEMOKRASIA HAIKUBALIKI !

    SULUHU:

    ...MSIOTAKA MUUNGANO MHAMIE ARABUNI...

    ReplyDelete
  27. Nimependa kweli mdau alivyoelezea kuhusu yaliyojiri ZNZ.

    Mimi ni mkristu na ndugu zangu waislamu nawapenda sana na kuheshimu dini ya kiislamu kwa sababu naamini Mungu ni mmoja na yeye anatusihi daima tupendane.

    Kama unamjua, unamheshimu na kumwogopa Mungu, daima utamtendea mema jirani yako bila kuangalia tofauti zozote alizonazo. Mungu atusaidie watanzania tupendane na kamwe tusitengane kwa sababu zozote zile. Kwa jina la Yesu, AMINA.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 30, 2012

    WAPINGA MUUNGANO:

    Mtumie njia za Busara kuyafikia malengo yanu na sio kujificha nyuma ya Dini Tukufu ya KIISLAMU!

    HATA SISI WA BARA UISLAMU SAFI TUNAUJUA!

    NI LAZIMA MTOFAUTISHE KATI YA UISLAMU NA UHALIFU!

    KAMWE:::::

    UISLAMU SI UHALIFU !!!

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 30, 2012

    MIE BINAFSI SIJAELEWA KWANINI WATU WANAONA WAISLAMU NI WAKOROFI LAKINI HAWASEMI KUHUSU UISLAMU KUHUJUMIWA DUNIANI HIVI SASA, ZANZIBAR NI YA WAISLAMU NA ILIKUWA NA MAADILI MAZURI YA KIISLAMU AMBAYO HAKUNA HATA DINI MOJA INAWEZA IKAJISIFU KWENYE MAADILI LAKINI HUU MUUNGANO LENGO LAKE NI KUHUJUMU UISLSMU NA NDIO MAANA UNANG'ANG'ANIWA SANA KWANI WAZANZIBAR WAKIJITENGA KUNA TATIZO GANI NCHI NGAPI NDOGO ZINAJITEGEMEA KWANINI MUUNGANO USISHIRIKISHE WANANCH WA ZANZIBAR WAPIGE KURA ZA MAONI, MIE NADHANI VURUGU ZINATOKANA NA WANAOTAKA MUUNGANO KWA MASLAHI YAO KUJIFANYA VIBURI MBONA VURUGU ZIKIANZISHWA NA CHADEMA TUNAISEMA SERIKALI AU KWA VILE ZANZIBAR NI WAISLAMU HATUTAKI KUWASAPOTI WAJITEGEMEE, MIE NADHANI WATU WANASUBIRIA MAMBO KAMA YA DAAFURI
    WAZANZIBARI KUWENI NA MSIMAMO MAADILI, UCHUMI USTAARABU WENU VINAPOROMOKA SIKU HADI SIKU KUTOKANA NA MUUNGANO
    LINI ULISIKIA VIMINI ZANZIBAR WAKATI WA KARUME MUASISI?

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 30, 2012

    Zitto na wabunge wengine waropokaji na walalamikaji bila vitendo wajifunze. Na shule kubwa inapatikana kwa kijana mwenzake anayeitwa January Makamba au "February" kama alivyomwita Masanja. Yule anajua nini maana ya kuwa mbunge na siyo kutaka umaarufu tu kwa kuongea......

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 30, 2012

    Kama Wazanazibar hawawataki wabara basi na wapemba warudi na Wazanibar wote warudi kwao. kama wataweza kuzifanya biashara zao huko kwao. Soko kubwa la biashara zao liko bara. Hao Waarabu wanawadanganya na hiyo misaada ya hapa na pale.

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 30, 2012

    Mdau ahsante kwa Makala nzuri kabisa.

    Ni lazima wakorofi hao Zanzibar waelezwe ya kuwa:

    1.UISLAMU na UHALIFU ni vitu viwili tofauti!

    2.Huwezi kutekeleza UISLAMU kwa kupitia UHALIFU!

    3.Kamwe maji yasivyo changanyika na mafuta, kamwe UHALIFU hauwezi kuwa pamoja na UISLAMU!

    4.Kuwa MHALIFU sio kigezo cha UISLAMU SAFI!

    5.UISLAMU DAIMA UNAKATAA UHALIFU!!!

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 30, 2012

    ZANZIBARI NI SEHEMU YA TABORA!

    HAIWEZEKANI KUVUNJA MUUNGANO!!!

    Jaribu kuwauliza wengi wa hao hao Wazenji utasikia ohhh mimi Mnyamwezi,

    Je inaingia akilini mtu akadai Zanzibar iwe Arabuni wakati Zanzibar ni sehemu ya Tabora?

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 30, 2012

    Itakuwa ni Jiografia ya kipuuzi kabisa mtu akidai kuwa Zanzibar ni sehemu ya Arabuni wakati Zanzibar ni Tabora tu!

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 30, 2012

    Zitto Kabwela ameshindwa kuendeleza mkoa wake. Sasa anataka ahamie kwenye masuala ya Dini, hana maana yoyote kwa mkoa wake na Taifa kwa ujumla

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 30, 2012

    Sasa Zitto wa watu kakosea nini? Kuweka mambo wazi kwa faida yenu watu wa Zanzibar ni kosa? Kwa nini msingeutumia ukweli huo kuvunja muungano kwa amani kama kweli hilo ndo lilkuwa tatizo? Hata hivyo nia wasiwasi kuwa Zanzibar inataka kujitenga ili iwe kituo cha kigaidi kama walivyo Alshabaab, Boko haram n.k.

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 30, 2012

    Ahsante Mdau:

    Aliyeandika Makala hii ndio miongoni mwa Wazanzibar wachache waelewa!

    Wanaounga mkono Muungano ni watu wenye mtazamo wa mbali na werevu na wenye akili.

    Mfano tatizo la Ugumu wa maisha lipo Dunia nzima linalokwenda sambamba na Kudorora Kiuchumi na Kifedha mambo ambayo Serikali (achilia mbali hiyo ya Zanzibar sema hizo za Ulaya na Marekani Wanauchumi wanafuta jasho za vipara wakitafuta suluhisho, na bado inakuwa vigumu kupata majibu ya haraka na ya miujiza)!!!

    KUPATA MAJIBU YA NAFUU NA KUONDOA UGUMU WA MAISHA.

    WAANGALIE HUKO KWA WAARABU WADHAMINI WANAOWATEGEMEA MAMBO NI MAGUMU ZAIDI WANAANDAMANA KILA KUKICHA 'ARAB SPRINGS'

    Wazanzibari watazame mambo kwa upana zaidi wasije kufanya maamuzi na baadae wakajuta!

    MKATAA PEMA PABAYA PANA MWITA!!!

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 30, 2012

    Wazanzibar wale wasiowaelewa:

    Ukiacha Mdau muungwana aliyeandika Makala hii pamoja na watu makini kama Maalim Seif Sharrif Hamad, wengi wapinga Muungano ni 'mabwege' wasioelewa chochote kuhusu Dunia inavyokwenda!

    NI JAMBO LA AKILI KUTOFAUTISHA MAMBO MAWILI HAYA CHINI:
    ...................................
    1.UGUMU WA KIMAISHA UNAOKWENDA PAMOJA NA MABADILIKO YA DUNIA:-

    Ni wazi kuwa Dunia nzima imefilisika Kifedha na Kiuchumi, kwa sababu amefilisika Mwarabu (Huyo Bosi wenu na Mdhamini wenu mkubwa mnayemfikiria hasa kwa Jeuri na kiburi mnachofanya sasa),Mwarabu mwenye Utajiri wa Mafuta pamoja na Mzungu mwenye kufanya mambo yake kwa umakini wa hali ya juu wamefilisika KIFEDHA NA KIUCHUMI,,,ije kuwa Ninyi Zanzibari wenye uchumi wa kumiliki samaki watatu na nusu(3.5), na ng'ombe 7 wa kuvuta Mikokoteni?
    ...................................
    2.UWEZEKANO WA KUWAFIKIA WATAWALA WA KIMAMLAKA ,KISERIKALI NA KISIASA NA KUSIKILIZWA HADI MATAKWA YAKAFANYIWA KAZI:-

    Sio kweli kuwa Wazanzibari wote hawautaki Muungano!

    Wapo Wazanzibari kama aliyeandika hapa Makala hii hawataki kusikia juu ya kuvunja Muungano sio kwa vile wana Maslahi bali wanaona mbali zaidi yenu ninyi 'Mabwege' wachache mnaofikiri labda kujitenga ndio kutaweza kutatua njaa yenu kitu ambacho sio kweli!.
    ...................................

    KWA HIVYO SERIKALI (YA MAPINDUZI ZANZIBAR) HAIWEZI KUTEKELEZA MAONI YA WACHACHE NA KUWAACHA WENGI, UTARATIBU HUO UNATUMIWA NA NCHI ZOTE DUNIANI.

    TENA KWA TAARIFA YENU HATA ZIKIPIGWA KURA ZA MAONI ITAONEKANA WANAOTAKA MUUNGANO UENDELEE WATAWAZIDI MSIOTAKA MUUNGANO KWA HIYO SIO RAHISI MFIKIE LENGO, LABDA NJIA MBADALA NI KUHAMIA HUKO ARABUNI MNAKOTEGEMEA MKAOMBE URAIA HUKO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...