Hoja Yangu,

Mimi Kama mpenzi mkubwa sana wa club yetu ya Simba nimekuwa nikifuatlia kwa makini sana kauli zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya viongozi wetu hasa baada ya kifo cha kijana wetu mchezaji mahari kwenye Kiuongo marehemu Patrice Mutesa Mafisango. 

Hakuna ubishi kwamba huyu kijana kacheza season moja tu Simba na kafanya mambo makubwa sana lakini hakuwa na jina kubwa kwasababu waandishi wetu wa habari Tanzania ambao mimi huwaita waandishi uchwara hawakuwa wanampa nafasi ya kutosha kwenye magazeti yao au radio zao, ni aghalabu sana kupata mchezaji anacheza namba sita alafu akafunga magoli 12 na waandshi wa habari wasitoe nafasi ya kutosha kusifu ama kutambua mchango mkubwa kama huo.

Suala la pili lililonisutua ni ile kauli ya mwenyekiti kwamba jersy namba 30 haitavaliwa tena!!! naamini hili mwenyekiti hakulifiria sana na mimi sioni mantiki hasa ya kutovaa jersy hiyo. Naomba tutambue michango iliyotolewa na wachazeaji wetu wazamani lakini jersy zao zinaendelea kutumika hadi leo. ni nani hakumbuki mchango wa Edward Chumila, Ramadhan Lenny na wengine wengi lakini hatunao duniani. 

nalisema hili kwasababu Mafisango hakufia uwanjani. Naamini mwenyekiti alizungumza kwa kuteleza au jersy hiyo haitatumika kipindi yeye akiwa madarakanivinginevyo sioni maana halisi ya kutovaa jersy No 30.

Idrisou anavaa jersy No 17 Cameroun, jersy iliyokuwa ikivaliwa na Mac Vivien Foe pamoja na kijana huyu kufia uwanjani ikiitumia timu ya taifa.

Nawasilisha

Rwebu
Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2012

    wote waliotangulia mbele za haki vifo vyao havikuwa sawa na mafisango.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2012

    Mdau uliewasilisha mada, nashukuru kwa kuliona hilo, inawezekana ni kweli hakuna Mantiki kwa kuistaafisha jezi namba 30 ila tu ni kwamba wanaSIMBA wote tunakubali kuwa walikuwa wachezaji wetu MAHIRI sana kuwahi kuwepo ndani ya SIMBA SC ila tu ni kwamba hakuna kati ya hao uliowataja ambae alifariki akiwa MCHEZAJI active wote walifariki baada ya kustaafu soka

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2012

    mdau, kwanza kumbuka tu kuwa kuna tafauti kubwa baina ya timu ya taifa na timu za kawaida.

    timu inapoamua kuwa jezi number fulani haitovaliwa (retired) tena hiyo ni ishara ya kuheshimu alokuwa mtu wa mwisho kuivaa, sio kuidharau la hasha. Timu nyingi tu duniani zinafanya hivyo, sio kwa wachezaji wanaliokufa, bali wale ambao wameacha kucheza au kuhama club zao baada ya kuichezea kwa muda mrefu na kwa mapenzi ya hali ya juu.

    Kwa ufupi ku-retired jezi ni heshima kwa Mafisango. Tatizo lako na la wengine ni hii tabia ya nchi yetu kuiga kila linatendeka nchi nyengine na kufanya bila ya kutowa maelezo ya kutosha ili wananchi waelewe maana ya vitendo hivyo.

    ReplyDelete
  4. Ahsante sana mtoa mada, kwakweli umesema mawazo yangu. Mimi sio fan wa Simba ila pia sikuona mantiki ya kutovaliwa tena kwa jezi namab 30. Ni jezi ngapi zitafutwa pindi wachezaji mahiri wa sasa wa simba wakirudi mavumbini? Tunaheshimu msaada wa mafisango kwa msimu aliocheza ila hakukua na sababu ya kufutwa kwa namab30.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 29, 2012

    ni kweli mafisango hakufia uwanjani lakini alikufa akiwa bado mchezaji wa simba. nawathamini sana magwiji wetu lakini wote chumila na leny walikufa wakati wameshaacha soka. mbona maradona hakustaafu soka akiwa napoli lakini jezi yake haivaliwi tena ilhali wapo waliostaafu soka wakiwa napoli na jezi zao bado zinavaliwa?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2012

    Nadhani Hussein Tindwa ndio alistahili heshima hiyo (ya jezi yake kutovaliwa). Alikufa wakati akiiitumikia Simba uwanjani. Mambo ya kufanya maamuzi kwa kukurupuka hayo!!

    ReplyDelete
  7. Huo ni mtazamo wako mdau wala hauwezi kupima kiwango cha heshima aliyoamua kuitoa Mwenyekiti wa Simba kwa Marehemu Patrick Mafisango. Nilipoanza kuusoma mchango wako nilianza kushawishika na Hoja yako ila mfano ulioutumia kuthibitisha hoja yako umetia dosari uzi wako baada ya kubaini upotoshaji wa makusudi ulioamua kuufanya hapo. Camerun wameamua kuendelea kuitumia jezi ya Marehemu Mark Vivien Foe, lakini klabu yake ya Zamani mabingwa wa sasa wa Premeir League klabu ya Man City wao walimpa heshima ya kuiondoa kabisa katika huduma Jezi yake N0.37 ambayo imetunzwa katika museum ya Club. Kwa hiyo maamuzi ya RAGE NI SAHIHI KABISA KAMA MWENYEKITI WA SIMBA hakuna dosari katika hilo, wao wameamua kuumbuka mchango wa Mafisango kwa staili hiyo. Wapo wachezaji wengi wamefariki michezoni lakini klabu au timu za Taifa hazijaamua kuwapa heshima ya kumbukumbu.

    Yahya M

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 29, 2012

    Mdau uliyetoa hii status nakupongeza kwa hoja yako. Lakini napata shida na wewe kwa kuponda taaluma ya wenzako na kuelekeza kazi ya kufanya, huu si uatamaduni mzuri mnachopaswa kufanya ni kushauri siyo kuponda. Hata wewe katika taaluma yako kuna mangapi mabaya unayofanya au kwa vile hii ya uandishi wa habari inagusa kila mtu. Tanzania leo hii kila mtu anamuona mwandishi mtu asiyejua lolote bila kufahamu uandishi huohuo ndiyo unaomfanya aone kile kizuri kinachofanyika Ulaya au kwingineko. Umefika wakati kwa Watanzania kuwa na adabu na kazi za watu, hivi uchezaji mzuri wa Mafisango ndiyo kigezo cha kumuandika vizuri kila siku au nini hasa, kwani alipokuwa anafunga hakuandikwa. Au wewe ulitaka aandikwe kwa namna ipi ambayo hakuandikwa? Inauma sana kwa nchi yetu kuponda kila kitu hasa taaluma za watu. Tazama hata wasanii ambao ni 'wasanii' tu kama Mpoki anaponda eti waandishi wa 'miezi' mitatu hawana lolote, kesho anawafuata hao hao wamuandikie kuhusu tamasha lake la komedi huko Arusha au Mwanza. Kwa nini kila siku waandishi tu? Wala hamuoni watu wanaoyumbisha nchii kwa kuzembea katika taaluma zao lakini mmekaa kimya. Ninachokiona mimi ni kuthamini vitu vya nje na kudharau vyetu. Haya unaleta habari za kina Chumila na Mafisango kuhusu jezi, kila uongozi una falsafa zake. Enzi za Chumila, yawezekana Simba haikuwa na utaratibu wa naba ya jezi maalum kwa wachezaji wake, sasa hao viongozi wangezuia vipi? Pia jiulize Chumila alikufa akiwa anachezea Simba au baada ya kuondoka? Au mnakurupuka tu kisa mmekaa katika vijiwe vyenu na kujazana maneno. Tatizo siku hizi hawa waandishi wengi rafiki zenu mnaokaa nao mitaani kwa hiyo hata akifanya vipi huwezi kukubali hadi huwe humjui na umekutana naye tu mahala. TUHESHIMU TAALUMA ZA WATU WAKATI MWINGINE

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 29, 2012

    Kwa taarifa yenu Husein Tindwa na Saad Ali walikufa wakiwa active.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 29, 2012

    Ni maamuzi ya Simba SC kumuenzi Mafisango kwa jinsi watakayoona inafaa, Whats your Problem with That? RIP Mafisango!! You Will always be Remembered!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 29, 2012

    wewe vaa hiyo Jezzy namba 30 ila sisi wanaz wa kweli hatutaki kuona jezzy hiyo tena uwanjani!..tena acha kabisa kutukumbusha MUTU YA WATU wewe!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 29, 2012

    nilitegemea wadau wangeona tatizo, kwenda kuzika hamkwenda iweje mjifanye mnajua sana mchango wake acheni fitna zenu sudan mmeenda wote mpaka mkakosa pa kulala msibani je AIBU KUBWA KWA SIMBA.Endeleeni na sherehe ya ubingwa acheni kutuyeyusha

    ReplyDelete
  13. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHMay 29, 2012

    Huyu mafingo anayezungumziwa hapa kwa matukufu yote haya ndio yule ambae viongozi hawa hawa kina ADEN walimfungia kwa utovu wa nidhamu na chupuchupu aachwe kwenye safari ya ALGERIA kutokana na kibano hicho au mwingine?

    Tunapomsikitia mwenzetu alitangulia tusiwe wepesi wa kusahau,naungana na mdau aliesema Husein Tindwa ndio alistahili heshima hii aliyopewa mafisango,lakini nitamlilia mafisango kama mwanandinga mashuhuri wa ukanda wa CECAFA,lakini si mfano wa kuigwa na wachezaji chipukizi wa kikosi cha pili cha simba na wengine kwenye suala nidhamu

    ReplyDelete
  14. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHMay 29, 2012

    samahani,huyu mafisango ndio yule ambae viongozi hawa hawa walitangaza kumfungia kabla ya kwenda algeria kutokana na utovu wa nidhamu uliopindukia au mwingine?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...