Katibu Tawala Msaidizi - Mkoa wa Mwanza Bw. Ndaro Kulwijila akifungua mafunzo kwa mafundi Mchundo kuhusu njia bora za kuhudumia majokofu na Viyoyozi na umuhimu wa kuhifadhi tabaka la Ozoni. Mafunzo hayo ya siku mbili yameratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na yanafanyika Jijini Mwanza.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya Mafundi Mchundo wa Majokofu na Viyoyozi kutoka viwanda mbalimbali vya Jiji la Mwanza wakisikiliza kwa makini umuhimu wa kuhifadhi tabaka la Ozoni.
Katibu Tawala Msaidizi - Mkoa wa Mwanza Bw. Ndaro Kulwijila wa pili kutoka kushoto (waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Mafundi Mchundo wa Majokofu na viyoyozi kutoka katika viwanda mbalimbali vya jiji la Mwanza waliohudhuria mafunzo ya njia bora za hifadhi ya tabaka la Ozoni. Mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wakufunzi kutoka VETA Mwanza na VETA Kigoma.

Na Lulu Mussa

Imeelezwa kuwa Tanzania imefanikiwa kuondoa matumizi ya kemikali zinazoharibu tabaka la Ozoni kutoka tani 254 mwaka 1999 hadi tani 35.76 mwaka 2009. Hayo yameelezwa leo Jijini Mwanza na Bw. Ndaro Lulwijila, Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Mwanza katika hotuba ya ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya mafundi mchundo kuhusu teknolojia mbadala ya majokofu na viyoyozi.

Bw. Kulwijila ameainisha baadhi ya kemikali hizo kuwa ni methyl bromide, halons na chloroflorocarborns ambazo hutumika kama vipozi katika majokofu, viyoyozi, vifaa vya kuzima moto, usafishaji chuma, ufukizaji wa mazao katika maghala na utengenezaji wa magodoro ambazo huleta madhara kwa tabaka la ozoni na adhari zake hutokea kwa binadamu, mimea na viumbe hai.

Amezitaja athari za uharibifu wa tabaka la ozoni kuwa ni kuongezeka kwa magonjwa ya saratani ya ngozi,uharibifu wa macho maarufu kwa jina la mtoto wa jicho, na upungufu wa uwezo wa mwili kujikinga na maradhi. Athari hizi kwa kiasi kikubwa zinatokana na shughuli za kibinadamu kama vile matumizi ya kemikali haribifu na zisizo rafiki kwa mazingira.

Bw. Kulwijila amewataka wanahabari kutoa elimu zaidi kwa wananchi juu ya athari hizi ikiwa ni pamoja na kuiomba Serikali kudhibiti uingizaji wa majokofu yaliyotumika. Jitihada za Uhifadhi wa tabaka la ozoni umetokana na utekelezaji wa Mkataba wa Montreal na Vienna ambayo Tanzania iliridhia mwaka 1993.

Warsha hiyo imeratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais imehusisha washiriki kutoka, Chuo cha ufundi VETA - Mwanza na Kigoma, wanahabari, Maafisa mazingira wa Mkoa wa Mwanza na mafundi mchundo kutoka viwanda mbalimbali vya Jiji la Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2012

    AMA KWELI NI MAFUNZO KWA VITENDO:

    Ukali wa baridi la Kiyoyozi, Fundi Mchundo wa Viyoyozi na Majokofu anateseka!

    Hadi Ustaadhi aliyevaa kibaragashia picha ya pili kutoka juu amekaa kulia usingizi umempata kwa baridi kali la Kiyoyozi !

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2012

    AMA KWELI NI MAFUNZO KWA VITENDO:

    Ukali wa baridi la Kiyoyozi, Fundi Mchundo wa Viyoyozi na Majokofu anateseka!

    Hadi Ustaadhi aliyevaa kibaragashia picha ya pili kutoka juu amekaa kulia usingizi umempata kwa baridi kali la Kiyoyozi !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...