Mchezaji maarufu wa mpira wa kikapu na anyechezea ligi ya NBA ya Marekani , Hasheem Thabeet akiongea na waandishi wa habari (hawako pichani) kuhusu kliniki ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Sprite itakayofanyika katika viwanja vya Don Bosco, Upanga Dar es Salaam kuanzia Ijumaa Juni Mosi 2012.
Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) Michael Maluwe akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani)kuhusu ya kliniki ya vijanai chini ya umri wa miaka 17 itakayofanyika katika viwanja vya Don Bosco, Upanga jijini Dar es Salaam kuanzia Ijumaa Juni Mosi mwaka huu. Kliniki hiyo imedhaminiwa na Kampuni ya Coca-Cola kupitia kinywaji cha Sprite. Katikati ni mchezaji wa Ligi maarufu duniani ya NBA Hasheem Thabeet na kulia ni Meneja Bidhaa Msaidizi wa Coca-Cola Tanzania Warda Kimaro.

Sprite, moja ya vinywaji maarufu vya kampuni ya Coca-Cola leo imetangaza kudhamini kliniki ya mchezo wa kikapu kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 itakayofanyika kwenye kiwanja cha Don Bosco, Upanga, jijini Dar es Salaam kuanzia Ijumaa juni 1hadi June 2, chini ya mchezaji wa kimataifa wa mchezo huo Hasheem Thabeet.

Zaidi ya vijana 200 kutoka mikoa sita watashiriki kliniki hiyo ambayo itatoa mafunzo ya awali ya mchezo wa kikapu kama vile kumiliki mpira na kutoa pasi. Katibu mkuu msaidizi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini Michael Maluwe amesema kuwa washiriki watatoka mikoa ya Mwanza, Mbeya, Dodoma, Kilimanjaro, Arusha, Unguja na Pemba.

“Tunashukuru kupata fursa hii ya mafunzo ya awali kwa vijana ambao kusema kweli ndiyo uti wa mungongo wa maendeleo ya mchezo wa kikapu hapa Tanzania”, amesema Maluwe na kupongeza juhudi zinazofanywa na Coca-Cola kupitia Sprite za kudhamini shughuli za maendeleo ya mchezo wa mpira wa kikapu.

Hii ni mara ya pili kwa Sprite kudhamini kliniki ya kikapu kwa vijana chini ya ukufunzi wa Hasheem Thabeet. Kliniki kama hii ilifanyika mwaka 2010 kwenye uwanja huo huo wa Don Bosco na kushirikisha zaidi ya vijana 200 kutoka Dar es Salaam na mikoa mengine.

Thabeet ni nembo ya mafanikio katika mchezo wa mpira wa kikapu na ni mchezaji pekee kutoka Tanzania kuwahi kucheza kwenye ligi maarufu duniani ya NBA. “Najisikia fahari kupata fursa kama hii, kwa mara nyingine tena, ili kuweza kuwafundisha na kuwahamasisha vijana kucheza mpira wa kikapu. Naamini baadhi yao watachomoza kuwa wachezaji nyota siku za usoni”, alisema Thabeet ambaye yuko nchini tayari kuendesha kliniki hiyo.

Kwa upande wake, Meneja Mzaidizi Bidhaa wa Coca-Cola Tanzania Warda Kimaro amesema: “Sprite inajisikia furaha kupata nafasi hii ya kusaidia maendeleo ya mchezo wa kikapu na tunaamini kwamba kliniki hii ya Hasheem Thabeet itawasaidia vijana kuelewa vitu msingi katika maendeleo ya mchezo wa mpira wa kikapu”.

Sprite ilianza kudhamini mchezo wa mpira wa kikapu hapa nchini tangu mwaka 2010 na tangia hapo imeweza kudhamini shughuli mbali mbali za kikapu ikiwa ni pamoja na mashindano ya vijana mikoani, mashindano ya kanda ya tano, mechi za timu ya Marekani AND1 ambao walikuwa hapa nchini mwezi uliopita na kucheza mechi za kirafiki katika mikoa ya Mwanza, arusha na Dar es Salaam kwa udhamini wa Sprite.

Mbali na kudhamini mashindano, Sprite pia imesaidia kuboresha viwanja wa mchezo wa mpira wa kikapu katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Dodoma, Mbeya, Mwanza, Arusha na Kilimanjaro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2012

    "Mchezaji maarafu" sio umaarufu mzuri kwa namna hiyo

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2012

    Hongera Hasheem. Je unaangalia Playoffs? Off season hii nadhani unajifua na trainer kujiweka sawa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2012

    Ahsante saaana Bwana kaka Hasheem Thabeet !!!

    Fanya jitihada uwawezeshe nduguzo nao wafikie ulipo wewe, pia la zaidi wape mwongozo wa kufanya mambo kwa tija na malengo!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 29, 2012

    Kazi nzuri ndugu Hashim lakini akina Charles Barkley,Shaq , na Hakeem Olujuani wanakusubiri ukapige kambi nao.
    24th pick in the 2008 NBA Draft, Serge Ibaka, anafanya mambo makubwa,tunataka tukuone ukirusha bendera yetu kama Ibaka.

    Maoni yangu tu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 29, 2012

    Michuzi, na we bwana wakati mwingine unakera sasa. Huyo hasheem huku Marekani wala hajulikani kama nyie mnavozania na wala si maarufu kwani huyo ni bench warmer (muulize tu), kakuambia nani kama yeye ni maarufu? Kila timu anayecheza anatemwa wakati wenzake wanachuma pesa yeye anashushwa, je umewahi kujiuliza kwa nini anashushwa? Acha kumbeza mwana wa watu ndo nyie mnafanya ajiskie anajua kucheza kumbe mnamuharibia.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2012

    Bwana Thabeet tunafurahi kuona unafanya huduma za kijamii huko bongo, lakini la mhimu zaidi ni wewe kuyatumia mapumziko haya kuongeza kiwango.Umedisapooint sana kwa miaka yako mitatu ya kwanza na ukiendelea kuspendi summer breaks bongo kuuza sura huna future nzuri NBA. Unatakiwa kuwa unafanya mazoeszi na watu kama akina Mutombo, Hakeem NK na sio kufanya fushion shows bongo.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 30, 2012

    Hana lolote huyo atawadanganyeni nyie msio mjua na kujifanya kwake kiswahili akijui anaongea kama mzungu aliyezaliwa London. Iyo ni sawa nakuchukua mwalimu aliyeishia la saba kwenda kufundisha A level

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...