Na Mary Ayo.

 Shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kwa jina la Springs of
Hope –Tanzania lenye makao yake makuu Mjini hapa limefanikiwa kuelimisha jumla ya watu 120 waishio kwenye mazingira magumu ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo jinsi ya kuweza kuanzisha miradi midogomidogo ili kujikwamua na hali ngumu ya kimaisha  waliyo nayo.

Kutolewa kwa elimu hiyo kunafanyika katika maeneo mbalimbali ya mkoani
hapa, huku wakilenga zaidi jamii iishiyo katika mazingira magumu kutokana na kuwa  wengi wao wakishindwa kuwasomesha watoto wao kutokana na ugumu wa maisha walio nao hivyo kuwaozesha ili kupunguza
gharama .

Akizungumza na mtandao huu , Kiongozi wa vikundi  hivyo kutoka  shirika
hilo ,Linus Hokororo  alisema kuwa mbali na kutoa elimu hiyo wameweza  kuwaelimisha kuunda vikundi vya watu 30 kwa lengo la kuweza  kukopeshana mikopo midogomidogo  pamoja na kuwawezesha wao kuunda
mfuko wa jamii  utakaowawezesha wao binafsi kujitatulia changamoto  mbalimbali za maisha , ikiwa ni pamoja na  kuwasaidia wao kuanzisha
saccos yao wenyewe bila kusaidiwa na mtu yeyote.

Alisema kuwa, baada ya elimu hiyo tayari jumla ya vikundi vinne vyenye 
idadi ya watu 120 vimekwisha undwa huku wakiweza kuchangishana fedha  na kuanzisha miradi midogomidogo pamoja na kuweza kujiwekea akiba yao
 kwa ajili  ya kuwasomesha watoto wao ambao wengi wao wamekuwa wakibakia majumbani tu kutokana na ukosefu wa ada.

‘Sisi tulifikia uamuzi wa kufanya hivi baada ya kuona kuwa, jamii
nyingi zimekuwa zikipata magonjwa mbalimbali ikiwemo ukimwi kutokana na kuwepo kwa umaskini, hali inayowapelekea kuingia kwenye vishawishi
mbalimbali, hivyo kwa kufanya hivi elimu hii imewawezesha kuwatoa kwenye mazingira magumu na kuweza kujiinua kuichumi kwa ujumla.’alisema  .

Aliongeza kuwa, katika kufanikisha shughuli zao wamekuwa wakiwezeshwa
na wahisani mbalimbali ikiwa ni pamoja na  East Africa Adventure  Safari company ambao waliwapatia masaada wa kiasi cha USD 360 kwa ajili ya kutoa elimu hiyo kwa jamii itokayo kwenye mazingira magumu.

Aidha alisema kuwa , elimu hiyo imewafikia watu waishio mazingira
magumu kutoka kata ya Bwawani, Oldonyosambu, Muriet  , kata ya Suye , Tengeru, Kimandolu na Sanawari.

Hokororo alisema kuwa, watu hao wametokea halmashauri ya Arusha 
vijijini, halmashauri ya Meru na manispaa ya Arusha huku wakiendelea  kuongeza maeneo zaidi kulingana na watakavyoendelea kufanya uchunguzi  na kubaini maeneo yenye uhitaji huo.

Aliongeza kuwa, lengo hasa la kutoa elimu hiyo ni kuwawezesha watu 
watokao mazingira hatarishi kuweza kujikimu kimaisha na kuondokana na  hali ngumu ya maisha wanayokabiliana nayo kwa kujiwezesha wao wenyewe
baada ya kupatiwa elimu hiyo.

Mbali na kutoa elimu hiyo kwa jamii hiyo pia wameweza kuokoa jumla ya 
watoto 50 watokao mazingira hatarishi ambao waliwahi kuachishwa shule  kwa kutaka kuozeshwa na wazazi wao, huku wengine wakishindwa kuendelea
na masomo kutokana na hali ngumu ya maisha ikiwa ni pamoja na wengine  kupata mimba za utotoni.

Aidha wanafunzi hao wamekuwa wakisomeshwa bure na shirika hilo kuanzia 
kidato cha kwanza hadi chuo kikuu lengo ikiwa ni kuhakikisha watoto  hao wameweza kujitegemea na kuondokana na hali ngumu waliyokuwa nayo .

Ambapo wameweza kuwalipia fedha  kiasi cha milioni 15 kwa ajili ya 
kuwasaidia watoto hao katika kuwalipia ada na mahitaji mbalimbali  waliyonayo huku wengi wa watoto hao wakiendelea kuongezeka na kuhitaji  misaada zaidi.

Pia wameweza kuwapeleka Nursery watoto waishio mazingira magumu kwa  
kuwajengea shule yao iitwayo Make a Different Foundation ambapo hadi  sasa hivi ina jumla ya watoto 36 wanaosomeshwa na shirika hilo huku wakiwalipia kiasi cha milioni 6 kwa mwaka.

Aidha shirika hilo, baada ya kutoa mafunzo kwa jamii hiyo iishiyo
mazingira magumu na kuweza kujitegemea baadaye ndio wanatoa msaada wa  kuwaongezea mitaji ili biashara zao ziweze kukua zaidi.

Naye mwezeshaji wa mafunzo hayo , Aisha Hussein alisema kuwa, amekuwa 
akiifundisha jamii hiyo itokayo kwenye mazingira magumu kwa muda mrefu sana huku akikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya wengi wao kuendelea kuwa maskini kutokana na kuwa hawana uwezo kwa kukopa banku kwani riba ni kubwa sana.

Ambapo hali hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa sana jamii nyingi 
kuendelea kubakia maskini kwani hawana uwezo huo lakini kupitia mafunzo hayo wengi wao wameweza kuondokana na hali ngumu ya maisha na
kuweza kuanzisha miradi yao midogomidogo kwa kukopeshana wao kwa wao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...