habari za kazi, 
siku moja niliona Tangazo la nafasi za kazi kwenye Libeneke letu hili Pendwa la Globu ya Jamii na kuvolunteer katika NGO ya Mercy corps, kilichotakiwa ni kutuma cv tu, lakini katika kufuatilia kwangu niligundua kuwa kuna dalili za utapeli katika mtu huyo aliyetoa tangazo hilo.
1. baada ya kumtumia cv alisema nafasi za kazi zipo Nacargua America ya kusini kwa hiyo ukipata kazi watakulipia ticketi ya ndege, watakupa malazi, na nauli ya kila siku ya kwenda na kurudi kazini ila unachotakiwa kuchangia ni work permit ambayo ni usd 197 tu.
2.Kisha alinitumia barua ambayo inanijulisha kuwa nimepewa offer ya kazi kwa hiyo nitumie sh 315,200 ambazo ni sawa na usd 197 ambapo kiasi hiki cha pesa nilitakiwa nideposit katika account moja katika benk ya stanbinc.
Query yangu.
  • unawezaje kupata work permit kabla ya kupata hata visa?
  • unawezaje kupata work permit bila mtu kujua hata passport namba yako?
  • iweje wewe kuchangia kiasi kidogo cha pesa dola 197 wakati wao wanaweza kukulipia  tiketi bei kubwa na mshahara alisema dola 1850
maoni
hao ni matapeli wanataka kuliza watu kwa kutumia Globu ya Jamii ambayo ni itaweza leta kashfa kuwa kuonyesha kuwa Globu ya Jamii inashirikiana nao hao watu,wajihadhari na watu hao
nimefanya utafiti wa hali ya juu nikagundua hilo kama unataka details zaidi naweza kukutumia emails ambazo alinitumia
kazi ni kwako.
ANGALIZO LA GLOBU YA JAMII KWA WADAU
Kwanza kabisa tunatoa shukrani za dhati kwa mdau alietuletea taarifa hii kwani kwa namna moja ama nyingine itawafungua macho watu wengi ambao walikuwa hawajalibaini swala hili ambalo hata Globu ya Jamii ilikuwa haijalitambua.
Neno la Globu ya Jamii katika leo hii na siku zingine zijazo,ni kwamba haihusiani kabisa na hiyo NGO ya Mercy corps ambayo ilituma tangazo lake la kutafuta wafanyakazi hapo Juni 21 na ukweli ni kwamba NGO hiyo iliweza kutumia moja ya kauli mbiu za Globu ya Jamii ambayo inasema hatubagui na wala hatuchagu kwani atae tuzika hatumjui,hivyo ujumbe huo ulifikishwa kwetu nasi tukaiwasilisha kwenyu.

Hivyo tunaomba kutoa angalizo hilo ili kila mmoja wetu aweze kufahamu.

Glogu ya Jamii.
Hedi Kota.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 28, 2012

    hata mimi nilimfatilia mtu uyo kwa karibu akasema anaitwa lilian joseph kisanga na ni mtanzania.chakushangaza je huko hakuna watu wa kufanya kazi kama adm,clerks na kadhalika?watanzania tumekuwa watu wagumu kutambua mambo

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 28, 2012

    Pole sana mdau hapo juu. Hata mimi nilishakumbwa na hao matapeli ila bahati nzuri nikawashtukia. Maana no Interview No chochote. Na ukitaka kuongea nao wanakupigia.

    Mi niliongea na hilo tapeli mwanamke anayejiita Country representative anaitwa Mary Kibona. Akaniambia nafasi ipo South Sudan.

    Mimi waliniambia nika-deposit Diamond Trust Bank. Ki ukweli sio watu wazuri. Hilo tangazo la kazi nililikuta kwe website ya Mwananchi. Mbayaaa. Sharlyn

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 28, 2012

    Kweli kabisa...mjumbe hauwawi....

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 28, 2012

    DUNIA NZIMA IMEFILISIKA:

    Watanzania tuelewe ni tatizo la nchi zote za Dunia nzima kuhusu suala la kazi au ajira, sio Marekani sio Uingereza na Ulaya nzima.

    Hivyo msitegemee kuona mambo kama ajira au kazi kirahisi rahisi, ni muhimu mfikirie sana ajira Binafsi za kujitegemea zaidi kuliko kuingizwa mikenge kama hiyo.

    1-MJITEGEMEE KWA AJIRA BINAFSI.

    2-JIJENGEENI UWEZO NA KUJIAMINI.

    3-KUWA UMEAJIRIWA AU KAZINI SIO NDIO UHAKIKA WA KUFAFIKIA MALENGO YA KIMAISHA.

    ZINDUKENI!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 28, 2012

    Watanzania wengi wetu tuna maradhi mabaya ya kupenda kuajiriwa.

    Angalieni mtu anasoma hata kama akiishia Daraza la Saba anatarajia kuajiriwa!

    Mtu anamaliza kidato cha nne au cha sita hata Taaluma hana anawaza kuajiriwa!

    Walio katika Vyuo vya Elimu ya juu ndio kabisa wengi wao ukiacha wenye asili ya Ujasiriamali, wengi wao hata ukute aliyehitimu masomo ya Biashara ktk ngazi ya Shahada hawana uwezo hata wa kuendesha Kiosk cha Soda!

    Sasa kwa mazingira hayo haya ya kutapeliwa kazi na vibarua yasitukute?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...