Napenda kuwatangazia wana-Bumbuli kwamba ile ahadi niliyotoa wakati wa kampeni – ahadi ya kuanzisha Shirika la Maendeleo Bumbuli – imetimia.  Shirika limepata usajili, limefungua ofisi, lina watumishi wa mwanzo na tayari ipo miradi minne ambayo utekelezaji wake utaanza mara moja. Tutazindua Shirika hili tarehe 4 Agosti 2012, katika mkutano wangu na wana-Bumbuli waishio Dar es Salaam na mikoa ya jirani, na baadaye katika mikutano na wananchi jimboni Bumbuli. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 09, 2012

    OPEN LETTER TO ALL TANZANIANS.....

    HIVI NDIYO TUNAVYOTEGEMEA KUTOKA KWA WABUNGE SIYO MAMBO YA KINA MAIGE KWENDA KUNUNUA JUMBA LA DOLA LAKI SABA AMA TABIA YA KINA SUGU KUZUNGUKA ZUNGUKA TU MIKOANI HUKU WAKIIMBA NYIMBO ZA MATUSI ZA BONGO FLAVA AMA KINA SUMARI KWENDA MAREKANI NA KUUZA SURA KUPIGA MIPICHA NA KUPAMBA BLOGS. JANUARY UNA MAWAZO MAPYA AMBAYO WABUNGE NA WATANZANIA KWA UJUMLA WALIO WENGI HAWANA WALA HAWAYAJUI. TUNGE PATA WATU WENGI KAMA WEWE TANZANIA INGEKUWA MBALI SANA LAKINI KWA SABABU AKILI YA WABUNGE WENGI IKO KWENYE TAMAA YA PESA KULA BIA NA STAKE WENGINE KUHARIBU WATOTO WADOGO NINA WASIWASI WATA KUPIGA VITA SANA. NIMEKUFUATILIA SANA KWENYE MAMBO MENGI NIMEONA UPEO WAKO NI MKUBWA SANA MIMI SITOKI BUMBULI LAKINI NINAPENDA MAENDELEO YA WATANZANIA AS A LARGE NINAKUUNGA MKONO NITACHANGIA KIASI CHA DOLA 400 KWA KUPITIA NJIA ULIZOZIWEKA. WATANZANIA IMEFIKA WAKATI TUWE NA MAWAZO YA UTAIFA KULIKO UMIMI. NAKUTAKIA KILA LA HERI JANUARY NA MUNGU AKUJALIE MEMA, WATANZANIA TUJITOKEZE KWA WINGI KUCHANGIA HAYA MAENDELEO SIYO HARUSI NA KITCHEN PARTY TU AMA OFA ZA POMBE NA NGONO.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 09, 2012

    Mh. January unachowaandalia wana Bumbuli ni kwa kuona jinsi mkulima anavyoteseka na kilimo halafu mwisho wa mavuno hambulii chochote Matunda yanaoza Tanga kwa kukosa viwanda vya kusindika kiasi kwamba mkoa umegubikwa na umaskini wakati Rslimali zipo Amkeni wana Bumbuli mpeni sapoti Mbunge wenu ambaye kati ya wengi ameanza kuonyesha ahadi zake kwa vitendo MUNGU AKUBARIKI KTK MIPANGO YAKO ili kuinua Taifa kiuchumi na umeonyesha wazi kuwa wewe siyo mchoyo unakula na watu wako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...