Natumaini tunaweza kukubaliana kuwa sera yoyote hupimwa ufanisi wake kwa kuzingatia inatekelezwaje mkabala na mahitaji ya uanzishwaji wake.Hakuna sera isiyokuwa na lengo, lengo likitimia ndipo tunapoweza kubaini  kuwa sera imefaulu au imeshindwa. 

Dhana na lengo la mifuko ya hifadhi ya jamii ni kuwakinga wananchi (wafanyakazi wa umma, binafsi, walioajiliwa na waliojiajili) dhidi ya matukio yasiyo tarajiwa  maana ambayo ni bayana. 

Lakini tukumbuke kuwa, neno “jamii” katika sera hii linatuvuta kuangaliazaidi ya mteja wa mifuko ya hifadhi ya jamii, lakini pia watu na taasisi zinazowazunguka ambazo  kwa njia moja au nyingine huweza kuathiriwa na matendo ya mteja  wa mifuko ya hifadhi ya jamii, hii ndio maana mifuko mingi ya hifadhi ya jamii hutoa mafao kadhaa kwa ndugu wa karibu wa mteja kama watoto na warithi wengine wa mteja huyu. 

Je, wajua kuwa tasisi za kifedha hutoa mikopo kwa wafanyakazi kwa kutegemea mifuko ya hifadhi ya jamii ikiwa mteja atapatwa na janga lolote lenye uwezo wa kumfanya  ashindwe kulipa deni lake kwa kukatizwa kipato chake au kifo?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Makala nzuri lakini uchanganyaji wa R na L wengine hautuvutii kusoma.

    sesophy

    ReplyDelete
  2. Umejitahidi lakini all in all withdraw benefit kwanza hayo mengine baadaye!!

    ReplyDelete
  3. Haya mambo ya "Kunguru" kuandika "KUNGULU" yanatowa raha na hamu yote ya usomaji. Tushindwe kwenye kutamka, thus fine, maana sometimes mtu anaweza kuwa affected na "dialect" inategemea na sehemu anayoishi. Lakini basi hata kwenye kuandika tunashindwa kuitambuwa ( L ) ndio ipi na ( R ) ndio ikoje jamani??!!!

    Ukijifunza lugha ya kiarabu ni rakhisi sana kuweza kutofautisha kati ya LAM ( ل ) ambayo ni sawa na herufi 'L' na na RAA/REE ( ر ) ambayo ni sawa sawa na herufi 'R' na inakuwa vigumu sana kuathirika na 'Dialect'. Lamsingi tujaribu kuzingatia umuhimu wa herufi tunapotamka na khasa kwenye kuandika ili tusipotoshe maana iliyokusudiwa.

    ReplyDelete
  4. mimi hii siiamini hata kidogo nchi hii imejaa wanyonyaji kila kona ya nchi,makala inaeleza vizuri na ni mambo ambayo yanaweza kutia matumaini kidogo,lakini tatizo hapa ni kitu kimoja kumekuwa na mambo mengi sana mazuri ambayo yamekuwa yakihubiliwa juu ya nchi hii lakini hatuyaoni hii ni sawa na kuwaaminisha watu wakawa na matumini na wakasubiri sanaaaa lakini mwisho wa siku ni uongo na utapeli,suala la kujitoa liwe hiari ya mtu na wala si sheria ya mamulaka husika,wafanyakazi wenyewe kujitoa kwa muda mfupi ama laah hii iwe ni hiari watachagua wenyewe endapo wataona faida ya mifuko ya jamii,kama vile kuwepo na mikopo ya hela,kukopeshwa nyumba n.k na hata kama mikopo itakuwepo iwe katika mazingira ya wazi na si rushwa na usumbufu usiokuwa wa lazima.

    ReplyDelete
  5. Hili halina tofauti na lile suala la watumishi wote wa Serikali kulazimishwa kuingia katika Mfuko wa Bima ya Afya, bila kujali kama mwenza (mume/mke) naye ni mtumishi wa Serikali au la.

    Ni wizi wa kimachomacho kwa kuwa kila mtumishi anakatwa 3% ya mshahara wake kwa ajili yake na watu wengine wanne katika familia yake au tegemezi.

    Wapo watumishi wengine wa Serikali ambao, kwa bahati nzuri waume au wake zao wanafanya kazi katika taasisi, mashirika ambayo siyo ya Serikali na wanao pia utaratibu wa Bima za Afya. Lakini Serikali haijali hilo, bali ni lazima ukishaajiriwa tu uingizwe kwenye Mfuko wa Bima ya Afya, upende au usipende!

    Na siyo kwamba Serikali haiwezi kupata taarifa za watumishi wake wa aina hiyo, la hasha! Ni wizi mtupu!

    Hakuna Bima huko duniani za kulazimishana. Bima zote zinatakiwa kuwa za HIARI. Endapo mtumishi ataachana na mkewe ambaye ana hiyo Bima nyingine, basi awe huru kujisajili na Mfuko wa Bima ya Afya kuanzia wakati huo.

    Twaelewa kuwa hii nchi inahitaji fedha, lakini siyo fedha za wizi kama hizi. Ndiyo maana pamoja na utajiri tulio nao bado yapo mambo mengi ambayo yanakwenda kombo, ni kutokana na DHULUMA kama hizi.

    Naweza kuandika hadi kesho mifano ya wizi wa namna hii lakini nahofia kuboa wadau. Hivi ni waalimu wangapi hapa nchini wanajua kuwa fedha wanazokatwa kwenye mishahara yao kila mwezi zinajengea majengo kama Mwalimu House pale Ilala? Jengo hilo lina gorofa nane, na kodi ya space kwa floor nzima sio chini ya TShs. Milioni 130 kwa mwaka! Hivi waalimu wa nchi hii, wanafaidika vipi na pesa hizo??? Mama yangu mzazi alichangia sana jengo hilo lakini alifariki kabla hata ya kupata senti moja ya mradi huo wa Mwalimu House.....imagine???

    Dhuluma, dhuluma, dhuluma kila upande, nchi itapona kweli hii????

    ReplyDelete
  6. Huku kuchangaya "L" na "R" ni kutokana na lugha za makabila. Hata "Z" na "S" wapo wanaozichanganya (masiwa badala ya maziwa nk). Dawa si kusoma kiarabu ila waalimu wa lugha wajitahidi kuwasaidai wale wenye matatizo kama hayo

    ReplyDelete
  7. Ni somo zuri. Asante kwa elimu hii sasa nimeelimika kuliko wabunge wetu wanavhobwabwaja bila kutuelewesha kwanza washka dau wao. Shida ya Tz yetu ni 1 tuu. Rushwa. Hakuna hata 1 alie mwema.

    ReplyDelete
  8. Davis MuzahulaAugust 09, 2012

    Naomba radhi kwa wale waliopata shida ya kuchanganywa kwa herufi kwenye makala hiyo hapo juu. Nakiri kuwepo kwa tatizo hilo. Lakini pia naomba mnipe pongezi yangu kwa kuandika makala hii kwa kiswahili kwa maana vyano vyote nilivyo tembelea vilikuwa kwa lugha za kigeni hasa kiingereza.Nitafanya urekebu wa tatizo na makala ijayo itakuwa bora zaidi.
    Nashukuru kwa changamoto hiyo, na pia kwa kuwa na tabia ya kusoma makala kwani inatujenga kimtizamo na kimawazo. Asante

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...