Najitokeza ili kuelezea hali ilivyo kwa sasa katika maeneo ya Yangeyange, Mvuleni Kitonga Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala, eneo linalopakana nalo la Tambani, Manispaa ya Mkuranga, Pwani na maeneo ya jirani yanayozunguka maeneo haya.

Kumeibuka na kushamiri vitendo vya uhalifu wa kutisha vikiwemo vya uvamizi wa maeneo ya ardhi, uporaji wa mali, kudhuru mwili kwa vipigo, kushambuliwa na unyang’anyi wa kutumia silaha.

Kwa miongo kadhaa iliyopita, wenyeji , wamiliki wa maeneo na wakazi wa maeneo haya walikuwa wakiishi kwa amani na usalama bila ya wasiwasi wa maisha yao na mali zao, lakini kwa miaka ya hivi karibuni na hasa baada ya baadhi ya wahamiaji wenye asili ya Kanda ya Ziwa kuhamia maeneo haya, kumekuwa na wimbi kubwa la uhalifu wa kutisha kwa kutumia silaha za jadi na hata silaha za moto ikiwemo bunduki zinazomilikiwa kinyume cha sheria.

Taarifa za uhalifu zipo wazi kwa Wenyeviti wa Serikali za Mtaa wa Mvuleni Kitonga na hata ofisi ya Kata ya Msongola upande wa Manispaa ya Ilala. Aidha, taarifa kama hizo zipo za kina kwa upande wa Serikali ya Tambani kwa upande wa Mkuranga, Pwani. Taarifa hizi zinajumuisha pamoja mambo mengine ikwemo vinara wa uhalifu, wafadhili na washirika wao wa uhalifu, waathirika, majeruhi, uharibifu wa mali na baadhi ya hatua zilizochukuliwa.

Wapo wananchi waliojeruhiwa kwa kukatwa miili yao kwa mapanga, kuvunjwa viungo vyao na pi walionyang’anywa mali kwa silaha. Pia Magari yameharibiwa kwa kushambuliwa na kupondwapondwa na mengine kuvunjwa vioo. Yapo maeneo ya ardhi yaliyoporwa kwa nguvu na mazao kuharibiwa, nyumba kubomolewa na vifaa kuporwa ilimradi tu kwa ufupi hali ni mbaya kwa wananchi wa Yangeyange, Mvuleni Kitonga, Msongola, Tambani na maeneo ya jirani.

Hali hii imepelekea wananchi wa maeneo haya kushindwa kufanya shughuli zao za kawaida za kila siku kutokana na genge hili la wahalifu kudiriki kuzuia wananchi kupita baadhi ya maeneo kwa kile wanachodai kuwa wameyateka na yako chini ya himaya yao. Kwa hivi sasa wananchi wa maeneo haya hujifungia ndani ifikapo saa 12:30 jioni kutokana na hali ya hatari iliyotanda.

Jitihada mbalimbali zimechukuliwa na wananchi ikiwemo kutoa taarifa kuanzia ngazi ya mjumbe, Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa, Kata na hadi vituo vya Polisi vya Sitakishari kwa upande wa Ukonga, Ilala na Mkuranga kwa upande wa Pwani na baadhi ya hatua kuchukuliwa lakini bila ya mafanikio na kwa hatua ya kuwasilisha tatizo hili kwenye vyombo vya habari ni dhahiri hali ni mbaya sana.

Genge hili la wahalifu linajiimarisha kila kukicha. Lilianza kwa silaha za jadi vikiwemo visu, mapanga na marungu hatimaye wakatumia pinde, mishale na mikuki na sasa wanatumia bunduku za moto wanazopiga hovyo hususan nyakati za usiku wakiwa wanasherehekea ushindi wa uhalifu wao dhidi ya polisi.

Wananchi waliochoshwa na hali hii walidiriki kumueleza kinagaubaga Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya kipolisi ya Mkuranga (OCD) katika mkutano uliofanyika eneo la Kitonga tarehe 8, Juni 2012 kuwa ikiwa Jeshi la Polisi limeshindwa, wananchi wajulishwe wazi ili wachukue sheria mkononi dhidi ya kadhia hii. Kamanda aliwasihi wananchi kutulia na Jeshi la Polisi litachukua hatua. Lakini matatizo yanaongezeka kila kukicha.

Haiyumkini kuwa Jeshi la Polisi lililo na jukumu la kulinda usalama wa raia na mali zao, kushindwa na genge la wahalifu wachache wanaotembea vifua mbele wakitamba kuwa wao ni wababe kwa polisi.

Raiamsongola
Msongola
Dar Es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mssisubiri polisi wala mwemyekiti jiandaeeni wananchi wote pangeni mikakakti yenu muwe na silhah za moto wavamieni na kuwacharanga wote na kama wana nyumba chomeni moto waungulie ndani wote msimuache hata mtu mmoja hai hakikiksha wote wamekufa ndilo suluhisho ya usalama wenu.Jiungeni na shirikiaeneni kwa pamoja kumaliza tatizo hili.Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.Nasubiri mtekeleze maoni yangu.

    ReplyDelete
  2. Polisi wetu wana hujuzi wa kuzuia maandamano zaidi. Poleni walazi wa Msongola.

    Mgewaambia Chadema wana mkutano au wanaandamana mgeona ma defender na washawasha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...