Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe
UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), naomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu lipokee, lijadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kutumia fursa hii kukupongeza wewe binafsi kwa kuliongoza kwa umahiri mkubwa Bunge hili la Bajeti la mwaka 2012/2013.  Napenda pia kuwapongeza Mheshimiwa Job Ndugai (Mb.), Naibu Spika na Waheshimiwa Wenyeviti wanaokusaidia kuongoza Bunge hili kwa kazi nzuri wanayoifanya. 

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee nachukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa uongozi wake mahiri wa Serikali ya Awamu ya Nne. Chini ya uongozi wake Taifa letu limeendeleza utamaduni wetu wa kudumisha amani, utulivu na mshikamano. Nawaomba Watanzania wote tuendelee kudumisha hali hiyo ili kuimarisha umoja wetu ambao ni tunu isiyopatikana kwa bei yoyote.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Dr.Patrick NhigulaAugust 07, 2012

    Michuzi,

    After reading Hon.Membe budget, I think two important areas were not included in his budget:

    1.Education
    2.Healthcare

    My question is as follows: why his ministry is not involved in healthcare and education projects?

    ReplyDelete
  2. Thank you Minister Hon. Membe,

    What about Malawi's allegations on demanding Lake Nyasa ownership?

    If Malawi demands this despite that they are out of point regarding internatinal laws on world's water bodies, can please start it to incalculate Tanzania to demand 'fully onwership' of Lake Tanganyika?

    How much money in the Budget have you set aside on tackling 'a Malawi's most serious quagmire'???

    We need to know please!!!

    ReplyDelete
  3. If Malawi demands Lake Nyasa, Now due to basis of name can also we Tanzania who we were formally know as Tanganyika start to demand ''full ownership'' of Lake Tanganyika?

    ReplyDelete
  4. Kuna mdau hapo juu anasema Mhe Membe hazungumzia Health Care na Education kwenye hotuba yake. Hivi hayo mambo mawili kweli yamo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa? Na kama ni kweli nini basi majukumu ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na ile ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi?

    ReplyDelete
  5. Dr. Patrick NhigulaAugust 07, 2012

    Dr. Nhigula,

    Hon. Membe budget touched in depth projects like energy, agriculture, diaspora, etc...but why we have forgotten human resources and healthcare which are very important components when it comes to economic development for any nation.If we are not investing in human resources we will continue having investors come in our country and running companies and we will have low end positions. we need to talk about education and healthcare!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...