Tufumbe macho tuombe kwa jina la Mungu Baba,
Nyoyo zetu zisiyumbe, tutazame msalaba,
Tusifu tena tuombe, Yesu wetu wa mahaba,
Hii ni nusu karne, Igogwe Hospitali.

Tangu ilipoanzishwa Igogwe Hospitali,
Sana tumefurahishwa wa Karibu na wa mbali,
Maisha yamerefushwa kwa matendo na kauli,
Hii ni nusu karne, Igogwe Hospitali.

Hii ni nusu karne, umri umetimia,
Nia ni watu wapone, ili wapate afia,
Maradhi waje wapime, maisha yawe murua,
Hii ni nusu karne, Igogwe Hospitali.

Heko majirani nyote, Igogwe eneo zuri,
Kuilinda mali yote, pasiwepo na hatari,
Mila, desturi zote, kwenu zizidi shamiri,
Hii ni nusu karne, Igogwe Hospitali.

Ziende kwake pongezi yule Padre Mellsoni,
Jitihada za uwazi kutafuta masikani,
Na hatimae ujenzi, hongera sana misheni,
Hii ni nusu karne, Igogwe Hospitali.

Katoliki ni dhehebu, la kiroho na kimwili,
Watu wapate thawabu, wamjue Mungu kweli,
Maombi na matibabu, elimu pia injili,
Hii ni nusu karne, Igogwe Hospitali.

Umma umenufaika kuwepo hospitali,
Vipimo vya kusifika, wataalam mbalimbali,
Maabara imeboreka, hongera kwa kutujali,
Hii ni nusu karne, Igogwe Hospitali.

Huduma mmeitoa pasipo dini kujali,
Eneo wala jinsia, kabila hata imani,
Mzidi kuendelea, awabariki Maanani,
Hii ni nusu karne, Igogwe Hospitali.

Waganga na wauguzi sifazo zawamulika,
Vipimo vyenye mionzi kwa wagonjwa hitajika,
Tumepata ukombozi kwa wakati muafaka,
Hii ni nusu karne, Igogwe Hospitali.

Kituo chetu yatima, watoto wanalelewa,
Waliofiwa na mama, mahitaji wanapewa,
Afya zao wanapima, lishe wanahudumiwa,
Hii ni nusu karne, Igogwe isonge mbele.

Basisita, bapatili, ndaga fijo mukulwasya,
Bakundwe mwe babombeli, abonywa mukubakasya,
Muli ni kisa naloli, buno mukubatetesya,
Finja kalongo bahano, ikipatala kya Igogwe.

Tutwale ubonywa bwetu, tungifisaga kukaja,
Kukupimigwa bagwetu, fiki bamo tukufuja,
Ubukimwi mbungo jetu, ngulalusya ba kukaja?
Finja kalongo bahano, ikipatala kya Igogwe.

Ukyala akisajege, ikipatala kikiki,
Nkyeni kyendelelege, ku bandu kije kifuki,
Abandu baponelege, basimanyege isoki,
Finja kalongo bahano, ikipatala kya Igogwe.

©Daudi Lugano Kilindu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...