Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( aliyesimama) akitoa maelekezo kwa Wajumbe wa Kamati za Sensa ngazi ya Wilaya zote sita za Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kati kati walioonesha mgogo) akiendesha kikao cha tathimini ya maandalizi ya sensa kimkoa.

Picha/Habari na John Nditi wa Globu ya Jamii,Morogoro

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, aliongoza kikao cha Mwenyeviti wa Kamati za Sensa za Wilaya sita za Mkoa huo ,zikiongozwa na Wakuu wa Wilaya hizo.

Pia Kamati hiyo zimewajumuisha Waratibu wa ngazi ya mbalimbali na tathimini hiyo ilifanyika Augost 4, mwaka huu, katika ukumbi wa Manispaa ya Morogoro.

Sensa ya Watu na Makazi imepangwa kufanyika siku ya Augost 26, mwaka huu na kila Wilaya iliwasilisha taarifa yake juu ya maandalizi yalivyofikiwa, maeneo ambayo bado hayajafikiwa na kuweka mkakati wa kuyafikia kabla ya siku hiyo sambamba na kiwango cha uhamasishaji kuangia ngazi ya Mkoa hadi Vitongoji na Mitaa.

Mkuu huyo wa Mkoa katika msisitizo wake , amewataka Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri zote sita na waratibu wao kuongeza nguvu zaidi pamoja na kujenga ushirikiano ili kuzikabili changamoto zitakzokuwa mbele yao kwa lengo la kufanikisha zoezi hilo kwa kiwango cha asilimia 100.

Tayari baadhi ya Wilaya zinaendelea kutoa uhamasishaji juu ya umuhimu wa kuhesabiwa siku hiyo kupitia maigizo na utoaji wa burdani kutoka kwa vikundi mbalimbali vya wasanii.

Pia Mkuu huyo wa Mkoa alitumia fursa hiyo kuwataka watendaji hao wa ngazi ya Wilaya , kuwahamasisha pia wananchi wajitokeza kutoa maoni ya uundwaji wa Katiba mpya wakati tume ya kuratibu maoni itakapokutana na wananchi wa maeneo hao muda muafaka utakapowadia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...