Zoezi la sensa limeendelea kufanyika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma na Wilaya zake kwa siku ya pili mfululizo.

Taarifa kutoka kwa Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya zimeeleza kuwa hakukuwa na taarifa kutoka kwenye maeneo yao zilizoripotiwa juu ya uhalifu na hujuma dhidi ya zoezi la Sensa.

Kwa upande wa Vifaa, asubuhi ya Leo ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri walikuwa wameomba kuongezewa baadhi ya vifaa hususani Madodoso na baadhi ya Fomu kwa ajili ya kuchukulia na kuandikia taarifa mbalimbali zinazochukuliwa kwenye zoezi hilo la Sensa.

Nae Mratibu wa Sensa wa Mkoa wa Dodoma Bw. Idd Muruke amesema kuwa wameendelea kupokea vifaa zaidi kwa ajili ya zoezi hilo kulingana na mahitaji ambapo alfajiri ya leo baadhi ya vifaa kama madodoso yameendelea kusambazwa/kupelekwa kwenye baadhi ya maeneo yenye kuhitaji ambapo kwa kazi ya leo na kesho vinatosheleza na vitaendelea kuingia kulingana na mahitaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hivi kwa nini chokochoko zote za shari duniani huwa zinaanzia ktk DINI hii?

    ReplyDelete
  2. Kwa kuwa wengi wao wanatumia akili zao wenyewe na sio za kutumwa na baba zao au viongozi wa dini zao. Penye dosari wao wanaingalia kama dosari sio kwa makengeza.

    sesophy

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...