Na Abdulaziz video
Zoezi la kufukua  Maiti za watu waliofunikwa na kifusi katika Machimbo ya Madini katika Kata ya Nandagala Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi jana limekamilika leo asubuhi  ambapo  maiti zote 7 zilipatikana.

Akiongea na Globu ya Jamii eneo la tukio, Diwani wa Kata hiyo, Bw. Andrew Chikongwe alibainisha kuwa kazi ya kufukua kifusi hicho imechukua muda mrefu kufuatia na kuwepo kwa zana duni za kufukua Mchanga hali iliyofanya kazi hiyo kuwa Ngumu kuanzia jana saa 9 jioni hadi leo asubuhi

Chikongwe aliwataja Marehemu hao ni Nyang'ana Mkelecha,Mkazi wa Musoma, Mohamed Omari Fondogoro, Mkazi wa Morogoro, Bakari Liganga mkazi wa Chunyu Ruangwa, Rajab maarufu ROGER Mkazi wa Musoma, Uwesu Bakari Abeid mkazi wa Rondo, Chakoda Mkazi wa Dar na Rashid Ally maarufu kama BADE Mkazi wa Masasi, mkoani Mtwara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...