Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bashir Awale (kulia) akisaini hati za makubaliano ya kimkakati na Meneja Mkuu wa Wateja wa Makampuni wa Benki ya Biashara na Viwanda ya China (ICBC), Jiang Tao (kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi Kampuni ya madini ya Tanzania China Mineral Resources inayoundwa kwa pamoja kati ya kampuni ya kichina ya Sichuan Hongda na Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Zhao Daoquan jijini Dar es Salaam juzi jioni. ICBC inamiliki asilimia 20 ya hisa katika benki ya Standard ya Afrika Kusini benki mama ya Stanbic Tanzania.
Balozi wa China nchini, Lv Youqing akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bashir Awale katika hafla ya utiaji saini hati za makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati kati ya Stanbic, Benki ya Biashara na Viwanda ya China ya ICBC na Kampuni ya madini ya Tanzania China Mineral Resources inayoundwa kwa pamoja kati ya kampuni ya kichina ya Sichuan Hongda and Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC). Kulia ni Rais wa ICBC, Yang KaiSheng ambayo inamiliki asilimia 20 ya hisa katika benki ya Standard ya Afrika Kusini benki mama ya Stanbic Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...