Akisalimiana na mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Ruvuma Daud Masiko ambaye pia ni kamanda wa takukuru mkoani Ruvuma.
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kushoto,akisalimiana na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernad Membe  katika uwanja wa ndege wa Songea wakati Waziri huyo alipooongoza ujumbe wa wataalamu kuangalia mpaka kati ya Tanzania na nchi jirani ya malawi katika ziwa nyasa ambapo kumekuwa na mvutano kati ya nchi hizo mbili juu ya uhalali wa umiliki wake
  Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernad Membe akisalimiana na Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki kabla ya kutembelea ziwa nyasa jana kuangalia mpaka kati ya Tanzania na Malawi ambao umeleta mgogoro mkubwa juu ya nani mmiliki halali kati ya nchi hizo.
 Baadhi ya wananchi  katika kijiji cha Lituhi wilaya mpya ya Nyasa mkoani Ruvuma wakimsikiliza Waziri wa mambo ya nje Bernad Membe hayupo pichani kuhusiana na mzozo ulipokati ya Tanzania na Malawi juu ya mpaka katika ziwa Nyasa.
 Mkuu wa Brigedi ya kusini Songea Kanali John Chacha akisamiliana na Waziri wa Mambo ya nje  na ushirikiano wa kimataifa Mhe. Bernad Membe mjini Songea.
 Wananchi wakimsikiliza Waziri wa mambo ya nje Bernad Membe hayupo pichani kuhusiana na mzozo ulipokati ya Tanzania na Malawi juu ya mpaka katika ziwa Nyasa.
  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akizungumza na wazee wa mji mdogo wa Lituhi wilayani Nyasa hawapo pichani juu ya ufahamu wao kuhusu mpaka halali wa nchi mbili za malawi na Tanzania uliopo katika ziwa nyasa Katikati Waziri wa mambo ya nje Bernad Membe.
  Mzee Gidion Ndembeka kulia akimuonesha Waziri wa mambo ya nchi za nje Bernad Membe kitabu chenye mipaka halali kati ya Malawi na Tanzania iliyopo ndani ya Ziwa Nyasa.
Mzee aliyefahamika kwa jina moja la Ngatunga akizungumza jana wakati wa ujumbe wa wataalamu kutoka Serikalini ulipotembelea ziwa nyasa wilayani nyasa Ruvuma ili kupata ushahidi wa mmiliki halali wa ziwa nyasa ambalo limeziingiza katika mgogoro Malawi na Tanzania.
Picha na Muhidin Amri. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Suala la Mpaka Tanzania/ Malawi:

    Hawa Malawi wasituchangenye kabisa juu ya suala hili.

    1.Je, kwa nini ile sehemu ya chini walipogawana ziwa na Msumbiji nako hawadai kama ziwa lote ni lao wanakuja kudai upande huu tunako pakana zziwa na sisi Tanzania?

    2.Kwa nini Malawi waegemee zaidi Mpaka waliopewa na Mkoloni wao Mwingereza ambao umekuja baada ya Mjerumani hapo nyuma kuuweka mpaka ndani ya maji?

    Kama issue ni kuegemea Mkoloni na sisi Tanzania tunaegemea ktk Mpaka aliotoa Mkoloni wetu Mjerumani wa mpaka kuwa ndani ya maji, kama Malawi wataegemea mpaka wa Mkoloni wao Mwingereza.

    3.Je ndugu zetu akina John Komba na wengine ktk ufukwe wa ziwa wanaoshi kwa uvuvi ziwani tutawabebaje kimaisha baada ya kuliachia ziwa looote kwa Malawi?

    4.Sioni sababu kwa nini wasitumiwe Majeshi kuchapwa wakati Vikosi viko tayari na ma Bosi tunawaoona hapo?

    ReplyDelete
  2. Jamani wazee wa Nyasa wanastahili pongezi kwa usafi na utanashati.

    ReplyDelete
  3. Ee bwana, yaani ukimtazama huyo Kanali unasikia raha na usalama tele.
    Hongera Membe, keep them busy hadi Joyce ajute kuwaruhusu watu wake kuingilia mipaka. Hivi yule Banda tuliyemnyamazisha hakuwa baba yake na huyu Joyce kweli?

    ReplyDelete
  4. Swala la ziwa nyasa,hakuna cha mjerumani wala mwingereza kwani waligawana AFRIKA kama vile hakuna binadamu wanaoishi,kwa kifupi ni kwamba WAMALAWI kama wanataka vita kirahisi basi waendelee kung`ang`ania mpaka.Mbona Waingereza kisiwa cha FALKLAND kilichopo Argentina wanasema cha kwao mpaka huko wapi?na walipigana vita wakashinda na bado wanakilinda .Watanzania kwa hili mimi niko tayari kuvaa gwanda niende huko kulinda mpaka kwa hali na mali.HAKUNA UTATA KIMPAKA

    ReplyDelete
  5. Ni swali zuri sana la kujiuliza:

    Huyu mama Joyce Banda anaetaka kuendelea na Uraisi wa Malawi huku akiwa na dalili 100% za Udikteta, kwa nini asidai sehemu ya ziwa Nyasa analopakana na Msumbiji(tena wamegawana kati kwa kwati) leo aje kudai huku kwetu?

    Au kwa ukarimu wetu na ucheshi wetu wanatuchukulia kama Mzee Jangala ili wapate ziwa kwa ubwete ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...