Taswira ya jinsi gani baadhi ya watu wasio waaminifu wanavyofanya hujuma katika Shirika letu la Tanesco.Hizi ni nguzo zilizoibwa na kufichwa maeneo ya kigamboni Jijini Dar es salaam na kufichuliwa na wafanyakazi wa Tanesco.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Sasa ktk hili picha gani tunapata?huyu alieficha haya magogo ana malengo gani, kuni?kujenga nyumba?au ndio hao wajulikanao kama vishoka wakitumia miundombinu ya tanesco kujinufaisha?makubwa haya tena la kustaajabisha alieyagundua ni mtanesco.

    ReplyDelete
  2. TANESCO WENYEWE WANAJUA ZILITOKAJE KWAO WAAACHE KUTUTANIA, WAMEDHURUMIANA KATIKA MGAO TUU HAKUNA JINGINE.

    ReplyDelete
  3. HAWA WANAJUA KILA KITU WAMEDHULUMIANA MSHIKO HAWA ZILITOKAJE MIKONONI MWA TANESCO ACHENI KUTUFANYA WAJINGA BANAAA.

    ReplyDelete
  4. Nilikumbana na swala hili mwanzoni mwa miaka ya 2000 kabla umeme kufika Ugindoni, Kigamboni. Ziliitajika kama nguzo mbili tatu kufikisha umeme eneo nililokuwa tukifuatilia. Basi tukataharifiwa na bosi wa Tanesco kwenye ofisi tuliyokuwa tunafuatilia kuwa tatizo la wizi wa nguzo linafanywa na wafanyakazi wenyewe wa Tanesco. Utakuta wafanyakazi wa eneo moja la tanesco wanaiba nguzo kutoka kwenye eneo lingine na kuenda kuwawekea wateja wao walio "wawezesha". Uzuri ni kuwa at the end of the day zinatumika kwa lengo lililokusudiwa ila bila utaratibu kwasababu ya rushwa. Kwahiyo hizi zinaweza kuwa zimeibiwa ofisi ya kinondoni maana kuna watu kigamboni wametoa pesa zaidi kwa wafanyakazi wa tanesco ili wawekewe kigamboni na utakuta ofisi ya TMK labda imeishiwa nguzo au zilizopo zipo kwenye utaratibu maalumu wa kugaia watu kwa folini

    ReplyDelete
  5. Kaficha nani na kafichua nani? Si hao hao Tanesco!!!!

    ReplyDelete
  6. ALAFU KIGAMBONI KAMA MDAU WA 4 ALIVYOSEMA NA MTU NAMJUA AMELALAMIKA SANA MTAANI WAMECHANGA PESA WAMEPELEKA TANESCO WAMEDAI WATAWAWEKEA NGUZO NA UMEME WAKAGERESHA MAGOGO TU YAMEkAA MUDA YAMEPUNGUA WAKIENDA KULALAMIKA WANaZUNgUSHWA MWISHO WAMEWEKEWA NGUVU YA UMEME NI NDOGO SANA NA MWENGINE ANADAI ALIWALIPA WAFANYAKAZI TANESCO KUFUATILIA WAKAMWAMBIA FUNDI KAFaRIKI AkAWAULIZA KAMA KAFARIKI NYIE HAMUWEZI KUMALIZIA? KUMBE MATAPELI AMBAO WANATOKA HAPOHAPO TaNESCO WASHAZULUMIANA NDIO WANACHONGEANA NA TANESCO WASHAANZA KUSIKIA TETESI ZA MAKAMpUNI YA UMEME NDIO WANAKUJA NA STYLE ZA KUJIKOSHA.

    ReplyDelete
  7. Ama kweli Bongo Tambarale!

    Lakini suala hili la kuingilia Mamlaka ktk Mchakato wa utendaji wake ili kujinufaisha tatizo hili lipo sehemu nyingi Duniani.

    Mfano Italia maeneo ya Kusini mwa nchi pana Koo au Familia ambazo hudhibiti migawo ya huduma muhimu na kukusanya makusanyo kama Serikali hivyo unakuwa huilipi Mamlaka (Serikali) isipokuwa unaulipa Ukoo/au Familia wakati miundombinu imewekwa na Mamlaka ya Serikali!

    Mifano ya huduma zinazopokwa kwa staili hiyo ya Kimafiosi kwenye Familia hizo Italia Kusini ni ktk huduma kama:

    1-Usambazaji wa maji safi na ukusayaji wa maji taka.

    2-Usambazaji wa Umeme.

    3-Usambazaji wa huduma za mawasiliano ya simu na intaneti.

    4-Huduma za barua na vifurushi.

    5-Huduma za Bima za Matibabu.

    6-Huduma za Kiserikali kama Vitambulisho na Hati muhimu.

    7-Ukusanyaji wa Kodi ya Serikali.

    Sasa kutokana na kukomaa kwa Rushwa na Ufisadi inafikia Huduma nyeti muhimu zinazowekwa na Mamlaka za Kiserikali lakini makusanyo ya mapato yanaelekezwa ama kuzifikia Koo za hawa Majambazi wa Kimafia wa Kiitaliana, huko ndiko mambo kama haya ya Tanesco Kigamboni yatakavyochukua taswira baadae kama yakiachiwa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...