Itakumbukwa kuwa wakati wa Mkutano wa
Nane wa Bunge uliofanyika kuanzia Juni - Agosti, 2012, Spika wa Bunge aliunda
Kamati Ndogo ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kuchunguza tuhuma zilizokuwepo
kuwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na baadhi ya Wabunge
walijihusisha na Vitendo vya rushwa wakati wa mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya
Wizara ya Nishati na Madini (2012/2013).
Hivyo, Tangazo hili linatolewa kuuarifu
Umma kwamba Kamati hiyo Ndogo imekamilisha kazi yake kama ilivyoelekezwa kwenye
Hadidu za Rejea na kukabidhi Taarifa ya Uchunguzi huo kwa Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano tarehe 27 Septemba, 2012.
Kwa
mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Spika atatoa muongozo kuhusu
utaratibu wa kufuata kuhusu uwasilishaji wa Taarifa hii Bungeni ambapo yaweza
kuwa Spika akatoa uamuzi ama Kamati kuwasilisha Taaarifa hiyo Bungeni.
Spika atatoa taarifa ya kukamilika kwa
uchunguzi huo Bungeni wakati wa Mkutano wa Tisa wa Bunge unaotarajia kuanza
tarehe 30 Oktoba, 2012.
Hata hivyo baada ya Kamati hiyo kumaliza
kazi yake baadhi ya wananchi, wanasiasa na vyombo vya habari vimeanza kuchambua
na kuchapisha maudhui ya taarifa hiyo. Kitendo
cha kuchambua na kuchapisha maudhui ya taarifa hiyo katika vyombo vya habari ni
kinyume cha sheria na kinaingilia uhuru, haki na madaraka ya Bunge kwa mujibu wa
Kifungu cha 31(1)(g) cha Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, SURA 296 (the Parliamentary Immunities, Powers and Privileges Act, CAP 296).
Kifungu
31(1)…Any person who-
(g) publishes, save by the general or
special leave of the Assembly, tiny
paper report or other document prepared
expressly for submission to the Assembly before
the same has been laid on the Table of
the Assembly;
...
shall be guilty of any offence and shall on conviction
be liable to a fine not exceeding five hundred thousand shillings or to
imprisonment for a term not exceeding three years or to both such fine and
imprisonment.
Kifungu hiki kinakataza mtu yeyote
kuchambua na kuchapisha taarifa ya Kamati kabla ya taarifa hiyo kuwasilishwa
Bungeni. Ikithibitika kuwa taarifa hiyo imechahapishwa wahusika wanaweza kulipa
faini isiyozidi shilingi laki tano au kifungo kisichozidi miaka mitatu au vyote.
Hivyo natoa rai kwa umma kuwa tuache Bunge
lifanye kazi yake kwa mujibu wa Katiba, Sheria na Kanuni.
Job Yustino Ndugai, (Mb.)
NAIBU SPIKA
25 Oktoba, 2012
Kifungu hakikatazi chochote bali kinasema ukichapisha utakumbana na faini na/au kifungo. Kwa hiyo ni uamuzi wa mtu kuchapisha ama la.
ReplyDelete