Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk (kushoto)akiwa pamoja na Balozi Mdogo wa China aliekuweko Zanzibar Chen Qiman (katikati)wakati Balizi huyo alipofanya ziara ya kutembelea vyombo vya Habari vya Serikali ya Zanzibar.kulia ni Mkurugenzi wa Zbc Radio Rafii Haji. PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
 Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk akibadilishana mawazo na Mhariri Mkuu wa Gazeti la Zanzibar leo Abdalla Mohd hapo katika Ofisi za Zanzibar Leo Rahaleo Mjini Zanzibar.
 Mhariri Mkuu wa Gazeti la Zanzibar leo Abdalla Mohamed akimuonesha nakala ya Gazeti la Nuru lililokuwa likitolewa Zanzibar Balozi Mdogo wa China aliekuweko Zanzibar Chen Qiman wakati alipofanya Ziara ya kutembelea vyombo vya Habari vya Serikali ya Zanzibar.
 Balozi Mdogo wa China aliekuweko Zanzibar Chen Qiman (wakatikati)akizungumza na baadhi ya watendaji na wakuu wa Gazeti la Zanzibar leo wakati alipofanya Ziara ya kutembelea vyombo vya Habari vya Serikali ya Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Yussuf Omar Chunda(kushoto) akitoa maelezo kuhusiana na Utendaji wa Idara yake kwa Balozi Mdogo wa China aliekuweko Zanzibar Chen Qiman (kulia)wakati alipofanya Ziara ya kutembelea vyombo vya Habari vya Serikali ya Zanzibar.


Na Ramadhan Ally
-Maelezo Zanzibar 

China imeahidi kuendeleza azma yake ya kusaidia sekta za habari nchini kwa kuwapatia Mafunzo wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Balozi mdogo wa China aliyepo Zanzibar bibi Chen Qi Man ameeleza hayo alipofanya ziara ya kutembelea vyombo vya habari vya Serikali ikiwemo Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC),Shirika la Magazeti na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

Bi Chen amesema mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu yataongezwa kwa wafanyakazi wa vyombo hivyo katika fani za uandishi wa habari,ufundi na utawala ili kuimarisha utendaji kazi wa vyombo hivyo.

Amezitaka taasisi hizo za habari kuandaa wafanyakazi wanaostahiki kupata mafunzo hayo hapo mwakani kwa mujibu wa fani zao.

Akizungumzia suala la Mtambo wa kuchapishia magazeti ya Shirika la Magazeti la Zanzíbar,Bi Chen amesema amewasilisha ombi hilo kwa Serikali yake ambapo kwa sasa wanasubiri jawabu kutoka Serikali ya China.

Mapema Mhariri Mtendaji wa Shirika hilo Abdulla Mohammed amemuelezea Balozi huyo mdogo kuwa wana mpango wa kuanzisha Gazeti la Kingereza lakini wanashindwa kutokana na gharama kubwa za uchapaji unaofanyika huko Dar es Salaam ambapo mtambo huo haupo Zanzibar.

Kwa upande wake Waziri wa Habari,Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya China kwa misaada mbalimbali inayotoa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Sekta mbalimbali ikiwemo ya Habari.

Amemuelezea Balozi huyo kwamba kwa sasa Shirika la Utangazaji Zanzibar limo katika kipindi cha mpito kutoka Mfumo wa Analojia kwenda Dijitali kuanzia mwezi Januari hivyo watendaji wa Shirika hilo wanahitaji mafunzo zaidi katika mfumo huo mpya.

Aidha amemuelezea Balozi huyo kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaandaa Sherehe kubwa za kutimiza miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambazo zinatarajiwa kuhusisha mashindano ya mpira wa miguu kutoka timu mbalimbali za Taifa hivyo amemuomba Balozi huyo kuanza maandalizi ya kuiarifu timu ya Taifa ya China kushiriki mashindano hayo mwaka 2014


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. balozi kavaa jeans!! balozi yuko kwenye ziara ya kikazi lakini amevaa kama anakwenda sokoni au saluni??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...