Description: C:\Users\rmtingwa\Desktop\NEW LOGO.JPG
Dar es Salaam 4 Oktoba, 2012 … Huduma mpya ya Supa Cheka kutoka vodacom imevuta mamilioni ya Watanzania kutumia huduma hiyo.
“Hii ni ishara kuwa wateja wetu wanahitaji kupata huduma za intaneti masaa 24 na kutuma SMS kwa gharama nafuu. Watanzania sasa wamejiunga katika ushindani wa matumizi ya intaneti… hii italeta mabadiliko  makubwa katika mawasiliano ya simu,” alisema Rene Meza, Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania.
Huduma ya Supa Cheka inayopatikana kwa wateja wa malipo ya awali  imeleta msisimko katika soko…”Tumeshuhudia mamilioni ya wateja wakitumia intaneti kuperuzi na kupokea taarifa ikiwa ni siku moja tu baada ya kuzindua huduma hii. . Hii ni ajabu sana supacheka inawavutia wateja kweli kweli ,” alisema Meza.
Wateja watapata MB 50  kwa shilingi 400 katika Supa Cheka hii itawawezesha:  kutumia facebook  kwa muda wa wiki , kupata  muda wa maongezi wa dakika 30 na SMS 100. Kwa shilingi 300 mteja atapata MB 15 ambayo itampa siku tano za matumizi ya facebook, dakika 20 za maonezi  na SMS 50. Kwa wale watakaochagua shilingi 200,  watapata MB 10 na siku mbili za matumizi ya facebook, dakika 10 za muda wa maongezi na SMS 25.
 “Lengo letu ni kuhakikisha kuwa Watanzania wote wanaweza kutumia data na ndio maana tumeweka kifurushi cha shilingi 100 katika Supa Cheka ambacho  kitawawezesha wateja kupata SMS 10. Wanachotakiwa kufanya wateja wetu ni kupiga *149*01#,” alisema Meza.
Wateja wetu wanatakiwa kutumia fursa hii… bado tunazo huduma na bidhaa nyingi za kusisimua ambazo ni maalum kwa wateja wetu.” Alihitimisha Meza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...