Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2012,wakiwa kwenye picha ya pamoja mchana huu katika kambi yao iliopo kwenye hoteli ya Geraffe,Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.Jumla ya Warembo 30 wameingia kwenye kambi hiyo kujiandaa ya kinyang'anyiro cha kumsaka Mrembo atakaemlithi,Salha Israel ambaye anashikilia Taji  hilo hivi Sasa,ambapo fainali za mwaka huu zitafanyika Novemba 3,katika hoteli ya Blue Peal,Ubungo Plaza jijini Dar.
 Baadhi ya Warembo wa Redd's Miss Tanzania wakibadirisha mawazo wakati wakielekea kwenye chakula cha Mchana wa leo kwenye hoteli ya Geraffe,Mbezi Beach jijini Dar.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa katika mazungumzo na Warembo wa Redd's Miss Tanzania,waliopo kwenye kambi yao iliyopo kwenye hoteli ya Geraffe,Mbezi Beach jijini Dar es salaam leo waliopowatembelea na kuzungumza nao maswala mbali mbali juu ya mashindano hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Mbona waandishi wa habari wote ni wanaumme?

    ReplyDelete
  2. mimi nina ombi au agizo tena naona bora iwe amri kwa sababu sasa imeshakuwa tabu alieagiza kuwa hawa ma miss wote ni lazima wawe wembamba au wamekonda ni nani?
    tanzania imejaaliwa mamiss walionenepa na kuburura matrela ya kila bidhaa kuelekea zambia sasa kila nikisikia mamiss huwa naangalia naona siwaoni hawa kina dada wenye kupendeza na wenye siha kamili juu ya mifupa siongelei kuwa mwembamba kuwa ndio hawana afya lakini sijaona mnunuzi wa ngombe au mbuzi aliekwenda sokoni akarudi na mbuzi aliedhoofika huchagua yule aliyenona ili tafrija ifane sasa katika kutuonyesha urembo wa hawa kina dada basi muwachanganye na wale walionona halafu muone nani atashinda hizo zawadi labda waamuzi wawe wanauguwa macho lakini kama wana vision 20/20 itakuwepo shughuli kumpa kombe mwenye visigino na mifupa ili hali mwenye mguu wa bia yupo.

    salaam.
    mdau.
    nachingwea.

    ReplyDelete
  3. Hahahahaha !

    Mdau wa Nachingwea anonymous wa Fri Oct 05, 01:03:00 AM 2012

    Umenichekesha sana, ni kuwa hawa Waandaaji wameshindwa kuelewa ya kuwa matashi ya watu yanapishana!

    Kama wengine wakipenda Biriani la kupaka, wengine huridhika na Makande kwa kachumbari!

    Kama wengine wakipenda chai ya sukari, wengine wanapendelea Kahawa ya uchungu!

    Ndio maana pana wanaopenda vimbau mbau, wengine wanapemndelea mabonge nyanya!

    Inaonekana hii Timu ya Waandaaji wa Miss Tanzania, ipo upande mmoja.

    Ndio hapo tu.

    ReplyDelete
  4. Jamani ule Mpango wa kurudi JKT vipi?

    Si inaelezwa moja wapo ya azma ya Urembo ni kulitumikia Taifa?

    Nafikiri ingefaa Warembo hawa kuelekea Mashindano yao wangepewa angalau siku 3 za Mafunzo ya JKT au vipi bandugu?

    ReplyDelete
  5. Fri Oct 05, 01:03:00 AM 2012

    Mdau wa Nachingwea inawezekana haya ni mapendekezo ya Waheshimiwa kule Dom dom maana wengi wao ni Madingi sasa wanapendelea kurudia walivyokuwa vijana zamani kwa kuwaona vichekechea hivi!

    ReplyDelete
  6. Mtoa Maoni wa kwanza,

    ...waandishi wa habari wote hapo ni wanamume kwa kuwa kama ujuavyo wanawake wanaoneana wivu na kudharauliana wao kwa wao.

    Hebu fanya utafiti nenda Bar ukiongozana na Mwanamke, kama Mhudumu ni mwamamke asalaleee atamtolea jicho la wivu mwanamke wako!,,,huku mwanamke wako akimdharau Mhudumu ambaye ni mwanamke mwenzie!

    Jaribu kwenda peke yako, ohhh Mhudumu wa Kike jino hadi la mwisho kwa kicheko na tabasabu lake kwako shavu dodo!

    Hivyo sio rahisi kuona Mwandishi wa kike akienda ktk mzingo wa Ma-miss kama huo!

    Ukizingatia Ma-Miss ni Vigoli na Waandihsi wa Kike wengi ni Wamama na Wa dada wakubwa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...